Raia waliouawa na polisi si majambazi-RC

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Raia waliouawa na polisi si majambazi-RC

2009-04-19 21:39:24
Na Charles Ole Ngereza, Arusha


Sasa imefahamika rasmi kwamba raia wawili waliouawa na polisi kwa risasi wakituhumiwa kuvamia kituo cha mafuta cha Mount Meru mkoani hapa na kupora Sh. 100,000, hawakuwa majambazi.

Hiyo imebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isidori Shirika alipotangaza rasmi jana matokeo ya kamati ya uchunguzi wa mauaji hayo yaliyofanywa na polisi dhidi ya raia wawili mwezi Machi mwaka huu.

Katika tukio hilo, Shedrack Motika (22) na Ewald Mtui (36), waliuawa kwa risasi na polisi waliodaiwa kupigiwa simu kuwa kulikuwa na tukio la ujambazi katika kituo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa alisema kuwa tume hiyo imebaini kuwa hakukuwa na tukio la ujambazi lilotokea katika kituo hicho cha mafuta kilichopo katika eneo la Kijenge.

Aidha, Shirima alisema kuwa katika uchunguzi huo, Tume ilipokea maelezo ya wananchi 51 kati yao 33 ni wale waliojitokeza kwa hiari yao kukutana na kamati huku 18 wakiwa ni wale walioitwa mbele ya kamati hiyo.

Shirima alisema katika mkutano na wandishi wa habari kuwa kamati hiyo imeridhika kwamba kuna utata mkubwa katika utoaji na usahihi wa taarifa kuhusiana na tukio hilo.

Alifafanua kuwa kutokana na matokeo ya uchunguzi wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Arusha baada ya kupitia na kuzingatia taarifa ya uchunguzi, imeridhika kuwa taarifa ya uchunguzi huo iwasilishwe katika vyombo vya sheria ili kufanya upelelezi wa kina kwa mujibu wa sheria.

``Tumeona kuwa tukabidhi kwa ofisi ya mwanasheria wa serikali kwa uchunguzi na hatua kuchukuliwa kwa watakaobainika kuwa na makosa,`` alisema Shirima.

Akijibu maswali ya waandishi waliohoji wahusika wa mauaji hayo wako wapi na hatua zipi zitachukuliwa, Shirima alisema kuwa hatma yao itajulikana baada ya ofisi ya Mwanasheria wa Serikali na vyombo vingine vitakapokamilisha uchunguzi.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa hakueleza uchunguzi huo utaanza lini kuchunguza ripoti ya kamati na kumaliza lini.

Pia taarifa hiyo ya Mkuu wa Mkoa iliyokuwa na aya nne tu haikueleza kama kulikuwa na utoaji wa taarifa za uongo na ni hatua zipi zitachukuliwa dhidi ya waliobainika kuidanganya kamati hiyo.

Wakati taarifa hiyo ikitolewa jana, ndugu wa marehemu walikuwa nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakisubiri nini kitasemwa lakini hata hivyo baada ya kupata fununu walidai kuwa watatoa maoni yao kesho (Jumatatu).

Kamati hiyo iliyotoa matokeo hayo iliundwa na wajumbe kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa, ofisi ya mwanasheria wa serikali, mwakilishi wa jamii na jeshi la polisi.

Mauaji ya vijana hao yaliyodaiwa kuwa ya kinyama yalidaiwa kufanywa na polisi yaliyotokea Machi mosi, mwaka huu baada ya mhudumu wa kituo cha mafuta cha Mount Meru kuzozana na marehemu hao.

Katika mzozo huo ambao mhudumu huyo alidaiwa kumtaarifu tajiri yake ambaye naye aliwapigia polisi ambao baadaye waliwaua vijana hao.

SOURCE: Nipashe
 
Huo ni utata mtupu. Watu kuuwawa kwa laki moja tu? je kama polisi waliwaua kwa makosa familia italipwa fidia au ni kuombwa msamaha tu? Inatia huruma, tutauliwa hivi mpaka lini?
 
yaani jamani cjui niseme nini kuhusu hii ishu, hao ndio polic wa ki TZ! ngoja tuone mambo yatavyoendelea, RIP ma bro shed.
 
Kwa kweli ni masikitiko. Tunaomba haki itendeke hapa. Kuanzia kwa mkuu wa kituo cha mafuta aliyieta polisi, mhudumu aliyehusika na askari waliohusika wote hao waisaidie polisi. Hivi kwani mpaka dakika hii hawajakamatwa?? Tusaidieani wenye details. Wanatakiwa wawe wamekamatwa tangu tukio lilipotokea. Period.
 
Nini BONGO?
fuatilia news Uingereza kuhusu maaskari wa Kule walivyowaiga wenzao wazoefu wa Bongo pale inapotokea raia asiye na silaha anapoandamana kwa amani.

..Tatizo lipo hapa
utakuta maaskari wengi ni miongoni mwa wale ambao kwa namna moja au nyingine hawakwenda vidato sana halafu hawa ndiyo wanapewa silaha kulinda nchi baada ya tarining ya ukakamavu kule ccp moshi. sasa tegemea askari aina hii ambaye hata uwezo wake wa darasani si mkubwa anawezaje kulielewa somo la haki za binadamu seuse kuheshimu sheria aliyojiyaminisha kuilinda na kuitetea? pia hata misharaha yao ni midogo na hawalalamiki wala kusumbua maana wamefundishwa KUTII na kukubali kila kitu bila kuuliza na kwa kuwa wengi wamepewa fadhila kujiunga na JESHI hivyo hawezi kumsaliti mjomba au anko wake. Hivyo fastresheni ya mshahara, ufinyu wa kufikiri na kuamua ndipo hupelekea wanafanya miujiza wanapotekeleza kazi zai... UTASIKIA WANASEMA RIRIKUWA RINAPAMBANA NA PORISI TUKARISHINDA thubutuuuu!

Jeshi la polisi linahitaji REFORM ya hali ya juu. si ktk utendaji tu bali ianzie ktk sheria iliyoliunda ili kuboresha huduma zake kuondokana na aibu ya kuuwa walipa kodi wema wa nchi hii. vile vile liondokane na zama za kuwalinda mafisadi liwe jeshi huru ambalo hata DC (katibu wa jumuiya za Chama tawala) asiweze kuwa na amri juu yake. hata RC asiwe na amri ya direct kwa jeshi hili. Reform ianzie kwenye sheria kisha jeshi litabadilika lipende lisipende.
 
Haya mauaji ya Arusha inavyoonekana Serikali inapiga danana tu.

________________________________

Justice delayed is justice denied.
 
Hapo serikali inaposhikwa na kigugumizi..maana mauaji ya uonevu yamezidi sana kwa kisingizio cha uhalifu na ujambazi.....watuhumiwa wakamatwe haraka kabla hawajakimbia...bado Dar tunaisubiria ile report nayo isomwe hadharani haraka muda umeshapita
 
Mbona hakuna waziri aliyewajibika na kashfa hizi??
naamini akiwajibika ndipo zitakoma pia hizi kuuana kwa jina la sheria.
Masha pls for the sake of watanzania na chama step down ili uwe mfano wa kuigwa kama Mwinyi na lyatonga siku zileeee.
au bado hujamaliza fungate lako?
 
Back
Top Bottom