Raia Mwema hatarini kufungiwa makala 'kila awamu ina rekodi ya kuua', mtego kwa JK

sioni ubaya wa hii habari
mbona tv na hata magazeti ya nchi za wenzetu yanaanika uozo uliopo ktk nchi zao?
tupo ktk zama za tecknolojia mpya ule ujinga wa kuziba watu midomo kutoa habari haupo tena
ukizuia gazeti kuandika watu wataandika ktk blogs na mitandao mbalimbali
wanaotegemea habari magaazetini wanazidi kupungua
hawataweza kulifungia.
 
yelekea bado upo ktk zama za mawe
hiyo makala umeisoma au umesoma tu hii barua ukawahukumu wana hatia?
soma hiyo habari upate logic? kuuwa sio lazima uuwe mtu unaweza kuuwa demokrasia pia au uhuru wa watu kupata habari au kuwaziba waandishi midomo ili wasitibue uozo fulani.
kuna maafa yalitokea ndio enzi za utawala wao lkn sio kwamba viongozi hao walihusika
inategema mwandishi ana maana gani.soma hilo gazeti kabla hujawahukumu.

Hili si kufungiwa tu, inafaa wachukuliwe hatua za kisheria kali sana, na wapelekwe mahakamani, mhariri na muandishi wa hiyo makala, na wakishindwa kuthibitisha hizo kauli zao, wafungwe maisha. Hawa ni watu hatari sana na wanaweza kusababisha maafa makubwa sana kwa huu uzandiki wao.
 
..."unajua hii ni hatari sana, maana itakuwa ni sawa na kuisambaza hiyo makala na si kuizuia. Hata wale ambao hawakuisoma sasa wataitafuta na kuisoma...
Jii ni kweli maana hata mimi nimelitafuta hilo gazeti baada ya kupitia post hii, nimelitafuta gazeti mpaka nimelipata. Ngoja niisome hiyo makala
 
Wajaribu kulifungia waone moto utakavyowawakia. Tanzania ya sasa inabadilika kwa kasi kubwa sana

Tatizo la viongozi wetu hawasomi vitabu, wangesoma kitabu juu ya John Kennedy kiitwacho "LET EVERY NATION KNOW' wangejua madhara yanayoweza kuletwa na press censorship!! He regretted later on as to why he gagged the press prior to the BAY OF PIGS invasion!! Katika makala husika mwandishi hajaandika kitu kipya kwa mfano anapotabili kuwa ccm itamfia Jakaya mikono mwake; mbona haya haya ndio yanayosemwa kwenye luninga kila siku na wakina BUTIKU, KITINE,KADUMA NA WENGINE WENGI TU! Kama wana akili they should be thankful kwani inawapa nafasi ya kujirekebisha.
 
Back
Top Bottom