RAI yangu kwa TFF Yanga na Simba

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,488
908
Kwa makumi ya miaka niliyokuwemo DSM, nikiri sijawahi kuhudhuria Mechi uwanjani wala kuangalia mechi si redioni wala luningani na pia huwa nawashangaa watu sana kuwa wapenzi wa mpira. lakini jumamosi ya tarehe 18, nilijikita rasmi kwamba lazima nikautazame "mtanange' wa SIMBA NA YANGA(Sijui kwa nini watu wengi husema Simba na Yanga and not Yanga na Simba):kama wapenzi wa soka wenyewe wanavyosema, hii yote ni kutaka kumfurahisha mzee wangu ambaye ni shabiki sana wa yanga. nakumbuka enzi hizo yanga ikifungwa hom palikuwa hapakaliki, nikataka nione ni kitu gani hasa mzee wetu alikipenda kwenye soka, mapema nikawaagiza raia wanitafutie ticket nikakae pahala ambapo nitaushuhudia mtanange huo, kwa kuwa sikujua viingilio wakaniletea ticket ya 10,000 kwamba hiyo ndio ilikua top, baadae nikagundua kumbe zilikuwepo za 20,000, 7000, 5000, 3000 na nyingine sizijui. Nimegundua mambo mengi sana mazuri na mabaya ambayo napenda nitoe ushauri binafsi kama mzalendo na raia wa kawaida kabisa.

KUFIKA UWANJANI:

Cha ajabu parking ya magari hakuna, protokali ya kuingia uwanjani ni hovyo-hovyo, vurugu kila sehemu, kila mtu anafanya yake, parking is for your own risk, foleni ya kutisha si binadamu si magari, kila mtu ana makelele yake. kuna askari wanazuia watu kuingia na magari unless uwe somebody, kero hii haipendezi, niliposota kwa miguu na kuangalia ndani parking za uwanja ziko tupu kabisa, huu si uungwna, nitoe rai na ushauri kwa TFF ambao nadhani ndio wenye dhamana na uwanja embu waondoe kero hii, ustaarabu upo tu dunia yote, kuwepo na ticket za magari, hata kama ni 10,000 itakuwa vema mtu ukitazama mtanange huku ukiwa na uhakika baiskeli yako iko chini ya uangalizi wa jamhuri. kama haiwezekani basi wajenge sehemu ya parking.

KUINGIA

Kuna Milango miwili ya kuingia uwanjani, watu ni wengi foleni ni kubwa mno hujui ipi inaenda mbinguni ipi inaenda jehanam, hakuna vibao vya matangazo, direction, wala chochote, watu wanajiendea holela labda uwe mwenyeji sana. niliadhimia kwenda jukwaa la Yanga ambalo sikujua liko side gani, ingawa kwa nasibu nilijikuta nimevaa shati la dam-ya mzee, kama nyekundu-flan, ah nikajua hakuna atayejali hilo. Nilipopita getini tatizo la diretions likarudia pale pale, sijui nielekee wapi, masaa yote mtu unauliza uliza tu, jamaa mmoja akanielekeza pitieni njia ya chini, kufika huko askari wanadai kipande cha ticketi kilichobakia na kuingia. nikaona kwa upande wa kulia kuna raia waliolipa 20,000 wanaingia, i blame myself kumbe za 20,000 zilikuwepo?, (sio kwamba nilitaka ticket ya gharama no! kwa kuwa is my first time nilitaka nikione kiwanja na mtanange vema kabisa niliamini may be wale wanaolipa 20,000 ndio wanaokaa pahala bora zaidi ila mwisho wa mechi nimegundua binafsi wale waliolipa 3000, wanaokaa viti vya juu ndo wanafaidi uhondo wote wa mpira na uwanja. mpira ni msisimko asikwambie, lazima uone mpira na Vituko vyote uwanjani zikiwemo mbwembwe za washabiki, ngoma, fujofujo ndio ladha zenyewe, sasa ukiwa chini huku mpaka upindue shingo yako umeshapitwa na vituko, mtu kama inshu ni kuwaona wachezaji kwa karibu mbona viwanja vingi tu huku mtaani tunawaona kwa karibu, siku nyingine nakaa huko juu, najichukulia na kidarubini aaa!!) nashauri TFF waweke vibao vya matangazo, uwanja mzuri wahandisi wameshaujenga kuutunza ni kazi yetu jamani, hata sign boards uwekewe!!

nilipochupa ndani na kupanda ngazi za kuingilia uwanjani nikaona mtu si wa kawaida, mtu amevaa njano na Red, aisee, nikapata msisimko flan, nikajivuta upande wa mashabikli wa simba kwa ujio wa shati langu kama vile linaendana, nikaketi nao hasa sababu kubwa ikiwa ni kivuli kwa sababu kule yanga waliendelea kupata kijua kikali. nikasema nipoe kwanza hapa kivulini may be baade ntaweza kwenda huko yanga mtanange ukianza. Muda si mrefu nikagundua niko sahihi kuketi maeneo yale kwa sababu kule yanga akipita mtu kwa bahati mbaya kavaa red si maneno hayo anatupiwa, huku simba ndio balaa, akatize mtu kavaa njano atanyukwa hata makonde, nikasema kumbe hii kitu iko serious kiasi hiki?! anyway kwa kuwa mie sio shabiki wa timu yoote popote pananifaa.

BIG SCREEN

Kuna big screen Moja tu upande huu nyuma ya jukwaa la simba, hali hii inawafanya Simba kutojua kinachoendelea kwenye Plasma. nashauri kuwe na screen Mbili, moja pande ule wa yanga ili Simba waone kinachoendeleana pili hiyo iliyo upande wa simba ambayo yanga wanaona. kikitokea kituko kwenye big screen unaona wanajangwani wanapiga yowe na baadhi ya wanamsimbazi hawa mpaka wainuke, mfano wakati kombe linatolewa huwezi kuliona unless kwenye big screen, hivo unaona Yanga tu wakishangilia. pili kuna bongemtu mmoja kajifungashia mbwembwe za yanga aliweka pozi kwenye Kombe na kuligusa, sijui alipenyavipi maaskari na walinzi, kamera zikamchukua was too funny. Washabiki wa simba wao mpaka waambie na Yanga 'angaliaaa!!" ndio maskini ya mungu wainuke, wageuze shingo zao, taabu kweli kweli, sometime flap inakuwa imeshaondoka.

WADHAMINI

hii kitu ndio sikuielewa toka nimeingia uwanjani hadi kombe kutolewa. wadhamini wakuu Vodacom, washabiki wa simba na simba yenyewe hawana tofauti ya mavazi. wote wamepiga uzi mwekundu na nyeupe. of course trade mark colour ya Vodacom ni nyeupe na Nyekundu halikadhalika simba. na vijana vijana wengi wa Vodacom wanapitapita mbele as if ni mashabiki wa simba, mtu anayeangalia kwenye luninga inamshangaza sana hii. nawashauri Vodacom, kwenye baadhi ya matukio muwe mnaisaliti rangi yenu kwa muda, vaeni pink, au zambarau kujitofautisha rasmi kwa ajili ya that special day sio zambi kibiashara. Yanga alipompachika Simba bao la kwanza na wale vijana wa voda mashabiklki wa yanga walishangilia , so inaonyesha baadhi ya simba wanashangilia ni sura sio nzuri kwa mtazamaji wa nje.

MATANGAZO;

Very poor sound, matangazo as if mtu anaongelea mtungini, hakuna kinachosikika, uwanja mkubwa kwanini tusiwekeze kwenye sauti nzuri, uhandisi mzuri wa speaker kwa Outdoors ni Line-array system. wakifunga spika 24 tu 12/12 uwanja utakuwa na suti clear na nzuri sana.

VYOO:

hili la vyoo ni la kutisha sana na naliongelea kwa masikitiko makubwa, baadhi ya vyoo nilivyovitembelea ni Vichafu sana sana, vimeziba na watu wanaweka shughuli zao juu ivoivo, Koki nyingi zimeondolewa, maji hakuna ni mambo mabaya ya kutisha sana. jambo hili ningependa TFF walitazame kwa uharaka, nashauri kwamba lazima muamini jamii hazistaarabiki siku moja, lazima wezi wawepo waharibifu wawepo pia. Ufanyike upya uhandisi wa plumbing za chooni, achaneni na koki za kichina, tudesign Koki za stainless steel, ziwe firmly welded na zifanyiwe installation kwamba mtu hawezi kuiba. ile koki unaifunga kabisa kwenye bomba kwa threads na unaiweld a parmanent joint. mtu akitaka kuiba basi abomoe ukuta kabisa, sio hivi vya kichina vya kupachurua tu mtu anaweka mfukoni na kuenda zake. pia kila choo kiwe na mwangalizi ambaye always anafanya usafi, nakumbuka nchi moja choo cha wanaume alikuwepo mwanamke akifanya usafi na wenyeji wala hawastuki, mama anadeki watu wanaendeleza kazi kama kwaida. uwanja ni wetu nani tumtake atutunzie, kwa mwendo huu italazimika watu wawe wanachafua sana mazingira kama hili halitashughulikiwa mapema, wanasema nyumba ni choo, uwanja ni vyoo safi.

MAJUKWAA:

Kuna majukwa yenye viti vya aina tofauti, nilichogundua wale wa 3000,5000, na 7000 wanaingiliana tu, pia nikagundua kule juu zaidi mtu anauona mtananange kwa raha zaidi kwa sababu anauona uwanja na maudhui yake yote. huku chini ni jua, fujo, na mpira unauona kwenye binol angle.

MAWASILIANO:

Kwa sababu ya wingi wa watu mitambo inayolisha wananchi maeneo hayo inazidiwa sana, watu wenye sim za kupapasa ndio hawaopati chochote kabisa. labda makampuni ya cm yalione hili ili maeneo ambayo hukumbwa na mkusanyiko wa watu waweke mtambo wa nguvu.


KUTOKA UWANJANI:

kero, adha ni ile ile, nashauri waandaaji wa pambano kushirikiana na polisi weweke utaratibu mzuri, mech ikiisha magari yaachiliwe kwenye njia moja hadi yanamwagikia jijin. iwepo njia moja. mfano hii ya Chang'ombe mtu akifika huko anatafuta ustaarab wake ama aende ubungo, arudi mbagala kwa njia ya Tandika au aende kariakoo..

MWISHO SI MBAYA NIKAONGELEA MTANANGE WENYEWE.

Frankly Niseme wazi Mpira ulikuwa Hovyo, na niwe mwazi zaidi Mpira kama ni hivi basi ni mambo ya hovyo, yanga ilishinda bao 2-0, lakini mabao yote ni kama ya kubahatisha tu. sio simba wala yanga. Mchezo ni hovyo. wachezaji ni wavivu, hakuna mwenye Ari, wapowapo tu. watu hawajui kabisa kwamba mpira ni ajira lazima aweke bidii. niende mbali zaidi na kusema sio kwamba hawana bidii au ari wanazo, siwalaumu kwa kitu ambacho hawana, wanacho sana. ari, kasi, bidii wanavyo sana ila tu ni uvivu wa kujituma wanaishia kujisukumasukuma tu. nasema hivyo kwa sababu baada ya Simba kukosa penat, kwa dakika mbili tatu nilishuhudia mpira wa kasi, bidii na ari kama mzuka flan umewapanda. kila mchezaji alicharuka ila soon ukapoa tena. kasi kama ile ndio ilitakiwa mwanzo wa mchezo hadi mwisho. tunao wachezaji wazuri sana nisema, kumbe kitu ambacho kinatukwamisha ni uvimu, kama timu zetu zitaonyesha mechi za bidii na kasi sana kama ile niliyoiona baada ya simba kukosa penat kombe la dunia lazima tuwe nalo.

hongera mzee wangu Bihagaze hapo Urambo Tabora, hopely ushindi ulikuburudisha sana, Mungu akupe maisha marefu.

ADIOS.
 
umejitahidi kuandika, ushabiki ni mwingi lakini kukosa upeo(ustaarabu), upenzi wa mchezo kama mchezo haupo na ndio maana hatuendi mbele!
 
kuna kitu kimoja ambacho hujaongelea, ni suala la ulinzi na usalama wa uwanja , ndio siku ya kwanza toka nianze kuingia wanja wa taifa nifika hadi kwenye chumba cha kubadilishia nguo wachezaji, bila kuulizwa na mtu yoyote.

Hii ilitokana na kufungwa kwa kwa mlango wa kuingilia vip A NA B wakanahangaika kutafuta sehemu ya kuingilia kuna mtu akatuelekeza upande ambao lilikuwepo gari la matangazo la super sports naenda hadi pale nikakuta mzee 1 kasimama namuuliza leo VIP B tunaingilia wapi akanionyesha malango naingia nakuta na baridi ya a/c nikaoma mmh ngoja niende labda zipo ngazi nyingine huko na vuka vyumba vimeandikwa vimebandikwa karatasi imeandikwa simba sc, nikastuka huku mbona sio.

Ila nashukulu angalau na mm niliona madhali ya uwanja ule kwa chini kule na ule ukumbi wa mikutano , na kasoro nilizo ona ni aina ya vyumba vya kubadilishia nguo si kama vya wenzetu kule kuna meza kuubwa wanapanga jezi juu, kilicho nisadia ni skafu ya timu yangu ya simba tu.

Pengine walihisi na mm ni mdau au kiongozi wa timu , nikarudi tena nje kuna ka geti hakajafunguliwa vzr ndio unavuka uzio wa vip unaelekeza upande ule nakutana na mapolosi wanachana tiketi za bei ndogo wanakuachia upite mwenye tiketi ya vip ukisogea mbele unawakuta wengine ndio unavuka kuingia vip
 
kuna kitu kimoja ambacho hujaongelea, ni suala

Da hii hatari sana Kwa wachezaji, kuna yule kapwambe aliyesogelea kombe, hadi kuweka pozi, jamaa wa kamera wakamuangazia, he kustuka watu Kwenye big screen wewee!! He kuja kufungua macho Askari wanamwona jamaa kaweka pozi kidogo wampe kichapo, kumbe Kama kuliiba angeliiba zamani Sijui Yanga wangepewa Nini ?.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom