R.I.P Fr. Francis Lyaruu Mketa

Msafiri Kasian

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,133
659
Jana(tarehe 24/08/2012 ilikuwa siku ya mazishi ya marehemu Fr.Francis Mketa wa shirika la Roho Mtakatifu(Holy Ghost Fathers) -Usa River.

Padre huyu alifanya kazi maeneo mengi jimboni Arusha(Kikatiti, Ngaramtoni, Burka,St.Theresa, Usa River etc) na Moshi(St.James Seminary-Kilema, ambapo ndipo alipozaliwa na kusoma pia, pamoja na parokia nyingi kabla ya kuamua kujiunga na shirika la roho mtakatifu).

Mungu alimjalia kuishi miaka 98 duniani(alizaliwa mwaka 1914),moja ya kauli zake za uzeeni alipenda kusema"MIMI NI PANYA WA YESU"

Apumzike kwa amani.
 
Najiuliza,nitafika 98? Mara nyingi alipofikia uzee,alikuwa anaomba kufa kifo chema,hivyo alikuwa anafundisha kwamba;"MKISALI MUOMBE KUFA KIFO CHEMA"
 
Duh ananikumbusha fr. Magafu hi died very early huko musoma. Sitaki maswali.
 
Mungu amjalie pumziko la Miele! Tuliomfahamu, tutakumbuka jitihada zake za kuboresha mazingira- the physical environment in which we live! Aliamini mafundisho ya dini na elimu pasi mazingira stahili ni sawa na sifuri!

Natamani Rais wangu angeiga mfano wa Pd Mketa!
 
Najiuliza,nitafika 98? Mara nyingi alipofikia uzee,alikuwa anaomba kufa kifo chema,hivyo alikuwa anafundisha kwamba;"MKISALI MUOMBE KUFA KIFO CHEMA"
RIP Fr. Francis.
mkuu umenikumbusha hii sala ya kuomba kifo chema. huwa naisali kila siku katika sala za usiku. Nakumbuka nilianza kuisali tangu nikiwa mdogo, kila siku............
 
Back
Top Bottom