PROOF: Video ya Lwakatare Imerekodiwa Lini?

FrankMakange

Member
Jul 7, 2012
9
3
Nimejaribu kupitia mada kadhaa kuhusu video inayodaiwa kumuonyesha Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa CHADEMA Bw. Wilfred Lwakatare akitoa maelekezo ya kumdhuru mwandishi wa habari - na kuona kuwa waanzishaji/wachangiaji karibu wote waliojaribu kutoa hoja kuhusu video hii imerokodiwa lini wamekuwa na jibu moja tu, Desemba 28, 2012. Nafikiri jibu hili limetokana na jina la video hiyo katika YouTube ambalo ni "VID-20121228-00005"

Bila kujali uhalali wa video husika, ENDAPO jina la video hiyo (VID-20121228-00005) ndio sababu/uthibitisho pekee kuwa video hii imerekodiwa tarehe 28-12-2012, basi nafikiri kuna haja ya kuiangalia upya hoja hii kwani jina la video linaweza kuwa lolote lile kutegemea aliyeiweka hadharani video hiyo anataka iwe na jina gani.

Tunaweza kujenga hoja kuwa jina hili limetokana na jinsi kamera inavyotunza na kuzipa data majina, na mhusika amejisahau lakini pia tukumbuke kuwa inawezekana aliyeiweka video hiyo ameamua kubadilisha sehemu ya jina hilo kwa makusudi kabisa.

Hivyo basi (assuming kila kitu katika video hii ni cha kweli) kimantiki nionavyo mimi ni kuwa; Kama aliyerekodi/ajuaye ukweli wa video hii hatasema ukweli kuwa imerekodiwa lini, basi ni vema na ni sahihi kufikiri kuwa video hii imerekodiwa katika kipindi KATI ya "Bw. Lwakatare alipoingia CHADEMA na kuwa na madaraka yamuwezeshayo kuweka mikakati kama ile AU Mwandishi husika alipoanza kuwa tatizo kwa CHADEMA" NA "Siku video ile ilipowekwa hadharani"

IN SHORT:
JINA VID-20121228-00005 SIO UTHIBITISHO KUWA VIDEO IMEREKODIWA TAREHE 28-12-2012
 
Wapii, hawajui kitu ndio maana waliacha ma evidence kibao. FIY camera hutunza data by date.
 
wanajanvi tunakwenda wapi? kama hii CLIP niyakweli tuliachie jeshi la police lifanye kazi yake, kama kunamwanajanvi ambaye anaushaidi zaidi ni bora akalisaidie jeshi la police kitaalam zaidi kuliko kuongea zaidi. shuzi limepata mjambaji.

hivi wewe ni polisi ipi hii unayoiongelea,ni hii ya hapa bongo ya akina kova au itakuwa imechanganyikana na FBI? Skuelewielewi unajua
 
----- jingine! Kula wale akina Riz-One wewe utabaki hivyo hivyo kuwashabikia wezi pamoja na kizazi chako na mtalaaniwa muwe watu wa hovyohovyo hivyo hivyo maishani mwenu mwote!
 
mh jameni hili sakaa sasandio linatamba humu JF, ukitaka threadyako ibambe tu tuia neno la lwakatare humo lazima watu wachangie tu!
mfano...mkwe wa lwakatare akanusha kuwa video si ya mkwewe!
...........lwakatare aamua kufunguka...halaf inside the story unatuuliza sisi wafuatiliaji eti..hivi lwakatare hajasema ukweli wowote mpaka leo? mwenye info atueleze
...........chadema wasema hawakumtuma lwakatare.....halafu ndani ya thread unauliza hivi kweli cdm walimtuma lwakatare? mwenye info atujulishe pls...etc
Yatakuja mengi sana humu kumhusu lwakatare but they are not worth reading! kwa hiyo siyo lazima kila mtu aunde kathread kake...wengine tybaki kuwa wasomaji tu!
 
kwani ni ngumu sana kumfahamu muweka video? si kila kompyuta inayoingia kwenye network huwa ina IP address ambayo ni unique? huoni kwamba kwa kutumia IP address ya kompyuta iliyoweka video hiyo tutaweza kumpata muwekaji wa video hiyo maana tutaweza ku-trace historia ya kompyuta hiyo katika mitandao ya kijamii na hata emails?

je, TCRA hawana chombo cha kurekori na kuhifadhi taarifa za mawasiliano kwa Tanzania? na kama TCRA hawawezi kusaidia kupata IP address na ku-trace history ya hiyo kompyuta, Je, hatuwezi kufunga safari kwenda Marryland ambako kuna chombo kinachohifadhi taarifa za mawasiliano za ulimwengu wote?

mwekaji wa video ndiye atatufanya kujua kwamba video yenyewe imewekwa kwa sababu za kisiasa au uzalendo
 
Magogoni/Hollywood wametengeneza huo mkanda, kodi zetu zinatumiwa kutengeneza filamu za kijasusi. Ngoja niongee na LeMutuz tuanzishe Zeutamu nyingine
 
Sasa wewe ume-prove nini hapa? Kwa utafiti wako,imetengenezwa lini? Tunataka vitu vipya jadilifu...Where is your proof? Jibu badala ya kuuliza
 
wewe ndo siku ya kwanza kuanzisha thread? manake naona hakukua na umuhimu wa kuanzisha thread sababu hamna jipya uloliongea. tarehe haiwezi thithibitisha kama video ni fake au sio fake. mia
 
mh jameni hili sakaa sasandio linatamba humu JF, ukitaka threadyako ibambe tu tuia neno la lwakatare humo lazima watu wachangie tu!
mfano...mkwe wa lwakatare akanusha kuwa video si ya mkwewe!
...........lwakatare aamua kufunguka...halaf inside the story unatuuliza sisi wafuatiliaji eti..hivi lwakatare hajasema ukweli wowote mpaka leo? mwenye info atueleze
...........chadema wasema hawakumtuma lwakatare.....halafu ndani ya thread unauliza hivi kweli cdm walimtuma lwakatare? mwenye info atujulishe pls...etc
Yatakuja mengi sana humu kumhusu lwakatare but they are not worth reading! kwa hiyo siyo lazima kila mtu aunde kathread kake...wengine tybaki kuwa wasomaji tu!

Naunga mkono. MODS tafadhali tengenezeni sticky thread kuhusu hili suala ili kila anayeleta uzi wenye jina la Lwakatare hiyo habari ielekezwe huko. Inabidi tuendelee kuongelea masuala mengine ambayo ni muhimu katika taifa kuliko upuuzi huu.
 
Ngoja na mie nianzishe ya kwangu:

UTHIBITISHO-Mwanamke ahusishwa na video ya Lwakatare.

Alafu ndani yake naelezea jinsi yule mdada anavyoonekana kwy video, thats all. Simtachangia wengi wengi???

Nipeni maujanja basi ya kuanzisha sred.
 
i dont trust even a dead body, from today onwards!! ccm are bunch of cowards!
 
Back
Top Bottom