mustafa ommy
JF-Expert Member
- Feb 8, 2013
- 221
- 127
Na Ashton Balaigwa
Mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
Makamu wa kwanza wa rais wa Serikali ya Umoja wa kitaifa ya Zanzibar, Seif Shariff Hamad, amemtangaza Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao.
Aidha CUF imewatangazia neema Watanzania kuwa endapo itachukua madaraka katika uchaguzi huo itawajaza fedha mifukoni ikiwa ni njia mojawapo ya kuwaondolea umasikini.
Makamu huyo wa kwanza wa rais alisema hayo katika mkutano wa uzinduzi wa oparesheni ya mkachamchaka kuelekea mwaka 2015 (V4C), uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege, manispaa ya Morogoro.
Alisema Profesa Lipumba bado ni kiongozi shupavu anayestahili kugombea wadhifa huo kupitia CUF katika uchaguzi ujao kwakuwa anakubalika ndani ya chama hicho pamoja na kwa wananchi.
Alisema kuwa operesheni za V4C zilizoanza Mei mwaka jana zitaendelea nchi nzima kwa viongozi wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho na wafuasi wake kupita kila kata na wilaya mbalimbali wakihamasisha wananchi kukiunga mkono chama hicho.
Makamu huyo wa Serikali ya umoja wa kitaifa alisema kuwa malengo ya CUF ni kujenga umoja wa kitaifa na kuhakikisha kuwa wananchi wote pasipokujali mwenye nacho na asiyekuwanacho wanapata haki sawa na hizo ndiyo sera za CUF.
Kwa upande wake, Profesa Lipumba, akizungumza katika mkutano huo alisema utatifi uliofanywa katika baadhi ya nchi duniani zikiwamo nchi za Brazil na Mexico umebaini kuwa njia nyepesi ya kumuondolea mwananchi umasikini ni kumpatia fedha taslimu.
Profesa Lipumba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi, alisema jambo hilo linawezekana kufanyika nchini kwa kutumia teknolojia ya simu za mikononi na kuwapo kwa vitambulisho vya taifa vinavyotumia alama za vidole kama alama za ulinzi.
Alisema chama chake kikipewa ridhaa na watanzania ya kuongoza nchi kitatumia raslimali zilizopo nchini za madini, gesi, mafuta, mbuga za hifadhi na maeneo ya utalii kuboresha miundombinu lakini kuwapatia fedha taslimu wananchi ikiwa ni njia rahisi ya kupambana na umasikini.
Ikiwa Profesa Lipumba atagombea tena mwaka ujao, itakuwa ni mara ya tano kwake kwa kuwa amekuwa akiwania nafasi hiyo tangu mwaka 1995 lakini hajawahi kushinda.