Profesa kabudi"watu wasijadili muungano"

prakatatumba

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
1,328
190
Mkuu wa kitivo cha sheria-UDSM profesa Palamagamba kabudi amewatahadharisha watanzania wasijadili baadhi ya mambo ya muungano katka mjadala wa kuandika katiba mpya maana wanaweza kuuvunja,alisema jana jijini Das es salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya kitivo hicho.(source NIPASHE,J.410/OCT/11)
HUYU NAYE MAGAMBA AU YUPO SAHIHI
 
Ni mtazamo wake binafsi na nina amini ana sababu zake za msingi za kuamini hivyo. Lakini mimi naamini kuwa kila kitu ndani ya katiba ni lazima kijadiliwe kinaga ubaga. Muungano ambao unadumishwa kwa usiri hauwezi kamwe kuhimili misukosuko kwa muda mrefu.
 
Anatetea magamba tu,watanzania tunataka katiba mpya,unaposema vitu fulan visijadiliwe hapo unaandaa katiba mpya au unaweka viraka?
 
huyu ni mmoja wapo wa magamba anaye nufaika na system mbovu iliyopo sasa. ndo aliyebeba dhamana ya kupinga mgombea binafsi pale mahakama ya rufaa na ni mmoja wapo wa mawakili wa ccm na mshauri wa sheria ccm makao makuu...hivyo msitarajie mapya kutoka kwake...wasomi ni akina prof shivji , dr lwaitama nk pamoja yakuwa ni magamba lakini wao wametupa minyororo ya uchama na usisi na kujitwisha utanzania
 
Kiboko yake ni prof Maina!
Kabudi ni ms0mi ila ni mlamba nyayo wa politicianz,elim yake haina tija kwa watanzania!
 
huyu ni mmoja wapo wa magamba anaye nufaika na system mbovu iliyopo sasa. ndo aliyebeba dhamana ya kupinga mgombea binafsi pale mahakama ya rufaa na ni mmoja wapo wa mawakili wa ccm na mshauri wa sheria ccm makao makuu...hivyo msitarajie mapya kutoka kwake...wasomi ni akina prof shivji , dr lwaitama nk pamoja yakuwa ni magamba lakini wao wametupa minyororo ya uchama na usisi na kujitwisha utanzania

hawa ndiyo wanaoharibu elimu
 
Haya ndiyo matatizo ya kuingizwa kwenye mfumo, objectivity na academic independence vyote huzikwa. kwa ufupi, huyu ni jamaa ni mlinzi wa mfumo.
 
What a disgrace! Ila tumsamehe tu bure.. After all anaitwa Palamagamba!
 
Ili Muungano uimarike, hauna budi kujadiliwa na kurekebishwa katika katiba mpya. Bila kufanya hivyo, migongano ya kisiasa itaendelea na hatima yake ni kuvurugika kwa amani nchini. Prof. Kabudi angeeleza sababu za kutamka kwa nini muungano usijadiliwe katiaka mchakato wa kutunga katiba mpya.
 
alitoa baseless argument,anasema watu wanaweza kuuvunja na kuchochea vurugu
 
Back
Top Bottom