Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,623
- 19,553
Naomba kufahamishwa zaidi kuhusu huyu Profesa Bingu wa Mutharika. Nilipotafuta biography yake ninaona kama alisoma New Delhi India kipindia kimoja na Malecela akapata masters ya economics, baadaye akajiunga na "Mzumbe Group" ya miaka ya tisini kujipatia Ph.D ya Pacific Western Universty. Amefanya kazi sehemu mbalimbali ikiwamo serikali ya malawi chini ya Banda, UN, COMESA na baadaye kuingia tena kwenye siasa za Malawi hadi alipofanywa kuwa Rais wa Malawi na bwana Bakili Muluzi ambaye baadaye alijutia uamuzi wake wa kumwachoia madaraka jamaa huyu. Sina uhakika sawasawa na siasa za malawi hivyo ninategema kujifunza kwenye thread hii iwapo watatokea wachangiaji wanaojua siasa za malawi sawasawa. Nilichotaka kufahamu hapa ni chuo ambacho jamaa huyu alifundisha hadi kufikia kuwa profesa. Nimejaribu kutafuta publications zozote zenye authorship yake bila mafanikio zaid ya ripoti za kikazi alizoandika akiwa UN na COMESA. Je inawezekana ni kweli kuwa ugonjwa huu hauko Tanzania tu bali Afrika yote?