Prof Magembe akabwa koo na Bajeti kutopitishwa..!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Kutokana na kawaida ya mazoea ya baadhi ya mawaziri kuwa na mazoea ya kuleta bajeti ye nye samari bila takwiku hakiki sasa limemtokea puani Waziri wa Maji Mhe,Prof Magembe!!Wabunge wametupilia mbali itikadi zao sasa wanamsurubu waziri wa maji!!!wamerudi upande wa wananchi na kuwatetea...Kuna nchi 48!Mashirika yasiyo ya kiserikali!!(NGO's)120...nazaidi zinasaidia miradi ya maji..lakini nchi haina maji!!Wanauliza je pesa zote zinaenda wapi??
 
Kuna mbunge mmoja jana karopoka 75% ya TZ wana maji safi na salama. Kweli masikini hutumia kila liwezekanalo kuishi kama tajiri. Unajua kwa nini? Alikua vt maalum CCM....
 
Lakini itapita. Huo ni upepo tu. Kelele za mlango hazimuzuii mwenye nymba kulala. Tutaipitisha kwa namna yoyote. Liwalo na liwe.
 
duh we sijui ndo welu naona unafikiri kwa kutumia makalio maana mtu mwenye akili timamu awezi kuzungumza kitu cha ivyo a
 
ni upepo tu unapita,itapitishwa tu
hii ndio tanzania,viongozi wanajari itikadi za kichama kuliko mabosi wao wananchi
 
tatizo wabunge wa ccm ndio wanabebana we mtu kwenu huna maji ndugu zako hawana maji na hata kama maji yapo si masafi wananchi wanakufa na typhoid alafu unakaa hapo bungeni unaipitisha bajeti ya wizara kisa? ni ccm, amkeni hii ccm mnayoitetea sasa hivi iko siku itawapeni sumu au kuwatumia majambazi.
 
Nashawishika kusema kuna uwezekano kutopita hii bajeti!!Labda kwa nguvu za giza...maana aslimia kubwa wamekataa!!
 
Kutokana na kawaida ya mazoea ya baadhi ya mawaziri kuwa na mazoea ya kuleta bajeti ye nye samari bila takwiku hakiki sasa limemtokea puani Waziri wa Maji Mhe,Prof Magembe!!Wabunge wametupilia mbali itikadi zao sasa wanamsurubu waziri wa maji!!!wamerudi upande wa wananchi na kuwatetea...Kuna nchi 48!Mashirika yasiyo ya kiserikali!!(NGO's)120...nazaidi zinasaidia miradi ya maji..lakini nchi haina maji!!Wanauliza je pesa zote zinaenda wapi??
Mbuge wa Gairo Ahmed Shabib amemweleza Maghembe live kuwa wao wanashangaa kwa nini Rais amemrudisha tena kwenye post hiyo ya uwaziri wakati uwezo wake ni mdogo na akawalazimisha wabunge wote waikatae bajeti ya maji.
 
Alimpasua kweli live "Eti katika kuvunja baraza la Mwaziri tulijua fika haurudi lakini kumbe Rais akakuona unafaa"Bonge la tusi!Kweli maghembe uwezo wake ni mdogo japo ni msomi!!
 
Alimpasua kweli live "Eti katika kuvunja baraza la Mwaziri tulijua fika haurudi lakini kumbe Rais akakuona unafaa"Bonge la tusi!Kweli maghembe uwezo wake ni mdogo japo ni msomi!!

Hiy ndo CCM. Ukivuruga huku, unahamshiwa pengine ukavuruge zaidi. Maghembe uprofesa wake kama wa kapuya na mwandosya.

Hata Maji Marefu akipewa wizara anaweza ku perform vizuri kuliko hawa wazee.
 
Hiy ndo CCM. Ukivuruga huku, unahamshiwa pengine ukavuruge zaidi. Maghembe uprofesa wake kama wa kapuya na mwandosya.

Hata Maji Marefu akipewa wizara anaweza ku perform vizuri kuliko hawa wazee.
Nakubaliana na wewe wamechoka hawana tena tija!!!hata wakiwa wahadhiri..wanafunzi watasapu kila mara!!
 
Hiyo ni zuga tu ya magamba mwisho wa siku hiyo bajeti wataipitisha tu...!
Prof mzima unaleta bajeti isiyokidhi vigezo, nilifikiri atautumia uprofesa wake vizuri kuonyesha uwezo mkubwa.
Sasa prof Magembe si bora urudi tu ukafundishe?
 
Kelele za kumbikumbi hizo mwisho wa siku wanatiwa kwenye karai na kukaangwa na mtasikia bajeti imepita kiurahisi tu.

Hivi mnaelewa kama bajeti haikupita inabidi Raisi avunje Bunge ,je wabunge hao wenye viherehere wanaweza kukwamisha bajeti huku wakijua kuwa bajeti ikikwama ndio mwisho wa kazi yao ?
 
kiini macho cha Serikali ni Bajeti,Sheria,Utawala wa sheria,maadili ya Watanzania. AMANI yetu,Muungano wetu,na kuendelea.Maneno haya ni matamu na bajeti ni tamu kuisoma lakini ukweli unaoumiza hayo yote hayatekelezeki
 
Hakuna kitu hapo.... wabunge wataitwa kwenye Caucus ya CCM kuchimbwa mkwara wakitoka huko wote NDIYOOOOOO!
 
Back
Top Bottom