Prof. Lipumba niliyekutana nae akiwa na chupa ya maji mkononi!

Kwa mfano nikikupa ujumbe kwamba sitakuja kukutembelea kisha nikakupa ujumbe mwingine kwamba nimebatilisha uamuzi nitakuja kukutembelea,hapo utakuwa umeelewa nini?mbona ni rahisi sana kuelewa uamuzi wa prof
Process za ku-nulify ujumbe wa kwanza kati ya mtu binafsi, taasisi na chama ni tofauti mkuu... hicho ulichokieleza kiko sahihi kwa mtu binafsi tu..
 
Nyie ndo mnashindwa kusimamia ukweli mwanzo kipindi kabla ya uchaguzi mlisikika mkisema kabisaa kuwa hamtampokea mgombea wa urais kutoka ccm akasimama lakini mambo yalipobadilika baada ya DJ mbowe kupewa mabilioni akatelekeza hadi chama akamwachia salim mwalimu na baregu yeye akawa anahudhuria vikao vya kupiga dili na seif wake!! Leo nani atawaamini ata mkisema lipumba anatumiwa ??? Je mbowe atumiki kuhujumu chama
Asante kwa uchambuzi wako mzuri sana.
 
Maggid, Gideon Cheyo hajawahi kuwa mpinzani. Alikuwa Waziri wa Ardhi miaka ya tisini. Anatokea mkoa wa Mbeya. Uliyemzungumzia ni John Momose Cheyo, huyu ndo Bwana Mapesa. Na tunao wawili tu, mwingine ni Ndesa Pesa, Philemon Ndesamburo wa Chadema.
 
Professa Lipumba aliharibu yeye Mwenyewe, alijiondoa CUF kimtindo, hakuna aliyemfukuza bali alijifukuza mwenyewe, hana tofauti na Dr.Slaa. Watanzania walikuwa wanampenda Lipumba na Slaa kwa sababu ya Hoja zao na misimamo yao ya kuipinga CCM na Sera zake. Bahati mbaya sana wote kwa pamoja(Slaa na Lipumba) waligeuka na kuwa wasaliti. Usaliti ni dhambi mbaya sana.

Professa Lipumba ataheshimika sana kama atafanya mambo haya kwa sasa..
1/Awaache CUF waendelee na chama chao.
2/Abaki kuwa mtu huru asiyekuwa na chama.
3/Abakie kwenye kazi yake ya Ushauri wa kiuchumi.

Nina uhakika Professa akifanya hayo, Nature yenyewe itamuinua na kumpeleka pale juu anapopataka. Ni kanuni kuu ya Busara inayosema kuwa 'Muungwana Akiteleza katika jambo, basi anapaswa kujutia na kutulia kwanza!'
 
Lipumba angebakia mshauri wakisiasa hapa Nchini na uchumi kuliko kujidhararisha!!!kwa anayofanya sasa HV ni nonsense heri kuishi na fikra pevu
 
Wameshamuathiri kwa Upropesa sasa wanamtumia kwa faida yao ili alete mtafaruku ndani ya CUF na hivyo kuiathiri UKAWA pia.
mkuu nimependa hilo jina unalowapa: ProPesa!:):)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Lipumba angekuwa mchumi chama chakafu kingekua ni tajiri sana, wanachama nitaji mkubwa aliwatumiaje kujenga chama? Pili, Rudhuku na dayaspora alitumiaje nafasi hiyo pia? Wafadhiri aliwatumiaje kujenga chama. Watanzania tuache kumpamba mtu alieshindwa hata kwao tabora amepeleka mchango gani kama mw/kiti mda wote?
 
Acha dharau Niffah kila binadamu ana thaman yake mbele ya Mungu na wanadam awe maskini au jobless athaminiwe tu,tuache dharau
 
Etii leo wapinzani wanajiita UKAWA genge la madili wanamwini fisadi lowasa na kingunge mtu ambaye kazi yake sasahivi ni kula na kulala wanafanya kila aina ya hujuma profesa lipumba aondoke CUF muasisi wa katiba ya wananchi !!! Teh teh teh hawa watu tuwaogope kama ukoma
Aliita camera NA vipaza sauti mwenyewe
Kujiuzulu
 
Hakuna mtu mwenye nguvu kushinda taasisi aliyomo,Chadema walimuondoa zitto, akaondoka Dr slaa lakini chama kimeimarika badala ya kudhoofika.CCM aliondoka Mrema,Lowasa,Sumaye nk nk na bado walishinda uchaguzi (kwa mujibu wa matokeo ya tume).Kwa hiyo ni kichekesho kudhani Lipumba akifukuzwa/akijiondoa ni tatizo kubwa kwa Cuf kama taasisi.
 
Ile haiba aliyokuwa nayo kisiasa imepungua.
Kwanini Prof. Lipumba Ni Mjadala Mkubwa?

Ndugu zangu,

Mada niliyoianzisha jana imezua mjadala mkubwa. Nimefutilia kila kilichoandikwa na wajumbe. Ningependa kufanya hapa majumuisho.

Kuna moja kubwa nililolibaini, kuwa wengi waliochangia hawakujihangaisha sana kutaka kuyajua ya jana kwa maana ya historia.

Wengi wamechangia bila kujibu hoja za msingi za Profesa Lipumba, ambazo kimsingi ni nzito na hazina majibu mepesi.

Binafsi ningelipenda sana kuisoma michango ya Wanachama wa CUF, maana, hili la Profesa ni mgogoro wa ndani ya CUF na unahusu Katiba ya chama hicho pia. Nyongeza hapa ni ukweli kuwa kuna kinachoitwa ' Siasa za CUF'. Hizi zina tofauti sana na za CCM, Chadema na wengineo. Kuzijua hizi ni lazima urudi nyuma hadi kwenye matukio ya walau 1984 ili upate mwanga.

Naam, kwa kuyafuatilia yanayoendelea ndani ya CUf, na kama viongozi wakuu wa CUf wasipotanguliza busara, nauona mpasuko mkubwa wa CUf- Bara na CUF- Visiwani.

Haiwezekani leo ikawa rahisi kumweka kando Profesa Lipumba kama ilivyokuwa kwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama hicho James Mapalala. Na hata ilivyokuwa rahisi kwa Musobi Mageni kukaa pembeni na kumpisha Profesa Lipumba kwenye uenyekiti.

Profesa Lipumba ana uungwaji mkono na wafuasi wa kutosha kuimega CUF wakitokea Bara. Ndani yake kuna wenye majina na wafuasi nyuma yao. Ni watu wa aina ya Magdalena Sakaya, Nachuma na Kambaya. Miongoni mwao ni wabunge.

Kumekuwa na manung'uniko ya CUF Bara kuwa CUF kama chama kinaendeshwa kwa msukumo na mashinikizo ya upande wa pili kwa maana ya visiwani. Maalim Seif pia anatupiwa lawama za moja kwa moja na wenye kumuunga mkono Profesa na hususan walio bara.
Hakuna namna nyingine iliyo bora ya kuinusuru CUF isimeguke bila kufanyika jitihada za kufanyika juhudi za upatanisho hata kwenye kuutafuta mwisho wa mafahari wawili kukaa zizi moja.

Profesa Lipumba, katika hali ya sasa, na kwa hoja alizoweka mezani, anaonekana dhahiri yuko katika matayarisho ya juu kabisa ya mapambano ya kisiasa.

Ni jukumu pia la Msajili wa vyama vya siasa ambaye pia ni mlezi wa vyama vya siasa, kuandaa mazingira ya upatinishi kuepuka mpasuko ndani ya CUF ambao unaweza kupelekea uhasama usio na tija kwa taifa miongoni mwa makundi yanayoibuka katika mgogoro huu wa ndani ya CUF.

Tumeshaziona ishara,

Maggid Mjengwa.
 
Ndugu zangu,

Nimepata kuandika hili mwaka jana, kuwa kwangu mimi, Profesa Ibrahim Rehani Lipumba ni mmoja wa wanasiasa walioacha pengo katika mbio za Urais kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.

Ni kwa kuamini, kuwa Profesa Lipumba ni mmoja wa wanasiasa makini na wenye misimamo, tunapozungumzia siasa za upinzani hapa nchini.

Profesa Lipumba ameng'olewa na chama chake cha CUF. Hata hivyo, Afrika miti mingine huachwa izeeke na kuanguka yenyewe. Ni kama mibuyu, kuing'oa kwake lazima iache kishindo na ardhi kutikisika.

Kwa mimi niliyebahatika kufuatilia kwa karibu siasa za nchi hii, silioni hili la Profesa kung'olewa CUF kuwa ni jambo jepesi. Nahofia kuwa wenye kumbeza Profesa Lipumba ikiwamo humu mitandaoni hawajisumbui kuyasoma ya jana yenye kutusaidia kuyatafsiri ya leo na kutusaidia kuyabashiri yatakayotokea kesho.

View attachment 397185

Kwa kuyaangalia ya jana, na kwa kumwangalia Profesa, tunaona, kuwa kwenye siasa za nchi hii, Profesa Lipumba si kama mti wa mpapai wa kuweza kukatwa kwa kiwembe. Profesa ni mbuyu mkongwe uliota mizizi ikasambaa. Kuung'oa kwakwe kunahitaji si shoka, bali mashoka. Na lazima mengine yakatike.

Naam, kung'olewa kwa Profesa lazima kuache majeraha makubwa na yatakayochukua muda mrefu kupona, si tu kwa CUF, bali kwa siasa za upinzani hapa nchini.

Maana, simwoni Profesa atakayehamia CCM, bali atakayebaki mpinzani wa CCM nje ya wapinzani wa CCM. Hilo la mwisho si jambo jema kabisa kwa siasa za upinzani na ustawi wa demokrasia hapa nchini.

Ni nani basi Profesa Ibrahim Lipumba?

Ni ukweli, kuwa Profesa Lipumba kwa wakati tulio nao, ni mwanasiasa pekee kwenye upinzani na pengine kwa nchi nzima mbobezi kwenye masuala ya kiuchumi na anayetambulika kimataifa.

Kwenye siasa zetu, uchumi ni moja ya ajenda zinazopaswa kuwa sehemu ya mijadala muhimu katika kupima uwezo wa wagombea. Ni katika kutafuta majibu ya ni kwa namna gani wagombea wamejipanga kimikakati katika kutuambia sio tu watafanya nini , bali ni kwa namna gani, kwenye kututoa hapa tulipo na kwenda kwenye hali bora zaidi kiuchumi, kama taifa.

Nakumbuka, kwenye Uchaguzi wa mwaka 2005, Vyombo vya Habari vilikazana kuandika habari za JK na Freeman Mbowe. Ikawa ni habari za CCM na CHADEMA kila kukicha. Vikasahau, kuwa kulikuwa na mgombea wa urais aliye kwenye mbio na mwenye umuhimu pia, maana, kuna wengi walimkubali. Yawezekana jambo hilo lilifanywa na media yetu kwa bahati mbaya au kwa makusudi. Kumsahau Profesa Ibrahim Haruna Lipumba wa Chama Cha Wananchi ( CUF).

Kwangu mimi, mwaka ule wa 2005, katika wote walioshiriki mbio za Urais, Prof. Lipumba ndiye alikuwa mwenye uzoefu zaidi wa njia ya urais ambayo wenzake na yeye walikuwa wanaikimbilia.

Ikumbukwe, Profesa Lipumba ana uzoefu wa kinyang'anyiro cha urais tangu mwaka 1995. Ilikuwa ni kwenye Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi.
Ikumbukwe pia , Profesa Lipumba anaingia kwenye historia ya kushiriki mdahalo wa kwanza wa wagombea urais akiwa mpinzani. Wenzake wawili; Augustino Mrema na Gideon Cheyo ( Bwana Mapesa) waliingia kwenye mdahalo ule wakipambana na Ben Mkapa, lakini, hatuwezi leo, kwa yakini, kusema hapa kuwa walibaki na wamebaki kwenye upinzani na chama tawala.

Kwenye mdahalo ule wa wagombea urais wa mwaka wa 1995, Profesa Lipumba aliiibuka wa pili kwenye mdahalo kwa kupewa alama za juu kutokana na maoni ya wananchi yaliyokusanwa na mashirika ya habari ya kigeni mara baada ya kumalizika kwa mdahalo.

Ni mdahalo huo wa 1995 uliomwacha Ben Mkapa akiongoza na Mrema akiambulia nafasi ya tatu, huku John Cheyo akikamata mkia.

Bila kuchezesha kalamu, kiukweli Profesa Lipumba alikuwa na anabaki kuwa ni mpiganaji mahiri kwenye harakati za kisiasa. Mwaka 1995 aliingia kwenye mbio za Urais kama ‘ Profesa’. Hilo lilikuwa kosa, akalirudia tena mwaka 2000. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Profesa Ibrahim Lipumba alionekana zaidi kama ‘ Ibrahim Lipumba’. Profesa aliamua kushuka chini, kuwa na watu na kuongea lugha yao.

Nakumbuka kukutana na Profesa Lipumba ana kwa ana kwa mara ya kwanza mwezi Oktoba 2005, wiki kadhaa kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu. Ni pale Isimila Hotel, Iringa. Ni Hotel ya kawaida kabisa. Ndugu yangu Saed Kubenea alikuwa kwenye msafara wa kampeni wa Profesa Lipumba, na ni Saed Kubenea aliyefanya maandalizi ya mimi kukutana na Profesa Lipumba.

Ilikuwa siku ya Alhamisi, nilifika pale Isimila Hotel kunako saa tatu asubuhi. Aliponiona, Profesa Lipumba alinijia akiwa mwingi wa tabasamu;
“ Kumbe, ndiye wewe Maggid!” Alitamka huku akionyesha furaha. Mkono wa kushoto alikamata jarida la Rai na chupa ya ‘Maji Afrika’. Saed Kubenea alisimama kando, mbali kabisa na sisi ili kupisha mazungumzo ya Profesa na mimi.

Kwenye mazungumzo yetu nilimwona Profesa Lipumba kuwa ni mtu wa kawaida sana. Tukiwa tumesimama, kuna wakati kwenye mazungumzo yetu, Lipumba alikuwa akipukuta vumbi kwenye suruali yake kwa kutumia gazeti la Rai.

Kwa kawaida, mwanasiasa huyu Lipumba anaongea kwa mpangilio na kwa kutulia. Kushiriki kwake katika uchaguzi wa 1995, 2000 na 2005 kumempa uzoefu zaidi katika vinyang’anyiro vya urais. Lipumba ana uwezo na kipaji cha kufafanua mambo magumu na yakaeleweka kwa mtu wa kawaida.

Mwaka ule wa 2005, kuna wakati nilimsikia Lipumba akitoa mfano wa ajira elfu moja zenye uhakika kwa vijana zinavyoweza kuathiri maisha ya mama mwuza vitumbua. Profesa Lipumba alitamka;

“ Ndugu zangu, bila ya vijana hawa kuwa na ajira na kipato , mama huyu atashinda na vitumbua vyake vikimtazama !.”

Hakika, Lipumba ana uwezo pia wa kutengeneza sentesi fupi na zenye kishindo; Mwaka ule 2005 nilimsikia akitamka;

”Wananchi nikopesheni kura zenu, nitawalipa maendeleo!” Hizi ni baadhi tu ya nguvu za Profesa Ibrahim Lipumba katika rethorik, sanaa ya kuzungumza.

Tuliofuatilia kampeni za Profesa za urais, tumeona kuwa huwa na sura za mikakati ya kijeshi. Mwaka 2005 tulimwona Lipumba akianza kampeni kwa kuanzia na kule ambapo aliamini kuna matumaini ya kupata ushindi, matumaini ya kuvuna kura.

Itakumbukwa, 2005 Lipumba alianza kampeni zake kwenye ‘ngome’ ya CUF kwa wakati huo, na hata hii leo. Ni mikoa ya Kusini; Lindi na Mtwara. Huko Profesa ‘alipiga kambi’ ya zaidi ya juma moja akifanya kampeni.

Baada ya kule kusini, tulimwona Profesa akichagua maeneo ya kwenda. Na kila alikokwenda kulikuwa ni kule ambako, CUF ilionekana kuungwa mkono.

Mwaka 2005, staili ya kampeni ya Profesa Lipumba ilibadilika pia. Profesa Lipumba alionekana kuwavutia zaidi wasikilizaji na watazamaji kwenye hotuba zake.

Lipumba baada ya kuongea majukwaani alishuka chini na kuongea na wapiga kura akiwa karibu nao sana. Kila mahali alipofika, aliunganisha masuala makubwa na yale ya mahali hapo. Aliachana na staili ya kutumia muda mwingi kukishutumu Chama Cha Mapinduzi bila kuwafafanulia wapiga kura yeye akiingia madarakani atafanya nini na kwa namna gani. Hivyo, kwa mwaka ule wa 2005, Profesa Lipumba alisisitiza zaidi nini angekifanya, yeye na chama chake, na kwa namna gani. Kile ambacho CCM wameshindwa kukifanya.

Kabla ya mikutano ya hadhara, Profesa alifanya jitihada za kuikaribia jamii ya mahali hapo. Mathalan, Profesa Lipumba alikwenda sokoni . Huko aliongea na wananchi, aliuliza bei za vyakula. Kule Musoma tukamwona Profesa akipima nguo kwa fundi cherehani, alitaka fundi huyo amshonee suti yake. Pale Bunda Lipumba akamtembelea nyumbani kwake Mzee Raphael, mwanachama wa CUF wa miaka mingi. Kule Geita tulimwona Lipumba akizungumza na wachimbaji madini wadogowadogo akiwa kwenye machimbo yao.

Ndio, tulimwona Lipumba akibeba mawe kuweka chini ya tairi na hata kusukuma gari lake kule Kondoa . Ni wakati msafara wake ulipokwama njiani. Tulimwona Lipumba akishiriki shughuli ya mazishi kule Mafia na Kagera. Kwamba kila alipokwenda kukampeni, Profesa Lipumba alitafuta habari kuhusiana na mahali hapo, ikiwamo pia habari mbaya kama misiba. Kwenye misiba kuna wapiga kura.

Hii nayo ni staili ya kampeni aliyoionyesha Lipumba katika uchaguzi mwaka 2005. Kushuka chini kwa watu. Mgombea usijikite tu kwenye kukusanya watu, unapaswa pia kuonekana iliko mikusanyiko ya watu, kuongea nao katika hali za kawaida, na si za maonyesho kwa vyombo vya habari.

Na bila shaka, nguvu za Profesa Lipumba za mwaka 2005 na mavuno makubwa ya kisiasa aliyovuna yeye na chama chake, hayakutokana na Profesa peke yake.

Nilipokutana naye mwaka ule wa 2005 pale Isimila, Profesa hakusita kuniambia, kuwa alijivunia nguvu za chama chake, CUF. Kwamba kimejitahidi sana kuweka mizizi chini waliko watu.

CUF imetoka wapi?

Chama cha CUF kiliundwa Mei 28, 1992. Ni chimbuko la kuunganishwa kwa Chama cha kutetea haki za Wananchi (Civic Movement) kwa upande wa bara na chama cha KAMAHURU cha Zanzibar.

CUF imetokana na vuguvugu la mageuzi nchini. Ingawa NCCR-mageuzi kilikuwa ni chama cha kwanza cha upinzani, CUF kilikuwa chama cha pili kusajiliwa katika mfumo wa vyama vingi baada ya CCM.

Hii ilitokana na sura yake ya muungano kuonekana dhahiri. Hii ni moja ya nguvu kubwa za CUF. Hakuna anayejisumbua kuweka hadharani, ukweli kuwa, kwa sasa, CUF ni chama pekee cha upinzani, chenye uhakika wa kuwa na wawakilishi bungeni kutoka Unguja, Pemba na Bara. Na kwa upande wa Bara, Profesa Lipumba, kutokana na kuaminika kwake, amekuwa mhimili muhimu wa kuhakikishia CUF viti upande wa Bara.

Chadema, na NCCR, pamoja na umaarufu wao Bara, vyama hivi viwili, havijapata kuwa na hakika ya kuvuna viti vya Ubunge Unguja na Pemba. Na siku ikitokea, hiyo itakuwa ni habari kubwa.

Naam, miaka kumi imepita tangu nikutane na kuongea na Profesa Lipumba. Mengi yametokea, ikiwamo ya yeye mwenyewe Profesa kuachia ngazi ndani ya CUF kwa kujiuzuru uongozi na kubaki mwanachama, kisha baada ya kuombwa, kama anavyosema, ameamua kurudi kugombea nafasi yake na kuibua sintofahamu ya ndani ya CUF. Hii ni moja ya changamoto ya demokrasia ya ndani ya vyama- Intra party democracy.

Profesa Lipumba ameibua mjadala unaoendelea. Nimeamua kuushiriki. Nitapenda siku moja nikutane tena ana kwa ana na Profesa, nizungumze nae, ni katika kuendelea kujifunza, hata kwangu.

Maggid Mjengwa.
Iringa.
Msaidie muanazishe chama,. Wewe uko kazini, yeye kijiweni... Tengenezeni pair bora muwasaidie Watz. Lakini kumbuka hapo Iringa ulipo palikuwaje na sasa pakoje. Sayansi ya siasa ina mambo. Uwakala nao unahitaji moyo na roho ya paka. Lakini ndivyo dunia ilivyo
 
Back
Top Bottom