Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,038
- 30,376
GAZETI LA UHURU LILIPOSEMA KUWA PROF. MALIMA ATAJITOA CCM MSIKITINI TABORA 1995
Ijumaa moja tarehe 15 Julai mwaka wa 1995 gazeti la Uhuru, lilibeba kichwa cha habari katika wino mweusi uliokoza likisema kuwa siku hiyo Prof. Kighoma Ali Malima atatangaza kujitoa kwake CCM kutoka Msikiti Mkuu wa Ijumaa Tabora baada a Sala ya Ijumaa.
Habari hii ilileta mzizimo wa aina yake nchi nzima Malima akawa kapakwa rangi kuwa ni mtu hatari anetaka kusababisha mgogoro mkubwa wa kidini nchini.
Mjini Tabora Ijumaa ile mji ulikuwa na hali isiyokuwa ya kawaida kutokana na taarifa ya gazeti la Uhuru.
Habari zilikuwa zinaenea kama moto wa makumbi kuwa Prof. Malima yuko Tabora na atawahutubia Waislam katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa.
Hata jua halijapanda sawasawa msikiti ukawa umejaa hadi nje barabara zimefungwa Waislam wamejazana kuuzunguka msikiti na misala yao na mikeka waswali Ijumaa kwenye jua kali kisha wamsubiri Malima kupanda katika membar kuwahutubia kuwaeleza kuwa anajitoa CCM.
Watu wa usalama walikuwa wamejichanganya na Waislam ndani na nje ya msikiti kwani jana yake Regional Police Commander (RPC) alifika ofisi za BAKWATA na kufanya kikao na uongozi akawafahamisha kuwa taarifa zao zinaonyesha kuwa Prof. Malima atazungumza na Waislam ndani ya Msikiti wa Ijumaa kwa hiyo BAKWATA wasimruhusu kufanya hilo kwani huko ni kuchanganya dini na siasa.
Muda mfupi kabla ya khutba Sheikh Mavumbi kutoka BAKWATA akaletwa msikitini pale na gari la polisi akisindikizwa na RPC.
Sheikh Mavumbi moja kwa moja akaenda kibla akachukua kipaza sauti akawaonya Waislam hatari ya kuchanganganya dini na siasa.
Msikiti ulikuwa umetulia kimya kabisa Waislam wanamsikiliza sheikh wa Mavumbi kutoka BAKWATA akiwanasihi.
Sheikh Mavumbi akasema anazo taarifa kuwa Prof. Malima atazungumza msikitini hapo na yeye amekuja kuzuia jambo hilo.
Allahu Akbar.
Vumbi zito likatimka.
Alipotaja tu jina la Prof. Malima msikiti ulilipuka Waislam wakimuuliza hizo taarifa yeye kapewa na nani?
Kelele zikajaa msikitini.
Waislam kila mmoja anazungumza anamuuliza Sheikh Mavumbi nani aliyempa taarifa hizo?
Sheikh Mavumbi akawa kachanganyikiwa hakutegemea kabisa kuwa Waislam watamghadhibikia kiasi kile.
Imam Mkuu wa msikiti ule Sheikh Issa Mzee, miaka ile kijana mdogo wa kiasi cha miaka 30 katikati akasimama kuwatuliza Waislam lakini hakuna aliyemsikiliza.
Vurugu ikaendelea msikitini.
Waislam waliokuwa nje ya msikiti kusikia kelele zile
wakanyanyuka wakawa wanaminyana milangoni wakitaka kuingia ndani msikitini.
Dalili zote zikawa wazi kuwa sasa heshima na hadhi ya msikiti ilikuwa taratibu inatoweka msikiti unageuka kuwa uwanja wa vurugu, fujo na mapambano baina ya Waislam na sheikh mmoja kutoka BAKWATA.
Hapo ndipo Mzee Bilal Rehani Waikela aliposimama akachukua kipaza sauti na kwa sauti yake ya upole ikasikia kutoka ''speaker'' za msikiti ndani na nje akisema, ‘’Waislam msalieni Mtume,’’ akiyarudia maneno haya.
Hakuna mtu Tabora amae hakuwa anaijua sauti ile achilia mbali kumjua mwenye sauti ile.
Kwa pamoja palisikika kibwagizo cha Waislam wakimwitika wakimsalia Mtume ndani na nje ya msikiti.
Utulivu ukarejea msikitini Waislam wakakaa chini wametulia.
Mzee Waikela kwa utulivu akamuuliza Sheikh Mavumbi wapi kapata taarifa kuwa Prof. Malima atakuja kuzungumza hapo msikitini.
Sheikh Mavumbi hakuwa na jibu.
Mzee Waikela akamwambia Sheikh Mavumbi aangalie kama anamuona Prof. Malima mle ndani msikitini.
Mzee Waikela akawauliza Waislam, ‘’Ndugu zangu kuna yeyote kamuona Prof. Malima hapa msikitini?
Prof. Malima si kuwa hakuwepo mle msikitini bali hata hapo Tabora mjini pia hakuwapo.
Mhariri wa Uhuru siku ya Jumamosi wala hakuwataka radhi wasomaji wake kuwa katika toleo lililopita alikuwa ameandika habari ambazo hazikuwa za kweli kuwa Prof. Malima atajitoa CCM ndani ya Msikiti wa Ijumaa Tabora.
Wala Uhuru halikufungiwa likaendelea na vita vyake dhidi ya Prof. Malima hadi umauti ulipomchukua mwezi kama huu wa August 1995.
Historia huwa na kawaida ya kujirudia.
Mtangazaji wa Radio Tehran, Iran Abdufatah Mussa akinifanyia mahojiano kuhusu Prof. Malima mwaka wa 2001.