PROF JAY KUANZISHA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU

msumba news

New Member
Nov 2, 2016
1
0
Mbunge wa Mikumi kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Joseph Haule.

Ameanzisha Ligi ya mpira wa miguu itakayohusisha Kata 15 zote za Jimbo la Mikumi.

Akizungumza na mwandishi wetu Mbunge wa Mikumi amedai

"Mimi kama Mbunge na Wananchi wangu wa Mikumi tunategemea Mashindano haya yatakuwa makubwa na ambayo hayajawahi kufanyika hapa jimboni ambapo mpaka sasa nimeshakamilisha utaratibu wa timu zote 32 ambazo zitachuana kwenye haya mashindano yanayoitwa PROFESSOR JAY CUP 2016"

Washindi watapewa zawadi kama ifuatavyo:-

Mshindi wa kwanza atapewa pesa taslimu Tsh/=2,000,000 pamoja na Kombe Kubwa

Mshindi wa pili atapewa pesa taslimu Tsh/=1,000,000 pamoja na Kombe

Mshindi wa tatu atapewa pesa taslimu Tsh/=750,000

Mshindi wa nne naye pia atapokea pesa Tsh/=500,000

Pia kuna zawadi lukukii kama timu yenye nidhamu,mfungaji bora mchezaji bora

Watakajituma vizuri kwenye ligi hii na chipukizi 20 watapelekwa wakafaye majaribio kwenye timu kubwa za vijana hapa nchini.

picha habari na @www.msumbanews.com

 
Hongera sana.
Good movement for young footballers.
Amewatendea haki Wananchi wake.
 
Back
Top Bottom