Prof Assad ameonesha mfano kwa wasomi wetu

Wasomi waliopo CCM (Genge la kamongo) kama Kabudi, Mwakyembe, Kitila na wengineo hawana tofauti kabisa na Msukuma, Kibajaji, Polepole, Jah People na Milinga. Ndio maana Sugu amewaita Poyoyo.
 
Kama kuna hizo hoja au taarifa zenye kuonesha udhaifu wa Bunge kwa mujibu wa Assad ziweke hapa ...mimi sina ujasiri wa mbwa hata siku moja
Ukisikiliza hiyo clip ya mahojiano kule UN, kila kitu kipo wazi. lakini nikuulize swali. enzi za Jk, tulizoea kuona bunge likiisimamia serikali, na kusababisha mawaziri kujuzulu na wengine kuwajibishwa. hilo hivi sasa halipo. Ni kwa nini?

Maana sasa hivi wabunge wanapoikosoa serikali, mfano katika suala la korosho, wanatishiwa maisha yao. NITAANZA NA SHANGAZI ZAO. sasa hivi wabunge, tena wa CCM, wanajiuzulu vyeo vyao kwenye kamati mbalimbali kutokana na kutokubaliana na mashinikizo ya serikali ya JPM ambaye amepenyeza watu wake bungeni: Naibu Spika na Katibu wa Bunge. Ndugai naye sasa hivi anaimba wimbo wa Magufuli. Kwa hiyo enzi zile walijiuzulu wale wanaosimamiwa na bunge, sasa hivi serikali ndiyo "inawajibisha wabunge". Lakini hiyo siyo kwa mujibu wa katiba yetu. katiba yetu inasema BUNGE LITAISIMAMIA SERIKALI. upo hapo?
 
Ujasiri wa Mbwa koko
Ukiona mtu anaokotoa mawe, ujue ngumi zimemshinda. ukiona mtu anatukana ovyo, ujue hoja zimemshinda. hivi kama CAG angeongea hiyo lugha ya mbwa dhidi ya Ndugai au bunge, si angeitwa kwenye kamati mara ya pili, kama vile ambavyo Ndugai alidokeza jana kwamba akitumia neno hilo tutamwita tena kwenye kamati? huko ndio kushindwa. POLENI SANA!
Ila la kufurahisha ni kwamba wananchi kwa wingi wao, wako nyuma ya Prof. Assad. na hilo lilimsumbua Ndugai jana. haelewi kwa nini vyombo vya habari vinamshabikia sana Assad. Ndiyo kupendwa huko. ndiyo kuaminiwa huko.
 
Prof Musa Assad Juma , ametoa fundisho la kutosha kwa tasnia inayo jiita ya wasomi hapa nchini.

Mbali ya kuonyesha jicho na fikra za msomi zinavyo stahili kuwa, lakini pia ameonyesha jinsi wacha Mungu wanavyo stahili kuusimamia ukweli.

Kuna kipindi fulani waliitwa hao wanajiita wasomi kwenda kuzungumzia ni jinsi gani serikali yetu inavyo weza kujiendesha na kutuletea mafanikio, mbona ilikuwa ni aibu , badala ya kushauri wao wabaki kutoa sifa za uongo uongo tu, kwa ukweli walitia aibu ya kupindukia.

Ni wazi kuwa awamu hii imekuja na kamtindo fulani ka kukataa kuambiwa ukweli, lkn Assad jipe moyo na watanzania wameona utendaji wako.

Ni wazi kuwa yajayo yanaweza yasifarahishe sana , lakini baki kuwa shujaa kwa kuto mpigia magoti shetani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mama Tibaijuka aliogea kitu nikamuelewa,nadhani sasa anaanza kulinda heshima ya Uprofesa wake,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujui usemalo! We unajua kwenye kamati aliulizwa nini na alijibu nini? Unajua alitoa maelezo gani kuhusu maana ya neno "dhaifu" kama linavyotumika kwenye tasnia ya ukaguzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo maana CAG aliomba majibizano aliyofanya na kamati ya bunge yawekwe wazi ili umma ujue alichoulizwa na alichojibu. Jambo ambalo si rahisi kutetekelezwa
 
kudharau sio kosa kama unavyodhaji.Ndugai na Bunge lazima wadharauliwe.kwa matukio wanayofanya unaachaje kuwadharau.Msomi ukiwanyenyekea wapuuzi kama Ndugai basi na wewe unaonekana usomi wako si kitu.
Msomi lazima uwe na kitu cha tofauti kulinganisha na wajinga kama Bashite,kibajaji,msukuma, na wengineo.Msomi lazima uwe strong kama Assad.
Inasikitisha wasomi kama Tulia wanaburuzwa na mazwazwa wengi wakati wao ndo ilipaswa wawe kioo
Kuwa msomi haimaanishi wewe kuona wengine kazi zao ni dhaifu.Kilikuwa ni kitu kidogo tu cha kuomba radhi na kufafanua hilo neno lake la udhaifu wanavyolitumia kwenye kazi yao kama neno la kawaida.Vinginevyo alionyesha kuwa yeye ni anadharau na hata kuweka sifa mbaya kwa wasomi ni watu wenye dharau wakiwa makazini.Nchi haindeshwi kwa misifa na majivuno ya usomi bali ni kwa weledi na ustahimilivu na kufuata sheria basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inapendeza sana...

Siyo kila wakati changamoto ziwe kwa wananchi pekee, acha nao serikali ipambane na changamoto...

Cc: mahondaw
 
Kuwa msomi haimaanishi wewe kuona wengine kazi zao ni dhaifu.Kilikuwa ni kitu kidogo tu cha kuomba radhi na kufafanua hilo neno lake la udhaifu wanavyolitumia kwenye kazi yao kama neno la kawaida.Vinginevyo alionyesha kuwa yeye ni anadharau na hata kuweka sifa mbaya kwa wasomi ni watu wenye dharau wakiwa makazini.Nchi haindeshwi kwa misifa na majivuno ya usomi bali ni kwa weledi na ustahimilivu na kufuata sheria basi.
Kwani ukiwa dhaifu na mtu akakwambia wewe ni dhaifu ni kosa ?
 
Acha kupotisha ,Prof alishafa
Kuwa msomi haimaanishi wewe kuona wengine kazi zao ni dhaifu.Kilikuwa ni kitu kidogo tu cha kuomba radhi na kufafanua hilo neno lake la udhaifu wanavyolitumia kwenye kazi yao kama neno la kawaida.Vinginevyo alionyesha kuwa yeye ni anadharau na hata kuweka sifa mbaya kwa wasomi ni watu wenye dharau wakiwa makazini.Nchi haindeshwi kwa misifa na majivuno ya usomi bali ni kwa weledi na ustahimilivu na kufuata sheria basi.
Acha kupotosha Prof alishatoa ufafanuzi wa alichokuwa anaimanisha ,usitake kulazimisha nyeupe kuwa nyeusi .
 
Kuna kipindi fulani waliitwa hao wanajiita wasomi kwenda kuzungumzia ni jinsi gani serikali yetu inavyo weza kujiendesha na kutuletea mafanikio, mbona ilikuwa ni aibu , badala ya kushauri wao wabaki kutoa sifa za uongo uongo tu, kwa ukweli walitia aibu ya kupindukia.
Tungekuwa na wasomi wenye kujua wanachosimamia kama prof Assad basi nchi ingekuwa mbali!
... Prof. Mussa Assad ni chapa halisi ya binadamu yeyote anayeitwa msomi wa angalau shahada ya uzamivu (PhD). Prof. Assad, ameuona na kuutamka ukweli kama ulivyo pasi na unafiki wowote; so amejipambanua kuwa tofauti na wachungaji, maaskofu, na mashekhe wetu ambao unafiki hauwaishi vinywani.
Binafsi nampongeza Profesa kwa msimamo wake na aendelee hivyo kwani angetaka angeweza kufanya yale ya kuhudumia tumbo lake. Baada ya hapo ni vizuri pia tujue Professa nafasi yake inalindwa kikatiba na sio rahisi kumfukuza kazi (ukiacha kutumia nguvu au vitisho). Sasa mkija kwa maprofessa wengine tujue kuna wazalendo wengi tu wanachapa kazi zao kama maprof. vyuoni. Shida inakuja wanapo pewa au wanapo tafuta kazi zenye siasa ndani yake, wengi husoma alama za nyakati na kuamua kuridhisha matumbo yao hadi kukana kile wanacho amini. Wapo pia ambao wao madaraka huyaweka mbele sana na wako tayari kufanya lolote bora tu wawe karibu na wahusika. Lakini pia wako wale ambao ni waoga na kwa sababu nafasi zao hazina kinga huamua kimya kimya kufanya yale wakubwa wanayotaka hata kama wao wenyewe hawayapendi (watoto lazima wale eti).
 
Nimekuja kugundua hii nchi haina uzalendo, kama raisi magufuli anahusika kwa namna moja au nyingine kwa ubadhirifu unaoelezewa katika ripoti hiyo basi mwenyezi Mungu na yeye ndo wanajua watakachofanyiana baadae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwa msomi haimaanishi wewe kuona wengine kazi zao ni dhaifu.Kilikuwa ni kitu kidogo tu cha kuomba radhi na kufafanua hilo neno lake la udhaifu wanavyolitumia kwenye kazi yao kama neno la kawaida.Vinginevyo alionyesha kuwa yeye ni anadharau na hata kuweka sifa mbaya kwa wasomi ni watu wenye dharau wakiwa makazini.Nchi haindeshwi kwa misifa na majivuno ya usomi bali ni kwa weledi na ustahimilivu na kufuata sheria basi.
Kuitwa dhaifu si dharau. Mm ni msomi.. na nikwambie tu.. hata chuo ukifel ww ni dhaifu. Yes
Usomi ni kutokumumunya maneno. Nyeusi ni nyeusi.. nyeupe ni nyeupe. Not otherwise.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakupa pole
umechelewa sana kugundua.

Ndani ya CCM hakuna mtu hasiye na damu ya kifisadi.
CCM, Chadema, na vyama vyote, hamna mzalendo hata mmoja, nchi pekee yenye uzalendo ni china tu, kule mtu wa serikali ukileta wizi na udanganyifu ni jela tu na kila mwisho wa mwaka wanatembezwa magerezani ili kujiwekea akilini kitakachotokea wakikamatwa wanaibaiba fedha za wananchi, huku hamna mtu mzalendo, japo kwa nje watu wanatimiza majukum yao kwa 70% still wizi bado upo, tena kwa mabilioni, no wonder hii nchi haipigi hatua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kigwangala. Mkuchika, Makmba
Mwisho wa siku munamtuhumu tu Spika lakini CAG aliamsha ye mwenyewe huu mgogoro..!
CAG hajaamsha ila ameweka ukweli. Kama unavyojua ukweli unauma. Na spika vile ana akili ndogo akakurupuka kuanza kuchimba biti..
Hili suala spika angeenda nalo taratib tusingefika huku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwa msomi haimaanishi wewe kuona wengine kazi zao ni dhaifu.Kilikuwa ni kitu kidogo tu cha kuomba radhi na kufafanua hilo neno lake la udhaifu wanavyolitumia kwenye kazi yao kama neno la kawaida.Vinginevyo alionyesha kuwa yeye ni anadharau na hata kuweka sifa mbaya kwa wasomi ni watu wenye dharau wakiwa makazini.Nchi haindeshwi kwa misifa na majivuno ya usomi bali ni kwa weledi na ustahimilivu na kufuata sheria basi.
Kwani amevunja sheria IPI?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom