Prince Bagenda kuwa Mhariri Mtendaji New Habari

hoyce

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,117
297
Habari kutoka za ndani ya New Habari 2006, kampuni ya Rostam Aziz inayochapisha mahazeti ya Mtanzania, Rai, The African, Dimba na Bingwa zinadokeza kuwa Rostam Aziz amekwishafanya mazungumzo na Prince Mahinja Bagenda ili aingie kwa lengo la kufunga "gavana" kasi ya magazeti hayo ambayo kwa siku za karibuni yalibadili upepo na kuanza kukipiga Chama cha Mapinduzi na Serikali yake.

Kinachogomba sasa ni kwamba, tayari wahariri wa magazeti hayo wamearifiwa kuhusu ujio wa Bagenda, lakini wameapa kuwa akiingia na kutaka kubadili mwelekeo wa gazeti tena, (kwani walikuiwa wanakusudia kushindana kihabari katika soko ili waweze kujilipa mishahara wanayodai kwa miezi kadhaa nyuma), hawatakubali wataweka kalamu chini na kumwachia gazeti lake.

Bagenda hivi karibuni alikuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Karamagi, Taifa Tanzania, ila sina taarifa alitoka lini na alitoka vipi, lakini kwa wakti wake gazeti hilo lilikuwa "maarufu" kwa habari za kuwatetea mafisadi na kuwashambulia wapambanaji dhidi ya ufisadi.

Mtakumbuka, ni kwa sababu hiyo, mengi akabadili Masterhead ya gazeti lake Taifa Letu likawa na font sawa na za Taifa Tanzania na kuandika habari zilizokuwa mwiba kwa mafisadi na wapambe wao. Na kuhusu Uhusiano wa Rostam na Karamagi sina cha kueleza bila shaka Ma-GT wote mnaelewa.
 
Bagenda ameisha hivi kiasi cha kugeuka kama changudoa anayeweza kuchukuliwa na yeyote. Nakumbuka alitunga kitabu cha hovyo kumsifia Kikwete akitegemea kumlipa fadhili kwa kumteua balozi nchini kwao Uganda jambo ambalo Kikwete alimtolea nje. Yeye na Salva Rweyemamu walijivua nguo kuhakikisha Kikwete anauzwa kwa watanzania. Salva alimzidi kete Bagenda akamtumia na yeye kubaki anaadhirika hadi kuanza kuramba matapishi yake. Ama kweli hujafa hujaumbika jua hilo wanangu.
 
Bagenda, kada wa ccm na 'Tumaini Lililorejea', karibu NH, ibane Rai lakini utashusha heshima kwa Mtanzania ambalo sasa ni gazeti makini na lisilopendelea mchana wala usiku
 
Kumbe Taifa Tanzania ni gazeti la Karamagi....!!!!

Hata mimi sikuwa najua hili kwa uhakika, lakini ofisi ya gazeti hilo ilipoungua pale jengo la ushirika Mnazi Mmoja, walihamia kwenye jengo la SmartCard karibu na British council, linalomilikiwa na Karamagi. Hivyo, nadhani hii ni sahihi.
 
Back
Top Bottom