Precision Air imeanguka Shinyanga?

Status
Not open for further replies.

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062
Hizi habari nimesoma somewhere kuwa kuna ajali imetoa Shinyanga maeneo ya Ibadakuli.

Kama kuna maelezo mazuri basi muweke. Nasikia kuwa ni Precision Air na watu kadhaa wamepoteza maisha.

Kama ni kweli basi poleni sana ndugu na jamaa kwa waliopata ajali/kufiwa.
 
Leo ndo mwisho wa kuuza share zao watakuwa nasherekea
 
Kutokana na habari kutoka Facebook kwa Mwana Miyeye, ameweka picha kuonyesha mmoja wa majeruhi akiingizwa hospital.

attachment.php

Ajali Shinyanga.jpg
 
Vipi Mkuu, kwani wewe una shirika lako la upinzani na hawa? Au walishakutibua sana siku za nyuma?

Kwa sasa tujali kwanza watu na si hiyo Mi-vyuma iliyoanguka.
Leo ndo mwisho wa kuuza share zao watakuwa nasherekea
 
Vipi share zao zitashuka? maana hii ina impact kwenye share
Kabla ya ndege kuanguka 1 Share Tshs 475

After ndenge kuanguka na kuuwa wanashare ( I propose 1Share Tshs 100 ili tununue wengi)
 
Hata mimi nimepigiwa cm na mama mmoja. Ni kweli precisionair imepata ajali ilipokuwa inajaribu kutua kwenye uwanja wa ndege wa Ibadakuli. Ulinzi ni mkali mno kiasi kujua kinachoendela ni ngumu. Viongozi wote wa mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa na RPC wako eneo la tukio
 
Ukweli ni kuwa hakuna ajali bali ni mazoezi ya kupima vyombo vya uokoaji wakati wa majanga vinavyoweza kufika na kutimiza wajibu wao inapotokea mkoani shinyanga, hivyo mambo yote yamepangwa na kufanywa kama ajali lakini ni mazoezi japokuwa hali hiyo imezua taharuki kwa wakazi wa Shinyanga.
 
Ukweli ni kuwa hakuna ajali bali ni mazoezi ya kupima vyombo vya uokoaji wakati wa majanga vinavyoweza kufika na kutimiza wajibu wao inapotokea mkoani shinyanga, hivyo mambo yote yamepangwa na kufanywa kama ajali lakini ni mazoezi japokuwa hali hiyo imezua taharuki kwa wakazi wa Shinyanga.​

Yanapotokea majanga ya kweli..tunashindwa kuyazuia na hatufiki kwa wakati..na tukifika hata vifaa....hahahaahaaha...haya kweli Mazoezi
 
hivi ni lazima kuwaweka watu roho juu kisa mnafanya mazoezi??inabidi sasa vyombo husika waache kufanya mambo kaama enzi za ujima siku wanafanya mazoezi watoe taarifa kamili kwa wananchi kwamba ni mazoezi tu ili kuondoa taharuki
 
duh! , hope haijalipuka ndo mana kuna majeruhi, nadra sana kupatikana majeruhi kwenye ajali za ndege.
 
Yanapotokea majanga ya kweli..tunashindwa kuyazuia na hatufiki kwa wakati..na tukifika hata vifaa....hahahaahaaha...haya kweli Mazoezi

Nakumbuka wanajeshi walifanya sana mazoezi pale bandarini na kigamboni,tukajua YEEESS mambo si ndo hayo, lakini yaliyotokea Nungwi kila mtu anafahamu!!
 
Kwenye mazoezi kama haya, ndicho hasa huwa kinatakiwa. Watu wote wanashtukizwa kuwa kuna ajali.

Ukiwaambia watu mapema, basi huwa wanajiandaa kila sehemu utakuta kila kitu kipo tayari.

Ajali nayo huja bila taarifa. Hivyo wanaangalia ufanisi wa huduka kutoka sehemu ya ajali hadi kuwafikisha hospital wagonjwa, huduma ya kwanza, ambulance, zimamoto, msaada wa wananchi nk.

Mwisho ndipo hukaa na kuanza kuangalia wapi kuna matatizo makubwa na nini kirekebishwe.
hivi ni lazima kuwaweka watu roho juu kisa mnafanya mazoezi??inabidi sasa vyombo husika waache kufanya mambo kaama enzi za ujima siku wanafanya mazoezi watoe taarifa kamili kwa wananchi kwamba ni mazoezi tu ili kuondoa taharuki
 
Ndio maana wamesubiria tarehe ya mwisho, ndio wamefanya mazoezi...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom