Popobawa,vipara,albino and now babu wa samunge.

kipindupindu

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
1,053
170
Watanzania tunahusudu ushirikina,tujaribu kujikumbusha matukio ya kishirikina yaliyowahi kutokea nchini:

POPOBAWA;Kuna kipindi ilisemakana kuna jini lilikuwa linawafanyia mchezo mbaya watu(linakula tigo)
VIPARA;Wakati fulani watu wenye vipara waliuawa ikiaminika vichwa vyao vinaleta utajiri
NGOZI;Mkoa wa mbea uliwahi kuwa na matendo ya uchunaji ngozi ambazo zilihusishwa na utajiri.
VIKONGWE;Maeneo ya shinyanga wanawake wazee wenye macho mekundu walituhumiwa kuwa wachawi hivyo walitafutwa na kupigwa mpaka mauti.
ALBINO:Ni mwaka jana tu tatizo la Mauaji ya walemavu wa ngozi Albino walikuwa wanawindwa kama swala ikiaminika viungo vyao vinaleta utajiri.
BABU WA LOLIONDO/TIBA YA VIKOMBE;muasisi wa tiba ya magonjwa sugu kwa kutumia kikombe kimoja tu cha dawa.kwa sasa wanaibuka waganga mbalimbali wanaotoa tiba ya namna hii.

Je nchi yetu ni ya wachawi au believers?
 
Babu wa Loliondo ni tofauti na hayo mengine na hawezi kufananishwa nayo. Yeye haui mtu, wala habaki mtu - anatoa kikombe cha dawa aliyooteshwa na katika briefing zake anajaribu kutibu pia roho. Kumlinganisha huyu na wauaji ni kutomtendea haki!
Hayo unayotaka yalinganiswe na babu hufanyika kwa siri , lakini babu mambo yote hadharani, hata mti anaoutumia ameuotesha pale nyumbani kwake; si siri. Dawa inachemshwa hadharani na kugawiwa hadharani.
Serikali inajikusanyia kipato kutokana na shughuli za babu wa Loliondo, je uliwahi kuona serikali inakusanya ushuru kutokana na hayo mengine?
 
yaani hujasikia kama watu wamekufa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom