Pongezi jiji la Arusha

MASIGA

Senior Member
Aug 29, 2015
130
281
Katika siku ya kilele cha mbio za MWENGE zilizohudhuriwa na maelfu ya viongozi na wananchi kutoka Pande zote za Nchi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira, Vijana Jenister Mhagama alieleza kuwa ktk Kanda Namba 1 inayojumuisha Mikoa mizito Yaani Dar,Arusha,Mbeya,Mwanza, Kilimanjaro, Geita na Songwe washindi ni Jiji la Arusha!

Ninaandika kutoa pongezi hizi fupi kwa Uongozi wa Jiji nikianza na Dc- Fabian Dakaro, Mkurugenzi Dkt Maulid Madeni na DAS-Kihenzile Mwakiposa! Kikosi hiki kilichosheheni viongozi watulivu, wachapakazi wasio na mawaa, wasio wapenda media kimeweza kufanikisha jiji kuongoza.

DC Dakaro kijana mpole asiye na hila na mnyenyekevu amejielekeza kwenye kazi zaidi tofauti na viongozi vijana wezake wengi ambao hata wakikamata panya anaekula nguo ndani huita media.

Nilipata nafas ya kuzungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya sherehe ya Jiji la Arusha ili kujua siri ya ushindi huo! Tofauti na Wilaya nyingi ambazo hukaa kujadili mambo juu juu, Arusha ni tofauti.

Ukiacha vikao vya kila kamati vinavyokaa kila wiki, Jiji Lina vikao vya aina tatu. Kikao kikuu, kikao cha Tathmini na ufuatiliaji na kikao cha kisekta. Kamati kuu inaongozwa na DC mwenyewe , Kikao cha uthamin huongozwa na DAS wake huku vikao vya kisekta vikiongozwa na Mkurugenzi.

Aidha, Arusha inawatumia vyema sana viongozi wa Chama akiwemo Katibu Wilaya, sekretariet na uongozi wa vijana. Chama hutumika kama jicho ktk kubaini mapungufu na hivyo kutoa nafas ya kurekebisha mapungufu hayo mapema. Lakini kilichonivutia zaidi kwa Daqaro ni ziara za mara kwa mara katika kuikagua na kubaini mapungufu katika miradi hiyo.

Mwisho ni namna anavyodhibiti mianya ya rushwa katika kila idara. Ubora wa maandalizi, miradi yenye viwango, eneo la mkesha lililosheheni watu mpaka asubuhi naamini ni moja ya sababu zilizopelekea ushindi kwa Jiji hilo!

Kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuunganisha Jiji hilo, vyombo vya dola pamoja na taasisi zingine zimekuwa kitu kimoja na hivyo kurahisisha ushindi.

DC huyo asiye na tambo, majivuno wala kujikweza pamoja na wasaidizi wake walistahili kabisa nafas hiyo ya kuwa Na 1 tena sio ktk mwemge tu bali ktk kila kitu! Kama walivyoshindanishwa Ma-RC, Natamani sku moja ifanyike tathmini ya utendaji kazi kwa Wilaya zote ambapo naamini Wilaya (Jiji ) la Arusha litakuwa kinara katika kila eneo.

Kila la heri Dakaro na timu yako!
 
Back
Top Bottom