Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,243
- 12,770
Tanzania ukiifuatilia sana utaona watu wengi wanaangalia mambo kinyumenyume sana. Sijui huwa sababu ni nini?
Pombe(Ethanol) ni sukari iliyogeuzwa kwa fermentation. Pombe ina nguvu kama tu chakula chenye wanga.
Inasemwa kuwa mtu anapokunywa pombe, mwili unaacha kutumia mafuta na wanga kama chanzo cha nguvu na kuanza kutumia pombe. Kwa hiyo mtu akinywa pombe mafuta yanazidi kutunzwa mwilini mwake.
Mahitaji ya nguvu ya mwili wa binadamu kwa siku ni 2,500 kilocalories kwa mwanaume na 2,000 kilocalories kwa mwanamke. Na wastani wa nguvu zilizopo kwenye 100mls za pombe kali(40ABV) ni kama 200kilocalories. Kwa hiyo mtu anayemaliza mzinga wa konyagi anaweza kupata kilocalories 1,000. Karibu nusu ya mahitaji yake ya siku ya nguvu. Hiyo inamaanisha kuwa kiasi kama hicho cha mafuta kitaenda kujijaza mwilini mwake na kuleta unene.
Pia pombe huwa ina tabia ya kuleta hamu ya kula. Ukipiga konyagi na nyama choma au kitimoto au hata ugali maharage, kitambi njenje.
Kwa upande mwingine. Bia hizi lite, moja kwa wastani ina kilocalories 110. Nazo si za kufakamia. Maana ili kuepuka unene mbovu inatakiwa kutozidisha kilocalories 2,500 kwa siku. Sasa ukipiga lite 10 tayari una 1,100Kcal. Bado hujanywa chai, ugali mchana na nyama choma usiku.
So, si kweli kuwa pombe kali zinapunguza unene. Ukweli ni kuwa ni chanzo kikubwa cha unene.