Polisi yakiri kuwa chanzo ucheleweshaji haki

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Kamishna wa Polisi, Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi, Shaban Hiki, amesema licha ya Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufanyia kazi kwa wakati sampuli inazozipokea, wataalamu na askari wa upelelezi huchelewa hadi mwaka kuzichukua na kuchelewesha haki kutendeka.

Amesema licha ya kuwapigia simu na kuwaandikia barua ili wafuate majibu, wakati mwingine majibu hayo hukaa miezi sita hadi mwaka bila kuchukuliwa na kwamba tatizo hilo pia ni chanzo cha mrundikano wa majadala ya mashauri ya haki jinai ambayo hayafanyiwi kazi.

Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo mjini Iringa jana akizungumza na wadau wa mnyororo wa haki jinai, wakiwamo askari polisi, mahakimu, madaktari na waendesha mashtaka wa mkoa wakati wa mafunzo maalum yaliyolenga kuhakikisha usalama wa uchukuaji, usafirishaji na utunzaji wa sampuli za uchunguzi wa kimaabara.

Kamishna Hiki alisema changamoto hizo zimeilazimu Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kati Dodoma, kujadiliana na wadau hao.

CHANZO: Nipashe
 
"Amesema licha ya kuwapigia simu na kuwaandikia barua ili wafuate majibu, wakati mwingine majibu hayo hukaa miezi sita hadi mwaka bila kuchukuliwa na kwamba tatizo hilo pia ni chanzo cha mrundikano wa majadala ya mashauri ya haki jinai ambayo hayafanyiwi kazi."
 
Hii nayo hufanyika na baadhi ya wapelelezi kimkakati ili kushawishi RUSHWA.
Kuna wengine watasingizia hawana nauli ya kufuata majibu, sasa hapo kama wwe ndiyo mwenye kesi,na kama hayo majibu yana ku fever wwe lazima utoboke mfukoni,la sivyo yatakaa hadi miezi 6 kwa Mkemia! Rushwa ni adui mkubwa wa haki!!
 
Back
Top Bottom