GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,974
- 6,744
Siikatai kuwa kuna Askari Polisi wasio waadilifu! Karibia kila taaluma kuna watu wasiozingatia maadili ya kazi/taaluma zao
Kule nchini Marekani, Polisi mmoja alibaini kuwa leseni ya udereva wa kijana aliyemsimamisha ilikuwa imeisha wakati wake. Alipomwuliza sababu za kuendesha gari huku leseni ikiwa imeshaisha wakati wake, alijitetea kuwa anatokea jimbo jingine nchini Marekani na kilichomfanya awepo hapo ni kusoma chuo. Alikuwa ameachishwa kazi siku chache zilizopita hivyo hakuwa na hela ya kulipia leseni.
Alimjulisha huyo Polisi kuwa alikuwa anaelekea kwenye usaili wa kazi.
Askari Polisi aliuona utetezi wa huyo kijana kuwa una mashiko. Alijikuta njia panda kama amwathibu kwa mujibu wa Sheria au amwache aendelee na safari kinyume cha Sheria.
Baada ya kutafakari kwa muda, aliamua kulipaki pembeni gari lake na kukamata usukani wa gari la huyo kijana na kumpeleka alikokuwa akienda, kwenye usaili.
Walifika eneo la tukio kwa kuchelewa kidogo, kwa hiyo aliamua kuwafuata viongozi wa hiyo Kampuni na kuwaomba radhi kwa kumchekewesha huyo kijana kufika kwenye usaili. Aliwaeleza kilichompelekea kumchekewesha na akaeleweka.
Huyo kijana alifanikiwa kufanya "interview" na kufaulu. Alipata kazi, na pia, alifanyiwa mpango wa kupata leseni ya ya muda wakati akikusanya hela ya kukatia ya kudumu.
Hii habari nimeisoma kwenye mtandao wa Quora.
Ingawa tukio hilo lilitokea Marekani, naamini hata hapa nchini kwetu kuna Askari wengi wema wa kupigiwa mfano.
Ninasema hivyo nikijua ninachomaanisha. Nimeshakutana na wa aina hiyo zaidi ya mara moja.
Tujizoeshe kuyasema mema ya Askari wetu kwa kadiri wanavyojitajidi kutenda kiusahihi.