Polisi wawili wauawa kwa mapanga na wananchi wenye hasira Ngara; kituo cha polisi chachomwa moto!

RIP marehemu wote. Mimi sina comment hapa inawezekana polisi ndio walikuwa na makosa au raia ndiye alikuwa na makosa maana muamba ngomba uvutia upande wake.
Mara kadhaa nashuhudia raia wakivimbiana na polisi na mara nyingine raia wakitamba kuwapiga polisi wanadharaulika.
Na mara nyingi pia nimeshuhudia polisi wakiwaonea raia.
Kuna matukio mengi nimeshuhudia polisi wanakosa jinsi inabidi watumie risasi za moto.
Lakini la mtu mmoja kupigwa risasi 2 hili lina mashaka lakini pia haingii akilini wampige risasi tu wakati wa kubishana kuna mengi yamejificha nyuma ya story maana mtu huandika story kwa maono yake
 
[h=1]Polisi wawili wauawa Ngara[/h]


polisi_kituo.jpg
IGP Said Mwema.

Na Mwandishi Wetu (email the author)

Posted Jumapili,Decemba16 2012 saa 8:14 AM

Kwa ufupi

“Wananchi walimvamia yule askari aliyebaki pale gereji na kuanza kumkata kwa mapanga na kumpiga mawe hadi akafariki dunia,” alisema.









WANANCHI wa Kata ya Mugoma, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamewaua askari polisi wawili na kuchoma moto Kituo cha Polisi Mugoma kwa madai kuwa polisi hao wamemuua kwa kumpiga risasi mwananchi mwenzao bila hatia.


Tukio hilo la lilitokea jana mchana wilayani humo na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi.

Akizungumza wakati akielekea eneo la tukio, Kamanda Kalangi alisema: “Tukio limetokea Kijiji cha Mugoma, sina details (maelezo ya kina), kwa sababu ndiyo nakwenda huko, ila nikifika ndipo nitajua nini kimetokea, nitatoa maelezo kwa kina.”

Habari zilizorushwa na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC), jana jioni zilieleza kuwa askari polisi waliouawa ni Koplo Pascal na Konstebo Alex wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilayani Ngara.

Katika taarifa hiyo ya BBC, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Costa Kanyasu naye alithibitisha vifo vya askari hao na kueleza kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi kujua ukweli wa tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kujua kama askari hao ndiyo walimpiga risasi mwananchi huyo.

Ilidaiwa kuwa polisi hao walifika katika Kijiji cha Mugoma kwa lengo la kukagua pikipiki mbovu na zisizokuwa na usajili.

Walipokuwa katika ukaguzi huo walifika katika gereji moja na kukuta mmiliki wake akitengeneza pikipiki, wakamtaka aipeleke kituoni kwa maelezo kuwa ilikuwa mbovu.

Ilidaiwa kuwa fundi huyo aligoma kutekeleza amri hiyo na katika ubishi, polisi mmoja alimpiga risasi na kufariki dunia papohapo.
Kitendo hicho kiliamsha hasira kwa wananchi waliokuwa jirani na eneo hilo ambao walianza kujikusanya katika eneo la tukio.

Mmoja wa watu mashuhuda wa tukio hilo, Mwandishi wa Habari wa Redio Kwizera iliyopo wilayani Ngara, Joyce Ngalawa alisema kuona hivyo, polisi anayedaiwa kufyatua risasi alikimbia na kujificha katika nyumba iliyopo jirani na gereji hiyo, huku akimwacha mwenzake.

“Wananchi walimvamia yule askari aliyebaki pale gereji na kuanza kumkata kwa mapanga na kumpiga mawe hadi akafariki dunia,” alisema.

Alisema baada ya mauaji hayo, wananchi hao walikwenda katika nyumba aliyokuwa amejificha askari wa pili na kutishia kuichoma moto iwapo angegoma kutoka.

“Mmiliki wa nyumba ile baada ya kuona wananchi hao wanataka kuichoma moto nyumba yake, alimtaka askari huyo atoke nje. Alipotoka tu, wananchi walimvamia na kuanza kumpiga mawe na kumuua,” alisema.

1 | 2 Next Page»
 
Polisi wetu wajifunze kubadilika na mazingira. Naomba wahusika watumie Polisi wenye akili timamu na wasio na uroho wa dhuruma maeneo ya mipakani.

Pili watumia BODABODA ni janga la kitaifa. Siasa na uhaba wa ubunifu vitasababisha tufe wengi. Ikitokea ajali kati ya gari na BODABODA bila kujali nani mwenye kosa hawa jamaa wanajimobilize na kutoa hukumu papo kwa papo. Hapa tunahitaji maamuzi magumu. Sheria za parabarani kwao ni msamihati.

Kazi kweli kweli.
 
Sipati picha. 'Pikipiki yako ni mbovu, twende kituoni - sitaki; akapigwa risasi'!. Au kuna maelezo mengine...? Labda tusubili taarifa kwa kirefu kutoka pande zote mbili.
 
Taarifa ipi ni sahihi sasa? Bodaboda alisimamishwa brbrni ndo akapigwa risasi, raia (fundi pkpk)aliyeuwawa alikuwa akikataa kupelekwa polisi au alipigwa risasi akiwa kituoni? Tanzania kufika huko bado, tunalazimisha kufika kufika huko kwa wote POLISI NA RAIA. R.I.P. MAREHEMU WOTE.
 
Hili liwe fundisho kwa watu wa maeneo mengine tusikubali uonevu wa polisi...vinginevyo tutakwisha
 
Hili jeshi alilopewa shemeji mtu litawamaliza raia wasio na hatia.
Mungu niepushe na hawa mumian polisi.
.
 
bado tunaambiwa tanzania ni nchi ya amani!!!!!!!!!! mauaji hayo yawe somo la mwisho kwa askari, viongozi na wananchi wote kwamba kila mtu ana haki ya kuishi, kulindwa na kuheshimiwa. yoyote asiyetimiza hayo asitegemee kutimiziwa. Hakuna aliye juu ya sheria.

mtu yeyote, watu wowote au kundi lolote lisichukue sheria mkononi kwani wanaoumia siku moja wataumiza tena vibaya sana
 
Imekuwa kawaida kuskia kuwa "wananchi wenye hasira kali" wamechukua uamzi fulani ( sheria mkononi).

Polisi inabidi wafundishwe jinsi ya kutumia silaha za moto na sehemu ya kutumia nguvu kubwa.Kwa hiyo scenario ya huyo boda boda excessive power (force) was not needed at all lakin ulimbukeni wao ndo umepelekea na wao wapoteze maisha.

RIP boda boda and polisi.
 
Polisi aliyemwua Mwangosi alikuwa na umri wa miaka 23... Naamini kuna majukumu mengine, sio kila mwenye zaidi ya miaka 18 aruhusiwe kuyafanya... kama ilivyo uraisi.
 
waziri Nchimbi yuko wapi? maana alisema akijiuzulu hatuwezi kumpata waziri mzuri kama yeye..sasa huu ndio uzuri aliojivunia...IGP naye ni kama kivuli tu matukio ya ajabu yanafanywa na askari wake yeye hashtuki si ajiuzuru tu asione aibu kazi imemshinda.!!
 
Jamani katika hili hatupaswi kuingiza masuala ya siasa hapa,tunapaswa kujadili hoja hii kwa umakini mkubwa,haya malumbano na hasa mnayoingiza vyama vya siasa kwangu mimi sioni kama yanaweza kuleta utatuzi wa matatizo yanayotukabili sisi kama wananchi,watu wanauawa,wanapoteza maisha halafu kuna baadhi yetu wanaonekana kufurahia hali hiyo kana kwamba wao hayawezi kuwakuta.

Taarifa ninazoendelea kuzipata kutoka ngara ni kwamba hali siyo nzuri na wananchi wanaendelea kuhamasishana ili kuvamia hata kituo kikuu cha polisi cha wilaya ya Ngara ambapo imewalazimu polisi kufunga njia zote za kuingia kituoni umbali wa mita 100 na wana silaha,eneo la Ngara kwa kiasi kikubwa limezungukwa na nchi jirani ya Burundi tena kwa maeneo mengine ni karibu kama kilomita mbili tu ingawa ilipotokea tukio ni kama kilomita 10 kutoka Burundi,hapa watu wasioitakia mema nchi yetu wanaweza kuitumia kusababisha vita na nadhani tunafahamu zote kwamba hili ni miongoni mwa maeneo ambayo silaha za kivita ziko njenje zinaweza kuanza kutumika katika tukio kama hili.

Niombe kwamba hili suala sio la kujadili kimzahamzaha kama ninavyoona hivi.......................


Mkuu upo Sirius? Hebu endelea kutujuza tafadhali, sababu ya kuhamasishana ili kuvamia nizipi? Wanaopeleka mashtaka mapya pia hawaruhusiwi? Wanaotembelea mahabusu wao pia hawaruhusiwi kusogea? Update please?
 
Taarifa za kuuawa Askari wawili, baada ya wao kumuua raiakwa risasi ni matokeo ya kutowajibishwa kwa Askari wote waliowahi kuua, nimatokeo ya IGP kulindwa na Amiri Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama. IGPameelezwa kasoro siku zote zinazofanywa kinyume na maadili ya jeshi hiloamezipuuza. Wameandikiwa Makala, wakazidharau. Sasa wananchi wanaonekanakuchoshwa, Askari akiua raia moja wanaua Askari wawili. Huku ndo mlikuwamnataka tufike? IGP kwa hili sasa Ujiuzulu aje IGP Mwingine ambaye hataingizasiasa kwenye jeshi, kuendelea kusubiri kunakuharibia jina. Tusifurahieumwagikaji wa damu, lakini sasa ni wakati wa kuchukua hatua. IGP Jiuzulu, ajeIGP atakayemwadhibu Shilogile, Kamuhanda, na Askari wote walioua kwa kutumiarisasi wafunguliwe kesi mahakamani kukomesha tabia hii.
 
Taarifa za kuuawa Askari wawili, baada ya wao kumuua raiakwa risasi ni matokeo ya kutowajibishwa kwa Askari wote waliowahi kuua, nimatokeo ya IGP kulindwa na Amiri Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama. IGPameelezwa kasoro siku zote zinazofanywa kinyume na maadili ya jeshi hiloamezipuuza. Wameandikiwa Makala, wakazidharau. Sasa wananchi wanaonekanakuchoshwa, Askari akiua raia moja wanaua Askari wawili. Huku ndo mlikuwamnataka tufike? IGP kwa hili sasa Ujiuzulu aje IGP Mwingine ambaye hataingizasiasa kwenye jeshi, kuendelea kusubiri kunakuharibia jina. Tusifurahieumwagikaji wa damu, lakini sasa ni wakati wa kuchukua hatua. IGP Jiuzulu, ajeIGP atakayemwadhibu Shilogile, Kamuhanda, na Askari wote walioua kwa kutumiarisasi wafunguliwe kesi mahakamani kukomesha tabia hii.

Ni kwa sababu watz ni wapole ushahidi kuwa IGP anatimiza maelekezo wa Raisi upo wazi kabisa sijui tunasubiri nini .Mwisho wa siku tunaanza kuuana wenyewe kwa manufaa ya watawala maana watanzania wanaouliwa, hawa polisi wanaoua na wanaouawa ni watz wenzetu
 
tumeweka hapa vilio vyetu mara nyingi na kwingineko tukiomba serikali ione namna polisi wanavyokwenda na utendaji kazi wao kuwa si salama kwa badae kwao wenyewe na hata kwa familia zao maana wimbi hili la polisi kuuwa watu kuchoma miji ya watu kujeruhi linaweka fundo mioyoni mwa wananchi wanyonge kila siku na wengine wanaoendelea kusubiri msaada wa serikali ukikosekana wanakata tamaa na iko siku yatatokea makubwa zaidi ya haya ya huko View attachment 75339
familia hii imebaki haina namna ya kuishi baada ya mji wao mzima kuchomwa moto kwa bomu na polisi wanaolinda mgodi huko NORTH MARA MINE
View attachment 75340
eneo la ndani la nyumba iliyoteketezwa na moto
View attachment 75341
 
Ni kwa sababu watz ni wapole ushahidi kuwa IGP anatimiza maelekezo wa Raisi upo wazi kabisa sijui tunasubiri nini .Mwisho wa siku tunaanza kuuana wenyewe kwa manufaa ya watawala maana watanzania wanaouliwa, hawa polisi wanaoua na wanaouawa ni watz wenzetu
hapa tunachotaka ni kujua kama wao wamewahi hata kufikiria ni kwa kiasi gani inauma kumwondoa mtu na sidhani kama itakuwa mara ya kwanza itakuwa ni mwendelezo ndio maana polisi wanazoea
 
Back
Top Bottom