Polisi wauwa tena!!!!

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,559
BREAKINGNES ..VURUGU ZAIBUKA UBARUKU WAWILI WAUWAWA KWA RISASI


IGP Mwema
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
RPC Mbeya Advocete Nyombi na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha usalama barabarani James Kombe (kulia)

Watu wawili wakazi wa ubaruku wilaya ya Mbarali akiwemo mmoja aliliyefahamika kwa jina moja la Justine wamekufa baada ya kupigwa risasi ya kichwani huku mmoja akijeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi ya kiunoni wakati wa vurugu kati ya wananchi wa ubaruku na polisi .

Taarifa za uhakika kutoka eneo la tukio zilizopata kuthibitishwa na mkuu wa wilaya ya Mbarali Kanali Cosmas Kayombo na kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi zinadai kuwa tukio hilo limetokea leo mchana baada ya wananchi wa eneo hilo kuzuia lori zaidi ya tani 10 kuingi katika eneo hilo kama serikali ya wilaya ilivyopata kupiga marufuku malori hayo kuingia maeneo yao.

Aliyejeruhiwa kwa risasi katika tukio hilo ametambuliwa kwa jina la Husein na kuwa amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mbarali kwa matibabu.


Pia wananchi hao wameteketeza kituo cha mafuta kinachomilikiwa na mfanyabiashara mweupe aliyetajwa kwa jina la Mnishi pamoja na kuchoma moto lori moja na nyumba mbili za wakazi wa eneo hilo huku polisi wakitumia mabomu na risasi za moto kuwatawanya wananchi hao bila mafanikio .

Hata hivyo inadaiwa kuwa wananchi hao walifikia hatua ya kuzuia lori hilo ambalo ni mali ya watu wenye rangi nyeupe kutokana na kuwepo kwa upendeleo ambapo wananchi wenye ngozi nyeusi wamekuwa wakipigwa marufuku malori yao kuingia eneo hilo kwa usalama wa barabara huku wengine wenye pesa wakiruhusiwa kuingiza malori yao.

Wakati wananchi wakidai kuwa polisi ndio ambao wamehusika na mauwaji hayo na kujeruhi wananchi hao kwa risasi ,jeshi la polisi bado halijasema lolote juu ya tukio hilo na kudai kuwa bado linafanya uchunguzi zaidi.

Hili ni tukio la pili kwa wananchi kuuwawa katika vurugu kati yao na wananchi ambapo tukio kama hilo pia limepata kutokea mjini Arusha ambapo watu kadhaa wameuwawa katika maandamano ya Chadema ambapo polisi walitumia nguvu zaidi kuwatawanya.
 
Back
Top Bottom