Polisi watetea mauaji waliyoyafanya Mbarali

Mbaha

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
697
73
Wana JF Kwa mara nyingine tena polisi wanatetea na kuhalalisha mauji ya raia waliyoyafanya huko Mbarali. Kwa mujibu wa Advocate Nyombi, polisi walilazimika kuwafyatulia risasi wananchi ambao yeye ameuita “umati” baada ya wananchi hao wa Mbarali kuwazidi nguvu. Kwa madai yake, polisi walitumia mabomu ya machozi kutawanya “umati” hadi mabomu yakawaishia bila mafanikio, wakaamua kukimbilia kwenye jengo moja kujificha humo lakini wananchi wenye hasira wakawafuata kwa lengo la kuvunja mlango na kuwaadhibu ndipo polisi walipoamua kuwafyatulia risasi za moto wananchi hao na kusababisha kifo cha mmoja wao. Nyombi alipoulizwa inakuaji wananchi wa kawaida wanakamata lori barabarani alijibu kuwa hilo lilitokea kutokana na kisasi walichonacho wananchi baada ya muwekezaji kuwafungia maji kwa ajili ya kumwagilia mashamba yao jambo ambalo lilisababisha mazao yao kukauka.

Ninachojiuliza, hivi hao polisi walifyatua warning shots ngapi kabla ya kuamua kutekeleza shoot to kill order??? Je hao wananchi walikua ni wengi kiasi gani hadi watumie mabomu ya machozi yote waliyonayo bila mafanikio ya kuwatawanya???


Chanzo: Dira ya dunia - BBC leo jioni.
 
Back
Top Bottom