Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,570
- 19,448
Nimeona picha hii inayohusu ajali ya barabarani hapo Dar. Ingawa maelezo ya picha hayakueleza kama abiria wamepona au vipi, ila nimejiuliza tena chanzo cha ajali hizi na kujidhihirisha kuwa chanzo ni polisi wa trafiki. Askari hao wamekuwa hahangaiki na kuadhibu wavunja sheria za barabarani na mara zote wameng'ang'ania kupokea rushwa na kuwaacha waenedelee kuvunja sheria.