Polisi tusafisheni kadhia hii

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Juzi watu wanaodhaniwa kuwa majambazi walivamia nyumba ya watawa wa Kanisa Katoliki wa Parokia ya Bikira Maria, Mji Mpya, Kipunguni `B' Ukonga jijini Dar es Salaam na kupora Sh. milioni 1.5, Rupia 5,000, Euro 100 pamoja na

sanduku la kuhifadhia Ekaristi Takatifu, kabla ya kupora fedha na vitu hivyo, majambazi hao waliwatishia watawa kwa mapanga na vitu vyenye ncha kali.

Inadaiwa kuwa majambazi hao walikuwa zaidi ya 10 na waliingia katika nyumba hiyo saa 8:00 usiku wa kuamikia juzi na kuanza kuwatishia watawa hao kwa mapanga, nondo na vitu vyenye ncha kali huku wakiwazuba midomo ili kupiga

kelele, waliendesha ushenzi wao baada kukata uzio wa nyumba hiyo na kuvunja geti la nyumba kisha wakawatisha watawa hao raia wa Asia, huku wakiwaamuru kwa lugha ya Kiingereza watoe fedha. Hata hivyo, hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Kama ambavyo imekuwa ni jadi kwamba mvunja nchi ni mwananchi, mlinzi wa parokia hiyo ametoroka baada ya tukio na bado anasakwa na polisi ambao walifika kwenye eneo la tukio usiku husika, pia wanaendea na uchunguzi kwa kuwa hakuna aliyekamatwa hadi sasa.

Mbali na fedha taslimu zilizoibwa, majambazi hayo pia yaliiba pasi mbili za umeme, deki moja ya dvd, laptop moja, printa moja, simu mbili za mkononi na mkoba (briefcase) mmoja.

Tunasikitika kwamba tukio hili limewakuta watu ambao kimsingi jamii inatambua na kuheshimu nafasi yao, yaani ni jambo lisiloingia akilini kuona kuwa taasisi za dini zinavamiwa na majambazi ambao wamekosa utu kiasi cha kuamini kuwa kuna mali ya maana kanisani au kwenye makazi ya watawa.

Tunachukulia tukio hili kama kielelezo kingine cha kuzidi kuporomoka kwa kiwango cha maadili katika jamii, kwa kuwa picha inayoonekana hapa ni kama ya dhana ya ‘mvunja nchi ni mwananchi’. Kuna hisia zenye nguvu kwamba wahalifu hao walisaidiwa na watu au mtu anayefahamu vizuri mazingira hayo.

Tunajua muhalifu hachagui wapi pa kufanya uhalifu, lakini ukiona sasa wanaelekeza nguvu hata kwenye nyumba za ibada, ambako kimsingi hakuna biashara yoyote inayofanyika na wakijua wazi pia kuwa ni kimbilio la wengi katika kusaka tiba ya kiroho wala si kimwili, ni ujinga uliopindukia kuwataka watu wanaofanya kazi hiyo wajisikie kukosa amani na utulivu wa mioyo kwa sababu ya ulafi wa majitu yanayotaka kula bila kutoka jasho. Tunawalaani kwa nguvu zetu zote.

Pamoja na kuwalaani, tungependa kuhamasisha jamii kushirikiana kwa karibu zaidi na vyombo vya usalama, polisi na wengineo, kuwatambua wahalifu hawa kwa kuwa wamo miongoni mwetu; tunasema haya kwa kuwa vifaa vilivyoibwa aghalab vinauzwa mitaani, na ni rahisi kujulikana kama kila mmoja wetu ataamua kuwa mlinzi na mtunza usalama wa taifa letu.

Tunasema haya tukikumbuka tukio la hivi karibuni kabisa la mkoani Morogoro ambako Naibu Waziri wa NIshati na Madini aliibiwa vitu vyake hotelini zikiwamo fedha taslimu, simu, kompyuta na pete. Thamani ya vitu hivyo ilikuwa ni mamilioni ya fedha, lakini haukupita muda vitu hivyo vikakamatwa.

Tunaamini haya katika tukio la watawa, polisi wa Dar es Salaam wataiga kasi ya wenzao wa Morogoro na kuwatia mbaroni waliohusika na wizi huo dhidi ya watawala ili kuwajengea imani wao (watawa) na hata jamii kwa ujumla kwamba Jeshi letu ni imara na linaweza kukabiliana na wahalifu kama hawa wa Ukonga.

Kuna maneno ambayo yamekuwa yanasema mitaani kwamba polisi wanawafahamu wezi wote na kama wakiamua kuwashughulikia kwa hakika wanawapata mara moja.

Dhana hii imejengwa kwa sababu mbili kuu, kwanza kutokana na tabia ya polisi kufika eneo la tukio unapotokea wizi na kutazama wizi ulivyofayika, kama vile zana za uporaji na huishia kusema hawa ni wa kutoka eneo fulani, na kweli wakienda hurejesha vitu vilivyoibwa.

La pili ambalo linafanana na hilo hapo juu, ni pale anapoibiwa mkubwa hakika vitu hivyo kwa kiwango kikubwa hupatikana hasa inapokuwa vinahusu mali ambayo si fedha.
Hali hii inajenga picha kuwa polisi wanawafahamu wezi, wanajua maficho yao na pengine hata mbinu zao wanazijua vilivyo, ndiyo maana inakuwa ni rahisi kukamata mali iliyoibwa kirahisi hivyo.

Tunafikiri polisi wanawajibika kuonyesha kwa vitendo kwamba wapo na wanamudu changamoto za majambazi uchwara kama hawa wa Ukonga waliokwenda kuwapora watawa kwa kutumia mapanga.

CHANZO: NIPASHE
 
dah. . . . . ! Hao wezi wana laana si bure.

Anyway khs polisi acha tu nikae kimya,nikiongea nitajaza page
 
Back
Top Bottom