Polisi mkoani Singida wamemkamata kijana mmoja mkazi wa Arusha kwa tuhuma za kujifanya afisa wa JWTZ

cheusimangala_

Senior Member
Dec 1, 2018
114
174
Polisi mkoani Singida wamemkamata kijana mmoja mkazi wa Arusha kwa tuhuma za kujifanya afisa wa JWTZ mwenye cheo cha Luteni. Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Sweetbert Anjewike amesema baada ya kumhoji kijana huyo alisema yeye ni mkulima ni siyo mwajiriwa popote. #KwanzaHabari
 
Attachments

  • kwanza.PNG
    kwanza.PNG
    123.1 KB · Views: 34
Polisi mkoani Singida wamemkamata kijana mmoja mkazi wa Arusha kwa tuhuma za kujifanya afisa wa JWTZ mwenye cheo cha Luteni. Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Sweetbert Anjewike amesema baada ya kumhoji kijana huyo alisema yeye ni mkulima ni siyo mwajiriwa popote. #KwanzaHabari
Part 6 lini Mkuu
 
Me huwa nashangaa sana! Hivi mtu unaweza ukajifanya na kujitosheleza mwenyewe na ukasavaivu?

Kazi za uaskari zina authentications kibao, mpaka upitie depot ndiyo utazielewa!

Kuanzia kutembea, uanzie mguu gani, vazi hili linaendana na jukumu lipi, vazi gani linavaliwa kwa kuchomekea ama kuchomoa, kofia gani inavaliwa na vazi hili, mpangilio wa vyeo, nani wa kuanza kumuabudu mwingine, salamu ina matamshi gani sahihi, cheo gani kinatakiwa kitembee kimeshika nini mkononi, kiatu aina fulani kinatakiwa kivaliwe kuanzia cheo gani, shati mshono fulani unatakiwa uvaliwe kuanzia cheo gani, shati mikono mifupi huvaliwa juma ngapi hadi juma ngapi, mikono mirefu iwe imekunjwa au imekunjuliwa na huvaliwa siku gani, cheo gani kikiwa uelekeo gani unatakiwa kukipigia saluti shingo na mikono ukiwa umeiwekaje nk nk.

Mtu ambaye siyo askari, kuigiza kuwa yeye ni askari na kukatisha mbele za maaskari wa kada yoyote na magwanda kutwa nzima bila ya kustukiwa ni muhali.
 
Back
Top Bottom