Polisi Kova suala hili linatia shaka kubwa sana

Mwakitobile

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
452
120
Mara nyingi sana tunamshuhudia polisi Suleiman Kova,mbele ya vyombo vya habari hasa televisheni, akijinasibu kuwa,jeshi la polisi limewatia mbaroni, majambazi sugu tena wakiwa na silaha nzito za kivita lakini majambazi hao hawaoneshwi live kwa kudai kuwa kufanya hivyo kutaaribu upelelezi.Je ni upelelezi gani huo?wakati majambazi hayo yamekamatwa na vidhibiti vyote na Je kwanini silaha zioneshwe lakini waliokutwa nazo wasioneshwe hadharani? Kwa mantiki hiyo basi,polisi kova anatufanya tuamini kuwa kuna watu mnawakamata na visu au mapanga lakini katika vyombo vya habari mnasema na mnaonyesha mmewakamata na silaha za kivita,ili tu viongozi wenu wa ngazi za juu waone mnafanya kazi sana na kwa uadilifu mkubwa.Mwisho kabisa,nakushauri polisi kova,punguza kujitwika mzigo wa usemaji kwa jeshi la polisi hata kama lengo ni kupata u-IGP Kwani mara nyingi unatoa misimamo inayoligharimu jeshi lenu.Unakumbuka sakata la Dk ulimboka na kesi ya Jerry Muro ulivyowaacha watu midomo wazi?
 
hivi nan kakuambia ulete uzi wa mwimba taarabu humu gthinker peleka mmu huwa wanafichwa macho tu na kovu anaju huyu kovu anatakiwa icc
 
Kama Saidi atastaafu kwa mujibu wa sheria Kova ana chances sana kuuvaa uIGP ila kama Baba Mwanaisha atamvuta Saidi wastaafu wote 2015 basi Kova asahau uIGP
 
Back
Top Bottom