Polisi Kirumba Mwanza, Mmiliki Mabasi ya Batco wazidi kutesa, kutapeli wananchi Mwanza

Batco hutoa Tsh. Milioni 5 kila mwezi kuwalipa Polisi

POLISI katika kituo cha Kirumba mkoani Mwanza, wameingia kwenye kashfa nzito za upigaji wa pesa kutoka kwa mmiliki wa Mabasi ya Batco ya jijini hapa Baya Kusanja Malagi kwa kuwakamata watu na kuwabambikizia kesi.

Batco amekuwa akiwatumia baadhi ya Polisi kupitia kwa mkuu wa kituo cha Polisi Kirumba, kuwatesa wananchi jijini Mwanza.

Miongoni mwa watu walioonja mateso hayo ni pamoja na familia ya mmiliki wa hoteli ya Tai Five, Wilson Tarimo ambayo imekuwa ikimatwa mara kwa mara kwa maelekezo ya Baya Kusanja na mkuu wa kituo hicho cha polisi.

Baya Kusanja anaamua kutumia jeshi la Polisi kuikamata familia ya Tarimo baada ya kununua hoteli ya Tai Five kwa njia za 'kitapeli' na hoteli hiyo ilikuwa ikimilikiwa na Tarimo.

Baya alinunua hoteli hiyo kwa njia za kitapeli kwa gharama ya Tsh. Bilioni 1 (moja) baada ya kuiba na kutengeneza hati feki ya kiwanja cha hoteli ya Taifa Five kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa benki ya CRDB.

Benki ya CRDB tawi la Mwanza ilikuwa ikimdai Tarimo kiasi cha zaidi ya Tsh. Milioni 500 ambapo iliamua kuuza hoteli hiyo kinyemera kwenda kwa Baya bila taarifa kwa mteja wao (Tarimo).

Baada ya hoteli hiyo kuuzwa na mmiliki wake kwenda Mahakamani kudai haki yake, Baya amekuwa akiendelea kukarabati hoteli hiyo licha ya kesi ikiwa bado ipo mahakamani.

Pamoja na kesi hiyo kuwa Mahakamani, bado Baya amekuwa akitumia Polisi wa Kirumba kuibambikizia kesi familia ya Tarimo kutokana na kesi yake kumkalia vibaya Mahakamani.

Hali ilivyo

Polisi wa Kirumba (majina yanahifadhiwa) wamekuwa wakichukua kiasi cha Tsh. Milioni 5 kila mwezi kutoka kwa mmiliki huyo wa Batco ili kuendelea kuwatesa wananchi.

Polisi hao, wamekuwa na utaratibu wa kuchukua pesa kwa Baya ili kumsadia kutesa wananchi wanaotofautiana nao kitendo ambacho kinalalamikiwa na wananchi wengi wa Ilemela na Jiji la Mwanza.

Pia miongoni mwa watu ambao wanaendelea kuonja mateso hayo ni mke wa Tarimo ambaye amekamatwa leo saa 10:21 karibu na nyumbani kwake.

Leo Mama huyo amekamatwa na Polisi wa Kirumba waliofika jirani na nyumbani kwake ambako ni jirani na hoteli hiyo na kumchukua na kumpeleka kituo cha Kirumba.

Mama huyo alikamatwa leo baada ya kumkataza Baya aliyekuwa na walinzi wake (mgambo), kuchukua mawe yaliyokuwa jirani na hoteli hiyo ambayo ni mali ya Tarimo.

Mama huyo baada ya kukamatwa na Polisi, amepelekwa Polisi Kirumba na kubambikiziwa kesi ya kuiba Trip 50 za mawe zilizokuwa jirani na hoteli hiyo.

View attachment 1255398
Mkuu inaonyesha ni mtu wa karibu sana na huyo jamaa maana una info za kutosha, cha msingi peleka hizi taarifa sehemu husika kwa msaada zaidi anza na takukuru
 
Mkuu inaonyesha ni mtu wa karibu sana na huyo jamaa maana una info za kutosha, cha msingi peleka hizi taarifa sehemu husika kwa msaada zaidi anza na takukuru
Asikuzingue hawezi enda, umeenda kufanya fujo polisi wakakukamata utaenda tkkr kudai Nini? Kesi iko mahakamani siwasubiri hukumu
 
We mchagga wa kishumundu wacha kuchafua watu, Tarimo tapeli la mjini alitaka kuwaibia CRDB bahati mbaya mchagga wao kaondolewa crdb na ngosha sasa maumivu kaanza kuyasikia. Kama sio mambo ya kipumbavu unaamini CRDB wanaweza mtapeli Tarimo? kwa hela gani aliyonayo. Sasa umelianzisha ngoja tukuchimbe vizuri.

Tarimo alimtapeli mkuu wa shule ya sekondari Pamba, mama kashushura akamruhusu kujenga maduka kuzunguka shule kwa mkataba wa miaka mitatu Tarimo na matapeli wenzie wakagushi mkataba na kuwa miaka 99. Tarimo huyuhuyu kajimilikisha jengo la halmashauri akajimilikisha ngosha kampokonya pana jengwa soko la kisasa. Sasa anataka kumdhuruma Batco nyumba yake aliyonunua kupitia Mnada wa CRDB baada ya Tarimo kujaribu kuitapeli bank fedha na kugonga mwamba. Shukuru batco kuinunua kwa 1bn angeweza kuinunua kwa 50m tu.
huo ndio ukweli issue ya mama kashushura naijua vizuri sana
 
Mkuu kuhusu ubia wake na matias manga ulishazikwa kitambo,matias anaendesha goldcrest kwa 100%,istoshe alikua analipa 90m per month alivyochukua kuendesha sio hizo billions ulizo sema.
Ni mtu naemfahamu na hapo hotelini nimeshakuja nae zaidi ya mara 3
Nimesema kuhusu umiliki wa Gold crest na wala sio majengo ya PPF Soma vizuri.
 
Nimeishi Mwanza Jijini Zaidi ya Miaka 15, Tena nimeishi Kitangiri hapo Minazi mitatu karibu na TAI FIVE Kiukweli pamoja na kwamba Mimi siyo Engineer but Hiyo Hotel Haina Thaman ya 5B kama Alivyosema mtoa mada Imezidi sana 2B.. Naona kama Hiyo 1B Aliyotoa Batco ni nyingi sana sema kwa sababu ni kitega uchumi Kwa miaka kadhaa Atarudisha.. But ni Hotel ya kawaida sana kama sikosei ni ghorofa 3. Vyumba vilivyoko hapo havizidi 20.. Hakuna Ukumbi wowote Mkubwa Hapo zaidi ya ule Aliokuwa Anautumia Dk Ndody Enzi zile anakusanya wagonjwa wa tiba mbadala.
Hata 500m ni nyingi
 
Batco hana kosa. Nyumba iliuzwa na Benki. Tarimo awafungulie kesi Benki na siyo kumsumbua Batco. Tufuate sheria ya nchi.
 
Back
Top Bottom