Polisi kasulu mjini inawashiria vijana wawili kwa wiki 2 kwa kesi ya kusingiziwa

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Nov 30, 2022
607
553
Habarini,
Kumekuwa na tabia ya kuwashikiria raia katoka vituo vya polisi nchini bila kosa lolote au pasipo kuwafikisha mahakamani kwa muda mrefu mkoani kigoma.

Wiki mbili zilizopita polisi kasulu iliwakamata vijana wawili kwa majina sospita silvanus na mashaka misuzi kutoka kijiji cha bugaga wilayani humo kwa madai kuwa ni kamchape baada ya kusingiziwa na ndugu aron luseba kuwa ni kamchape waliomchapa baada ya kuwa ametuhumiwa yeye ni mchawi.

Hii ni kinyume na sheria na ni uonevu kwani kama wanamakosa basi wafikishwe mahakamani na kama upepelezi bado ni haki yao kupewa dhamana.

Kwakweli kituo cha polisi kasulu ni moja ya vituo vinavyokamata watu na kuwashikiria kwa muda mrefu pasipo kuwafikisha mahakamani.

Wananchi tupaze sauti dhidi ya polisi kwa uonevu huu sijui wabunge na madiwani tunaowachugua wanatetea haki zipi za wananchi wao iwapo watu wanawekwa ndani muda wote huo na hawafuatilii wala kuwatetea.

Tunaomba waachiwe mara moja.
 
Back
Top Bottom