malimwengu
Member
- Aug 29, 2011
- 21
- 12
Katika hali ya kushangaza polisi kituo cha Chang'ombe wameanza kuuza hisa kwa wahalifu ili nao wawe sehemu ya jeshi hilo.
Hii iko hivi, kuna watu wanatengeneza document feki za kuibia mizigo bandarini na kwenye ma godown mbalimbali. Wakifanya dili hii polisi huabarishwa lakini polisi humuachia mwenye mali. Akishtuka polisi hufanya nae kazi na kuwakamata wahalifu, huchukua pesa kutoka kwa mwenye mali na huchukua pesa kutoka kwa wahalifu na kuwaachia, wote waliowahi kukamatwa na kutoa pesa wameachiwa. Hivi karibuni kuna watu wamekodi gari na kubandika namba bandia kwenda kuiba mzigo, mwenye mali akashtuliwa, akawashtua polisi, jamaa wamekatwa na gari limekamatwa cha kushangaza mwenye gari hajakamatwa bali yupo uraiani ameambiwa atafute milioni tano waweze kumrudishia gari lake na pia akitaka kufanya shughuli zake hizo awaarifu kwanza polisi. Hii dili inapigwa na mtu ambaye namba za gari lake zilitumika anayejulikana kwa jina la Massawe anayeishi Arusha pamoja na OCS CID Chang'ombe.
Jamaa sasa anatafuta hizo milioni tano na ameshaanza kuchangisha ndugu zake ili kununua hisa za kushirikiana na polisi katika uhalifu.
Kumbe kazi ya jeshi la polisi sasa imebadilika kutoka kuwa usalama wa raia na mali zao mpaka kuwa uhakika wa majambazi na kazi zao. Mungu libariki sana jeshi la polisi