Pneumonia kiswahili chake

Enny

JF-Expert Member
May 26, 2009
962
130
Napenda kujua maana ya ugonjwa wa pneumonia kwa kiswahili . Mwenye kujua anielimishe.
 
Homa ya mapafu.
Sasa ukishajua itakusaidia nini?

Hujui inanisaidia nini? naelewa namna ya kuongea kiswahili fasaha bila kuchanganya na kiingereza katika sentensi zangu. Sipendi kuongea KISWA_KING.
 
Katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu iliyotolewa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (Toleo la pili uk. 158), imeeleza maana ya neno "Kichomi" kuwa ni "nimonia" au "mkamba". Ndio kusema unaweza kutumia neno "nimonia" ambalo limetoholewa au "kichomi" au "mkamba".
 
kwa ufahamu wangu ni ugonjwa wa kupooza mwili au kifupi UNYAFUZI

Hapo uko nje saaana. Pneumonia ni kichomi/nimonia. Ugonjwa wa kupooza ule utokanao na vijidudu (si ule unaotokana na kiharusi au stroke) nafikiri ni polio. Unyafuzi nafikiri ni kiswahili cha kwashiorkor-matatizo ya utapiamlo unaotokana na kupungukiwa kwa protini mwilini.
 
Back
Top Bottom