ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,128
- 49,863
Waziri Mkuu akihutubia Wananchi huko Mtwara amewaambia kwamba Serikali ya Rais Samia Imetoa Zaidi ya Shilingi Bilioni 208 Kwa Ajili ya kujenga Shule Mpya za Sekondari Kwa Kila Halmashauri zote 184 Nchini..
Waziri Majaliwa amesema shule hizo Mpya ni maalumu Kwa Ajili ya kupokea Wanafunzi wa Kidato Cha kwanza mwaka 2024 na kwamba Kila shule Imepata kati ya sh.570mln na 600mln ambazo zinatolewa Kupitia mradi wa Sequip..
.........
SERIKALI imetoa zaidi ya Sh bilioni 208 ili zitumike kujenga shule mpya za sekondari kwenye Halmashauri zote hapa nchini ikiwa ni maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani.
Naibu Waziri (OR-TAMISEMI), Deogratius Ndejembi amesema wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliposimama kusalimia wananchi na watumishi wa Halmashauri ya Mtwara Vijijini kwenye kijiji cha Mkunwa, wilayani Mtwara, mkoani Mtwara.
"Halmashauri zote nchini, ziko 184 zimepatiwa kati ya Sh milioni 570 na milioni 600 za ujenzi wa shule mpya za sekondari. Tumewapa Wakurugenzi hadi Novemba, mwaka huu wawe wamekamilisha ujenzi huo ili waweze kupokea wanafunzi ifikapo Januari, 2024."
Akizungumza na wananchi hao na watumishi mara baada ya kuweka jiwe la msingi, Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua kuwa Halmashauri hiyo ni changa na ndiyo maana inapeleka fedha ili kuwawezesha watumishi hao watimize majukumu yao.-Zaidi tembelea
My Take
Hivi Kuna Rais katika Historia ya Tanzania amewahi Jenga shule nyingi Kwa mpigo kama Rais Samia? Mwacheni Rais Samia awafundishe kazi.