Pinda kiboko

Mchundo you have made your point so clear mkuu . Nadhani it is time Upinzani kuanzia huko kwa kasi ya pekee maana siku zinaisha na huko ndiko CCM wanako iba kura pamoja na kuwanyanyapaa wananchi. Mfano Kiteto wameona Mjini walitoa kura lakini kijijini walitishwa na kuamka kubwaga Manyanga.

Siasa za vijijini ni ngumu sana hata kuliko siasa za Bungeni na Mikoa na Kitaifa . Vijijini wana visa na kuuana na hata kuendeana gizani .Siasa za Kule you need to be smart na ucheze ngoma yao vinginevyo watacheka ukiondoka tu wanafanya maajabu yao .Ninajua kwa kuwa mimi ni Mwenyekiti wa Kijiji na si kiongozi ama mwenyekiti nwa Mtaa no ni Kijiji nawajua wananchi walivyo wagumu na wa ajabu .
 
Kuwaambia watu wasio wajibika ni udikteta? Huenda TZ inahitaji dikteta mpenda maendeleo. Wengi wetu tumezidi maneno mengi lakini vitendo hakuna. Lazima ifike mahali, viongozi ambao hawana uwezo wa kudeliver wang'olewe mara moja.

Halmashauri za wilaya zina pesa nyingi tu ambazo laiti zingelitumiwa vizuri, kungelikuwa na aina fulani ya maendeleo huko wilayani. Tatizo ni wizi na capacity ndogo ya watendaji.

Wasiwasi wangu tu ni kwamba Pinda alikuwa huko kama miaka miwili na hakufanya la maana.

Kama anajua sana kuwaambia watu wasiowajibika mbona anamkumbatia Lowassa na Mkapa? Kwa nini asiwaambie ukweli nao? Huu "ukiboko" selective ni usanii wa hali ya juu na unafiki. It is almost just one step from Lowassa's style ya kufukuza watu kazi kutoka jukwaani.
 
Kweli kwenye miti hapana wajenzi. Kwa kusema tu tayari ameshakuwa kiboko.

Hana ukiboko wowote ni kibogoyo tu, mimi mpaka nione amefanya kipi cha kututia moyo, aanze na wale wa Richmondi, kauli yake ya kwanza ilitia wasi wasi sana eti kosa ni pale unaporudia kosa....mmmmhhh karagabaho na ubozi wako
 
Inawezekana ni waandishi wanakuza mno habari, inawezekana pia ni katika hali ya kumpamba sasa (Mkakati) na asipofanya ipasavyo ionekane Bora aliyepita kuliko huyu.

Tangu jina lake kuteuliwa na hatimaye kupitishwa kwa kura nyingi kule Ddm, nasita sana kumkubali Pinda, labda nina tatizo binafsi, sijui.

Inawezekana kabisa Pinda asijihusishe na Ufisadi lakini pia asiwachukulie hatua Mafisadi hapa ndipo napata wasiwasi. hotuba zake kuanzia kule bungeni na kuendelea zimekuwa za kujichanganya sana. labda tuisubiri hiyo task force yake tuone atafanya nini kama haikuwa buying time kuepusha mizengwe zaidi.

Rejea huko nyuma, Mkapa as Mr claen. hatima yake mkuu wa mafisadi. JK, Chaguo la Mungu, Hatima yake mmmmmmm!!!!!!
EL, Mchapa kazi hodari na makini, hatima yake Richmond na sasa Mizengo Pinda, ????????????????

Math: (-) (+) = (-), (-)+(-) = (-), (+) (+) = (+) {FISADI & MWADILIFU)
 
Huyu Pinda alikuwa huko serikalini muda wote wa kashfa ya Buzwagi na Richmond na hakusimama ili ahesabiwe, juzi anasema kuwa watu wamwache Lowasa na Rostam Azizi kwani yaliyopita si ndwele, leo analeta mkwara mbuzi hapa kwa watendaji wa vijijini?! talking from both sides of the mouth! goosh
 
Heshima fundi, nikweli matatizo haya hayajapata mtetezi wa kweli, lakini tukumbuke sehemu kubwa ya haya matatizo yangeweza kushughulikiwa na halmashauri za miji kupitia vikao vya madiwani. msimamizi mkuu wa shughuli hizi ni tamisemi ambapo yeye alikuwa boss, sasa leo kapata wapi klorokwini ya kutibu maradhi haya.

pia kuna hii tabia ya kuwafanyia viongozi wetu mambo ya kipagani, sijui hii tabia itaisha lini? niliwahi shuhudia mkapa akivikwa ngozi ya kenge kule bariadi, leo MP amekalishwa kwenye kigoda, Ile sakrament imekuwa najisi sasa. haya mazindiko ya kipagani hayatawafikisha popote!
 
Heshima fundi, nikweli matatizo haya hayajapata mtetezi wa kweli, lakini tukumbuke sehemu kubwa ya haya matatizo yangeweza kushughulikiwa na halmashauri za miji kupitia vikao vya madiwani. msimamizi mkuu wa shughuli hizi ni tamisemi ambapo yeye alikuwa boss, sasa leo kapata wapi klorokwini ya kutibu maradhi haya.

pia kuna hii tabia ya kuwafanyia viongozi wetu mambo ya kipagani, sijui hii tabia itaisha lini? niliwahi shuhudia mkapa akivikwa ngozi ya kenge kule bariadi, leo MP amekalishwa kwenye kigoda, Ile sakrament imekuwa najisi sasa. haya mazindiko ya kipagani hayatawafikisha popote!

Kipi cha kipagani na kipi sicho?
 
Ni mapema mnoo kuanza kumsifia huyu jamaa hasa ikizingatiwa rekodi za viongozi wa CCM, JK alianza kwa mbwembwe kutembelea wizara na kuchimba mikwara mizito mizito, mapambano na majambazi, Kusimamia baa la njaa kwa michango hapa na pale, akavalia njuga sinema ya mapanki. Magazeti yakamsifu, Bendi zikamwimba hata bongo fleva hazikubaki nyuma.

Leo hii watu walewale na jumuia zilezile zinasikia kichefuchefu hata kusikia jina lake. Sababu ziko wazi:

1. Kupanda kwa gharama ya maisha kinyume na kauli mbiu maisha bora kwa kila mtanzania

Leo hii petroli/diesel imepanda kwa zaidi ya 35 % toka ameingia madarakani.

Bei ya mfuko wa mbolea ni zaidi ya bei ya baiskeli (Hii haijawahi kutokea toka Dec 1961)


Vyakula bei juu (zaidi ya asilimia 40 toka ameingia madarakani)

2. Kuendekeza ushikaji kwenye uongozi

3. Kuendelea kuchekacheka hata kwenye mambo mazito kama ufisadi.

3. Ahadi hewa kama vile kutoa taarifa ya EPA kwa umma na mpaka leo jiiiiii!

4. Hamna hata dalili za njema in some near future.

Kwa hiyo huyo Pinda sidhani kama ana jipya, tena nasikia amekulia ikulu............ sasa sijui kama atakuwa na vision tofauti na wanasisiemu wenzake waliotangulia na waliopo.
 
Hii style ya kuongoza nchi kwa kuchimba mikwara majukwaani na kutoa amri zisizotekelezeka ni kama dini kwa viongozi wengi wa Africa,na inaonyesha jinsi wasivyojua nini wanafanya,hakuna sababu ya kwenda huku na kule kupiga makelele ili watu wafanye kazi au wasiibe,unalaumu wilayani pesa zinaibiwa sana na solution yako ni kwenda majukwaani kuanza kulaumu kila mtu na kuchimba mikwara ya kitoto ukitegemea pesa hazitaibiwa? huyu ndugu anahitaji msaada wakitaalam zaidi kuliko siasa ili kuzuia wizi na unyanyasaji wa wananchi wasiolipa hiyo michango
 
WanaJF
Mambo yaliyoanzwa na aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa ambaye aliachia ngazi mwenyewe baada ya kuzidiwa kete na Richmond, sasa yameanza kuchotwa na mrithi wake, Mizengo Pinda.

Si mnakumbuka kuwa Lowassa alianza fukuza-fukuza akiwa mkutanono. Aliweza kufukuza watendaji mbele ya hadhara, kuwafokea wakuu wa mikoa na hata kuwadhihaki wakuu wa wilaya mbele ya wake, watoto na wananchi wanaowaongoza.

Naye Pinda leo jioni amemtimua kazi Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kabwe huko Rukwa kwa madai ya kutowajibika kwa wananchi.

Pinda alichukua uamuzi huo akiwa jukwaani baada ya eti kuelezwa na wananchi kutofurahishwa na utendaji wa ofisa huyo, hasa kwa kushindwa kuitisha mikutano ya wananchi anaowaongoza.

Hebu tujaribu kuijadili hali hii, je ni bora au ndiyo mambo yetu yale yale ya kushindwa utawala bora?
 

Attachments

  • pinda.bmp
    193.4 KB · Views: 83
Kiongozi mzuri ni yule anayetafakari na kutafiti kabla ya kuchukua hatua. Maamuzi ya kukurupuka yana madhara yake. Je, mtendaji alipewa nafasi ya kujitetea?
 
Kiongozi mzuri ni yule anayetafakari na kutafiti kabla ya kuchukua hatua. Maamuzi ya kukurupuka yana madhara yake. Je, mtendaji alipewa nafasi ya kujitetea?

Hilo moja, lakini la pili ni kwamba je, kiutawala na kisheria ana madaraka ya kumfukuza mtu kazi ki hivyo, au naye anatafuta umaarufu usio na mpango wowote?
 
Nadhani staili hii ya utendaji kazi ina mvuto wa aina yake kwa watawala wa Tz. Hali hii inaweza kuwa nzuri tu iwapo vyanzo vya taarifa inayosababisha wanene hawa kuchukua hatua hiyo ni vya kuaminika na havilengi kuwakomoa watendaji wanaochongewa.Aidha dhana ya utawala bora pia hailengi kulea uozo unaojidhihirisha dhahiri. Mfano mzuri NI HUU WA HIVI KARIBUNI AMBAPO kamati Teule ya Bunge iliyopewa jukumu la kuchunguza Mchakato mzima ulioipa Mkataba Richmond kuleta majenereta ya kuzalisha umeme wa dharura ILIPOWACHONGEA MAFISADI mbele ya Bunge na mara moja wakatimuliwa!
Kwa maoni yangu kwa vile tumechoshwa na utamaduni wa kuwalea viongozi wabovu na wababaishaji utamaduni huu utawaamsha kwa kuhofia kuaibishwa hadharani
 
Hata walimu wakuu wameshaacha mtindo wa kufukuzwa majukwaani!
 
Kata ya Kabwe has been named after Zitto Kabwe na yeye Pinda kawazuga yuko kupambana na wapinzani.Kiongozi wa Kata nadhani anachaguliwa na watu wa kata ile so sina hakika kama Pinda anaweza kumfukuza .Kama ni Mtendaji wa Kata hawa wanapewa ajira na Halmshauri za Wilaya .Je Pinda kaongea na Afisa Utawala wa Wilaya juu ya huyu Kiongozi ?Well wacha tuone .
 
Back
Top Bottom