PINDA dola milioni 53.7, zitatumika kuzalisha umeme wa megawati 8.0

Kokolo

JF-Expert Member
Mar 20, 2008
1,768
2,767
Mikataba mikubwa mibovu kufutwa-Pinda

2008-06-24 12:15:37
Na Boniface Luhanga, Dodoma
Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, amesema serikali inakusudia kuchunguza mikataba yote mikubwa ambayo inaiingizia nchi hasara.

Bw. Pinda alisema uchunguzi wa tuhuma mbalimbali utafanyika huku mkazo zaidi ukiwekwa katika mikataba mikubwa inayoiingizia serikali hasara.

Aliyasema hayo jana alipokuwa akiliomba Bunge kuidhinisha jumla ya Sh. 1,664,839,294,000 kwa ajili ya ofisi yake na Sh. 57,442,490,900 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2008/09.

Alisema katika mwaka huo wa fedha unaoanza Julai Mosi, mwaka huu, serikali itaendeleza mapambano dhidi ya rushwa na watakaobainika, watachukuliwa hatua za kisheria, kiutawala na kinidhamu.

Pia alisema serikali itajenga mazingira mazuri zaidi yatakayowapa wananchi uwezo, ari na ujasiri wa kutoa taarifa katika kupambana na rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali ya umma.

Alisema katika mwaka wa fedha wa wa 2007/08, serikali iliendelea na juhudi za mapambano dhidi ya rushwa ndani na nje ya taasisi zake.

Alisema hadi kufikia Machi, mwaka huu, jumla ya tuhuma 754 zilipokelewa huku tuhuma za mikataba mikubwa na matumizi mabaya ya fedha za serikali zikifanyiwa kazi pia.

Mikataba mibovu ambayo imekuwa ikipigiwa kelele mara kwa mara na wabunge ni ya madini.

Hata hivyo, aliliarifu Bunge kuwa, Kamati iliyoundwa na Rais chini ya Jaji Mark Bomani mwaka jana, imemaliza kazi yake na kutoa mapendekezo yake mazuri.

Bw. Pinda alisema mapendekezo ya kamati hiyo yatazingatiwa katika maboresho ya Sera na Sheria ya Madini na Sekta ya Madini kwa ujumla.
Alisema mwenendo wa ukuaji wa sekta ya madini, umeendelea kuwa mzuri kutokana na kupanuka kwa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini, hasa dhahabu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa umeongezeka kutoka asilimia 2.6 mwaka juzi na kufikia asilimia 2.7 mwaka jana.

Kuhusu sekta ya kilimo, alisema katika mwaka wa fedha wa 2008/09, serikali itatoa dhamana kwa kampuni ya mbolea Tanzania ili iweze kununua na kusambaza tani 150,000 za mbole ya kupandia itakayozalishwa na kiwanda cha Minjingu kabla ya msimu wa mvua kuanza.
Alisema alihakikishiwa na uongozi wa kiwanda hicho kwamba kina uwezo wa kuzalisha mbolea ya phosphate kati ya tani 150,000 hadi tani 200,000 kwa mwaka.

Kuhusu wananchi wanaovamia ardhi iliyopimwa na kuendelezwa kisha kudai fidia, Waziri Mkuu aliwatahadharisha kuwa serikali haitavumilia ukiukwaji huo wa sheria na taratibu za nchi na kwamba haitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu mara moja.

Kuhusu umeme, alisema katika mwaka wa fedha wa 2008/09, serikali itakamilisha ujenzi wa kituo cha kuzalishia nishati hiyo cha Somanga Fungu.
Bw. Pinda alisema mradi huo utanufaisha maeneo ya Kilwa Masoko, Kilwa Kivinje, Somanga, Kibiti na maeneo mengine jirani.
Aidha, alisema serikali pia itakamilisha uwekaji umeme maeneo ya Kilolo, Mbinga, Mto wa Mbu, Bahi, Uyui, Mkinga, Simanjiro na Kilindi.
``Vile vile, kiasi cha dola za Marekani 63.1 kitatumika katika ujenzi wa njia ya umeme wa chini ya maji kwenda Zanzibar,`` alisema.
Alisema dola milioni 53.7, zitatumika kuzalisha umeme wa megawati 8.0 kutokana na nguvu ya maji ya Mto Malagarasi.
Kuhusu hali ya chakula nchini, Waziri Mkuu alisema katika mwaka wa fedha wa 2008/09, serikali imekiongezea kitengo cha Hifadhi ya Chakula (SGR) uwezo wa kifedha wa Sh. Bilioni 26.3 ili kiweze kununua tani 100,000 za mahindi na tani 5,000 za mtama na kuhifadhi kwa ajili ya siku zijazo.


GHARAMA YA MITAMBO YA MEGAWATI(MW) 100= $ MILLION 42.00 REJEA REPORT YA MWAKYEMBE, KWA NINI PINDA ANASEMA GHARAMA YA MW8=$MILLION 53.7 KUNA NINI HAPO????. KWENYE SOKO SASA HIVI GHARAMA YA MW100 IN RANGE FROM $36 MILLION-$43 MILLION. PINDA PESA ZINGINE UNATAKA ZA UCHAGUZI WA MWAKA 2010 AU NINI??

QUOTE FROM MWAKYEMBE REPORT
Mheshimiwa Spika, kwa thamani ya LC iliyofunguliwa kwa Richmond Development Company LLC ya Dola za Kimarekani milioni 30.7 au Tsh 38.4 bilioni, TANESCO ingeweza kununua mitambo mipya yote minne pamoja na kumudu kulipia gharama za kusafirisha kwa meli hadi Dar-es-Salaam. Hivyo ili zipatikane MW 105.6 zilizohitajiwa na TANESCO ingehitajika mitambo sita (6) ambayo ni sawa sawa Dola za Kimarekani milioni 45 au Tsh. 56.25 bilioni badala ya Dola za Kimarekani milioni 87 au Tsh. 108.7 bilioni tulizobebeshwa na Richmond Development Company LLC.
 
Back
Top Bottom