Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Kauli ya Pinda ni kupindisha Sheria
na Asha Bani
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeeleza kushitushwa na kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyoitoa mkoani Iringa kwa kuagiza uongozi huo kuiondoa mahakamani kesi iliyofunguliwa dhidi ya Diwani wa Kata ya Itunundu, kwa madai kuwa wapinzani wataitumia kama mtaji kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Pinda alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akiagiza kufutwa kwa kesi hiyo inayomkabili diwani huyo, Philip Mkumbata (CCM), aliyefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kuhujumu miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji katika kata yake.
Katika maagizo yake, Waziri Mkuu aliutaka uongozi huo uliomburuta diwani huyo mahakamani kusikiliza mashauri hayo nje ya mahakama na si mahakamani kama walivyofanya hapo awali.
Taarifa ya CUF imeeleza kuwa chama hicho kinatambua kuwa utawala wa sheria ni kuendesha mambo kwa kuheshimu, kulinda na kufuata katiba na sheria nyingine za nchi, hivyo wananchi pia wana haki ya kuishi kwa amani katika mazingira ambayo haki zao zinalindwa. Jukumu la serikali ni kuhakikisha kuwa haki za wananchi zinalindwa.
Inaeleza kuwa Watanzania wana-demokrasia wanatambua kuwa maagizo na matendo kama haya yapo mengi nchini na hiyo ndiyo kasoro kubwa ya serikali ya CCM na kwa kipindi chote ambacho imekuwa madarakani kutokana na kuendesha nchi kwa mabavu, vitisho na ukatili.
Chama hicho kinamtaka Waziri Mkuu kuhakikisha kuwa serikali inaongozwa na katiba na sheria katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku na si matamanio binafsi ya viongozi wake, kama inavyofanyika hivi sasa na kwa kipindi kirefu cha CCM kuwa madarakani.