Pinda amfunza Makamu wa Rais unywaji pombe ya kifipa

4.jpg


sababu ya tanganyika kuendelea na muungano wa zanzibar ndo kama hii kudumisha mila na desturi za kibantu na kuondokana na ule ukiritimba wa kimanga wanaofanyiwa wabantu wenzetu huko visiwani

Nilishika kikombe cha chai, umeniumiza mbavu hadi chai kunimwagikia, mambao haya ya wakuu wetu yanafikirisha zaidi ya kuchekesha.

Niambieni hapo angefanya hivyo mheshimiwa Mbowe, Zito, Mnyika, Dr. Slaa magazeti yangepamba habari hiyo na gazeti la Uhuru lingetoa habari hiyo kwa mwezi mzima. Lakini kwa hawa magamba wanafanya jitihada zote kuzima isijulikane.
 


Kuna mirija mitatu ya kufyonza pombe pale, moja ya Pinda, moja ya yule mama na nyingine ya Makamu wa Rais, usipindishe habari, kwani kesho tukikukuta upo unavinjari eneo la machangudoa maana yake unafanyia mahesabu ya kuwapata.

Na huo mtungi kuna siri ile ya maana ya kusumbawanga na maana yake ukitaka kujua nenda pale Mazwi watakueleza maana ya wanga, kule mji mwema mchanganyiko hawajui maana ya sumbuwanga. Ukidharau na kuendelea na safari baada ya kuvuka gati la wanyamapori la Katavi gari likigoma kupanda mlima wa Lyamba lya Mfipa usijejutia.

Kuhalalisha hilo ipo siku ataenda kukagua mashamba na kukuta bangi ikitumiwa na wakinga kama kiungo cha mboga za majani na kushiriki itakuwa ni busara zaidi? Maana cheo si kinga ya uvunjaji wa taratibu za mila, afya na kanuni.

Nimepita pale getini Katavi juzi nikiwa peke yangu na drive hakuna kilichotokea, na sasa hivi nipo Mlowo.

Kuhusu Nguruwe na Bangi, hapo nadhani unajichanganya kama si kuchanganya mambo. Bangi ni haramu kwa mujibu wa sheria za nchi na mtu hatakiwi kuitumia by any means, wakati Nguruwe ni haramu kwa mujibu wa sheria za kiimani na unaruhusiwa kula kidogo kama una njaa.
 
Hiyo inaitwa Chimpumu,kwa kawaida hutiwa maji ya moto na majivu kidogo( kwa kifipa nyau) kama hujahahi kuinywa usijaribu ni kali kweli kweli. Si inaona mh. kijasho kinamtoka.
 
Huyo pinda anamfanyanini mzee wa watu asije anza kucheza kiduku :lol:
 
Nimepita pale getini Katavi juzi nikiwa peke yangu na drive hakuna kilichotokea, na sasa hivi nipo Mlowo.

Kuhusu Nguruwe na Bangi, hapo nadhani unajichanganya kama si kuchanganya mambo. Bangi ni haramu kwa mujibu wa sheria za nchi na mtu hatakiwi kuitumia by any means, wakati Nguruwe ni haramu kwa mujibu wa sheria za kiimani na unaruhusiwa kula kidogo kama una njaa.

Bangi nimeiingiza hapa katika maana ya kujenga hoja ya mmoja alivyotetea utamaduni. Kuna makabila ya kanda fulani yana mapokea ya kutumia bangi kama kikolezo (kiungo) kwenye mboga za majani. Kwa sababu ya bangi kuharamishwa matumizi yake ipo siku kiongozi wa kitaifa akifika maeneo ambayo yana mapokeo ya kutumia bangi basi tutatetea kulinda utamaduni kwa vile watu hao wana utamaduni wa kutumia bangi? Kuhusu la kuvuka geti la Katavi lisikuumize kichwa maana hapa manju anaporidhia audience kuna kitu kinachoitwa pambizo ili kusisimua ukumbi.
 
Kumbe ndo mana macho ya Pinda yako vile yalivyo, Chimpumu si mchezo nduguzanguni
 
2+(2).jpg


Kumbe ndo mana macho ya Pinda yako vile yalivyo, Chimpumu si mchezo nduguzanguni

Umeona ehe! kadiri ya picha hiyo Pinda kisha anza kuonja yupo ulimwengu mwingine, hata hajitambui kwani mkorogo huo uliandaliwa rasmi kuwaweka sawa.
 
Kuna jambo moja muhimu hapa kuelewa juu ya nafasi na mzingira ambayo kiongozi mkubwa kitaifa anatakiwa awe mfano si wa kutunza utamaduni tu ila kutoendekeza mambo ambayo hurudisha nyuma maendeleo.

Kesho hao hao watashinda vilabuni kwa hoja kwamba mbona Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu wakifika tunawaadalia pombe na wanakunywa, iweje sisi? Busara ni jambo muhimu sana..

Nimeongea mara kadhaa kuwa mwana CCM maana yake umechagua kupoteza mwelekeo sahihi wa kufikiri, na hatima yake ndio haya tunayoshuhudia sasa. Unaweza kushangaa mtu ambaye alikuwa na upeo wa hali ya juu anaweza kuanza kufanya kama ana fikiri kwa kutumia masaburi.

Kuwa Kiongozi haikufanyi upoteze the social part of yourself. Nani amekwambia kwamba ukiwa kiongozi ndo usinywe pombe na wanakijiji wenzio? Cha msingi hapa ni kuwaelekeza wajue muda gani wa kunywa pombe na muda gani wa kufanya kazi. Tusipende kuishi maisha ya kuigiza (artificial life) eti kwa vile wewe ni kiongozi ndo usinywe na kufurahia kinywaji na wananchi.....
 
Kuwa Kiongozi haikufanyi upoteze the social part of yourself. Nani amekwambia kwamba ukiwa kiongozi ndo usinywe pombe na wanakijiji wenzio? Cha msingi hapa ni kuwaelekeza wajue muda gani wa kunywa pombe na muda gani wa kufanya kazi. Tusipende kuishi maisha ya kuigiza (artificial life) eti kwa vile wewe ni kiongozi ndo usinywe na kufurahia kinywaji na wananchi.....

4.jpg


Utetezi wako dhaifu, hali hii wamejidhalilisha sana ndio maana vyombo vya habari vimewalinda kutotoa habari hii. Vyombo vichache vimechakachua na kutoa picha fulani ambayo haionyeshi wanavyokuywa pombe katika mkutano wao. Ni jambo la kushangaza serikali kupanga ratiba ya Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuwa na tukio la kwenda kunywa pombe huko mkoani Katavi? Tuna mambo mengi ya kuhangaika ambayo taifa limezama kwenye umaskini sasa wakuu wa nchi wanajiliwaza na kuchochea ulevi wazi wazi na hadharani, hapa tukubaliane bila utetezi bali kizalendo kwamba wameteleza. Wanapashwa kujirekebisha sana tu na inatakiwa waliombe radhi taifa na wananchi kwa kuonyesha mfano mbaya.
 
Mtu ni afya haya ni mambo ya kale sana


2+(2).jpg


Licha ya mtu ni afya au mambo ya kale, lakini cha aibu serikali kupanga ratiba ya viongozi wake kitaifa kwenda huko mikoani kunywa pombe hadharani kwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Waziri Mkuu kushiriki na kuhamasisha ulevi serikali imejidhalilisha mno. Ni dalili tosha kuhamasisha ulevi badala ya kuhamasisha watu uwajibikaji. Busara ingetanguliwa katika hili Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wasingepata nafasi ya kujidhalilisha hivyo. Washauri wao nao wamewategea mtego nao bila kutumia vizuri bongo zao wameingia kichwa kichwa.

Kikwete mwenyewe ameshaingia kwenye mitego kama hii mara kadhaa kufungua mahoteli na kadhalika, ina maana hata mwenyewe hatumii vizuri ubongo vinginevyo kurudia kosa juu ya kosa ni udhaifu.
 
Hiyo pombe ya kuinamia kwenye chungu namna hiyo, madhara ni kuwa ukishamaliza kunywa macho yanaanza kutaka kutoka nje kama mjusi aliyebanwa na mlango. Stop drinking that thing near the pot with your eyes open, lol!!
 
Hii ni dalili ya Utumwa.Ukiona hivi jua anaetuhumu hana asilia,hakika Pinda japo kuna ambayo amenichefua nayo ila kwa hili,umenionyesha kuwa bado ujamezwa na ukoloni mambo leo.Be proud of your origin.Asiyekubali asili yake jua huyo ni mtumwa.Viongozi wengi ndani ya Taifa hili ni Watumwa kupindukia.

Wakishajua kuvaa suti na mashari ya Mark Spenser basi wanasahau mila na desturi za vijijini kwao na pombe zilizowalea wanaziona kinyaa,ni aibu kubwa sana.Ukiona mtu anakandia au zodoa mila na utamaduni [Cultural and Traditional] jua huyo hana kwao.Kikwetu tunasema LA WILELO.Yaani huyu hana asili yupo yupo, hajui A wala BE,yaani ni MFU.Kesho uchumi wa dunia ukisambaratika kwa maana ya kiwanda cha bia kufungwa kwa kushindwa kujiendesha Mtanzania wa asilia ambae amesoma na anaheshimu mila na desturi yake ataludi kwenye pombe yake ya asilia na kuendelea na maisha kama kawaida na sio mwisho wa maisha bali ni mwisho wa kiwanda cha kizungu [Civilization] na ajira ya wakati ya baadhi ya Watanzania wa sekta hiyo.

Katika makabila ambayo yana wasomi kwa maana ya watu waliostaarabika [Civilized] lakini wanapenda kutumia na kuendeleza Pombe yao ya ASILIA hata kama akichaguliwa kuwa UN SECRETARY bado atarudi kuinywa na kuagizia atengenezewe ni WACHAGA NA MBEGE au Mkurya na OBUSARA [TOGWA] au OBULANDI.

Hivyo Utumwa wako Kwa wengine ASILIA hawaichi,Mwenye ASILI JASILI.

Sasa wewe shule umefuata nini kama unaandika pumba kama hizi. Kutumia pombe ya kienyeji na jinsi ya kuinywa ni vitu viwili tofauti. Kinachokera hapa sio kunywa hiyo pombe ya asili lakini jinsi inavyonywewa kwa kutumia mirija ambayo ina uwezekano wa kuvuta pombe kutoka kwenye chombo na kurudisha mabaki kwenye chombo hicho hicho ni hatari sana kwa afya za watumiaji.

Ndiyo maana mnakwenda shule kuelimishwa mambo kama hayo na ningetegemea wewe msomi kuwaelimisha wengine juu ya madhara yanayoweza kuwapata watumiaji wa pombe hiyo kwa mtindo huo.

Kwa namna nyingine hao waheshimiwa hapo walitakiwa kuwa mfano kuwaelimisha hao ndugu zao waliotoka huko walikotoka juu ya madhara ya kutumia mirija hiyo kwa pamoja kwenye chombo kimoja. Kama ni lazima watumie mirija basi kila mtu awe na chombo chake.
 
semeni ha hii sasa

262455_138558696228538_100002232255306_269428_3866715_n.jpg

We mchokozi, kwani muziki wa mdundiko ambao ndio kibwagizo kinacho konga nyoyo za watu hadi kuwa na mvuto mkubwa kwa watoto kufikia hatua ya kupotea wasijue walikotokea sababu ya kufuata mdundiko ni ishara za mkulu kuwa na mvoto kwa kuchangamsha hadhara kwa stretch za rap? Hapa naona pinda ni kujifunza tu maana rap si ngoma ya asili yake, ila mkulu ndo zake maana amekua akiiona na kucheza.

Ngoma ya mdundiko hakuna pombe ya machicha au komoni/kimpumu na pengine mbege, sidhani kama Pinda atastahimili, maana anahitaji nerves ziwe stimulated by alcohol hapo anaweza kuchamnkia microphone.
 
Back
Top Bottom