Pinda akiri polisi wameshindwa kazi!

"Mtoto wa mkulima" kawapiga chini polisi kusimamia zoezi la kuzuia utoroshaji wa sukari nje ya nchi, kisa WANAHUSIKA kufanya escort ya "mzigo".

Rungu wamepewa wanajeshi.

Hapa nina mawazo mawili

1. Kwa hiyo polisi wameshindwa kazi na wakuu wanajua!
2. Hawa wanajeshi nahisi nao wataangukia kwenye rushwa jamani, na wakipotea hawa ndo tumekwisha.

Lazima tukiri Tanzania kuna waziri mkuu jina.
 
PM anatakiwa kufanya maamuzi sasa anamwagiza RPC asimamie ambaye yuko kwenye pay roll ya hili "deal". Alitakiwa kufanya maamuzi palepale polisi wote border toa kama ushahidi upo peleka mahakamani, kama hakuna tafuta simamisha kazi then watakao kuja hawafanyi tena ujinga sasa utakuta hakuna hatua iliyochukuliwa maneno matupu tu

Waacheni waende JW, wale wanakula mawe hawana shida na hivyo vijisenti vya sukari.
 
"Mtoto wa mkulima" kawapiga chini polisi kusimamia zoezi la kuzuia utoroshaji wa sukari nje ya nchi, kisa WANAHUSIKA kufanya escort ya "mzigo".

Rungu wamepewa wanajeshi.

Hapa nina mawazo mawili

1. Kwa hiyo polisi wameshindwa kazi na wakuu wanajua!
2. Hawa wanajeshi nahisi nao wataangukia kwenye rushwa jamani, na wakipotea hawa ndo tumekwisha.
THE PRIME MINISTER DO NOT HAVE BOTH THE POWER TO COMMAND AND THE MANDATE TO INSTRUCT THE ARMY! WHAT HE SAID IS JUST A USUAL POLITICAL CRAP DELIVERED BY CCM!!
therefore:-YOU HAVE BEEN TRAPPED IN CCM CRAPS!!
 
Na ni nani anayezuia makampuni ya madini kusafirisha mchanga nje ya nchi?
 
Kwenye uchumi hii kitu inaitwa arbitrage. Bidhaa inayouzwa Tanzania kwa bei nafuu, Kenya (au nchi nyingine yoyote) inauzwa kwa bei juu, lazima watu wafanye trading kwa kuitoa kwenye bei ndogo na kuipeleka kwenye bei kubwa, ili wale ile tofauti. Hii ndo faida ambayo ndo msingi wa biashara zote duniani!!

Sasa mwenye akili inatakiwa ajiulize kwa nini sukari isafirishwe kutoka Tanzania kwenda nchi jirani? Manake Tanzania sukari ni bei ndogo na nchi jirani sukari ni bei kubwa! Ni kwa nini Tanzania sukari imekuwa bei ndogo na nchi jirani ni bei kubwa? Je soko letu ni huru? Huko inakotoroshewa, ni kitu gani kinafanya sukari iwe mali hivyo? Je tuanzishe viwanda zaidi ili tuzalishe sukari nyingi zaidi?

Utakuta hili ni jambo la muda mfupi tu linalosababishwa na utofauti katika mifumo ya utozaji wa kodi. Inawezekana Tanzania hatutozi kodi, wenzetu wa jirani wanatoza kodi. Hivyo kwetu bidhaa inakuwa nafuu sababu haina kodi! Ikipelekwa nje, hatutozi kodi au inaingizwa kwa njia za panya.

Hili kweli linahitaji "engagement" ya jeshi? Naona hapa ndo tulipofikia, hatujui tufanye nini na wakati gani. Basi viongozi huropoka tu kila wanalojisikia. Ikiwa sukari inatoroshwa kwa sababu hatuwezi kulinda mipaka, basi hakuna jeshi litakaloweza. Polisi na JWTZ yote ni majeshi chini ya Amiri Jeshi Mmoja! Ikiwa polisi wameshindwa, hivi tunafikiri wameshindwa kwa sababu hawana makombora na vifaru?

Hili linatatiza sana juu ya uwezo wa viongozi wetu kufikiri na kutoa kauli kwa umma. Mungu ibariki, Tanzania!
 
"Mtoto wa mkulima" kawapiga chini polisi kusimamia zoezi la kuzuia utoroshaji wa sukari nje ya nchi, kisa WANAHUSIKA kufanya escort ya "mzigo".

Rungu wamepewa wanajeshi.

Hapa nina mawazo mawili

1. Kwa hiyo polisi wameshindwa kazi na wakuu wanajua!
2. Hawa wanajeshi nahisi nao wataangukia kwenye rushwa jamani, na wakipotea hawa ndo tumekwisha.

Pinda na serikali yake ndio walioshindwa kazi.
Iweje mtu unayemkabidhi ulinzi wa mali na raia, linapokuja suala la malipo umpe kiasi asichoweza kujisaiddia?
Chanzo cha hayo yote ni maisha duni polisi waliyonayo.
Ona nyumba zao, watoto wao hata mavazi yao, utawaonea huruma.
Hebu fikiria, huyo unayemwambia alinde hiyo sukari isivuke mpaka, mshahara wake 200,000/ baada ya nyongeza kwenye bajeti mpya.
sasa akipata mtu wa kumpa 1,000,000/= atoe escort unadhani atakataa? kumbuka mshahara huo ni kwa mtu ambaye hajapewa cheo chochote regardless ana miaka mingapi kazini, ana familia kiasi gani anasomesha watoto wangapi.

IMESHINDWA SERIKALI YA KINA PINDA SIYO POLISI KAMA TUNAVYOAMINISHWA NA WANASIASA WASIOJALI USTAWI WA WATUMISHI WA UMMA
 
na ni nani anayezuia makampuni ya madini kusafirisha mchanga nje ya nchi?

swali lako zuri sana.
Pinda anawalaumu polisi kwa kushindwa kuzuia uvushaji wa sukari ambayo kama tungekuwa na mgawo mzuri wa mirahaba ya madini yanayosafirishwa nje ya nchi, tusingelalamika kwa bei ya sukari inayopanda kwa kuzingatia demand and supply kwani bado tungekuwa na uwezo wa kununua bidhaa hiyo.

Shame on pinda na serikali yake
 
"Mtoto wa mkulima" kawapiga chini polisi kusimamia zoezi la kuzuia utoroshaji
wa sukari nje ya nchi, kisa WANAHUSIKA kufanya escort ya "mzigo".
Rungu wamepewa wanajeshi.
Hapa nina mawazo mawili
1. Kwa hiyo polisi wameshindwa kazi na wakuu wanajua!
2. Hawa wanajeshi nahisi nao wataangukia kwenye rushwa jamani, na wakipotea hawa ndo tumekwisha.

Kwa hali hii anasaidia kupunguza ufisadi au anaongeza? Kwa nini
bado tunaendelea kuoneana haya hata kwa mambo mazito kama
haya? Kama hawaamini polisi kwa nini asiwawajibishe kwanza kabla
ya kuamua kuwapa tenda wanajeshi? Hivi nao wakifanya yaleyale
atawapa tenda watu gani?

Dawa si kuwabadilisha, kama ameprove kuwa wameshindwa alipaswa
kuwawajibisha ili iwe funzo kwa wengine, vinginevyo tutaendelea kucheza
maigizo kila siku...
 
Ukiona hivyo ujue nchi imekwisha, chukua chako mapema.

Tunaposema state apparatus, tunamaanisha jeshi, mahakama, polisi. Sasa kama vyote hivyo vimeshindwa, unasubiri nini? Mii nadhani tuingie barabarani tuu, kieleweke, au tufanye opposite yake, tupaki mabegi yetu tujiondokee zetu, bora kuwa mkimbizi kuliko kuishi tanzania

naunga mkono hoja. tukisafisha nchi hii, wakulima na wafanyakazi tutawapandisha madaraja ya utumishi wao sambamba na maslahi yao ili waweze kukabiliana na mifumuko ya bei na waweze kujikita katika kutoa huduma bora kwa umma wao tofauti na sasa ambo wapo kama wanalazimishwa na matokeo yake wanaamua kujilipa kupitia rushwa
 
"Mtoto wa mkulima" kawapiga chini polisi kusimamia zoezi la kuzuia utoroshaji wa sukari nje ya nchi, kisa WANAHUSIKA kufanya escort ya "mzigo".

Rungu wamepewa wanajeshi.

Hapa nina mawazo mawili

1. Kwa hiyo polisi wameshindwa kazi na wakuu wanajua!
2. Hawa wanajeshi nahisi nao wataangukia kwenye rushwa jamani, na wakipotea hawa ndo tumekwisha.

Kumbe huyu jamaa uwa anajua kutoa order sometimes...I think hii ni danganya toto!!!
 
MASILAHI YA JW na polisi yanatofautiana kidogo.
Labda watashindwa kuchukua rushwa kwa kuwa hawajazoea, lakini wakikaa barrier mwezi tu, watakuwa hodari kuliko polisi

Tofauti yenyewe ni kwa wakubwa tu, hawa ndugu zangu na mimi ni kama kawa, familia zenyewe ndo hizi za mjomba na shangazi.
 
nimecheka sana

Basi hiyo avata yako ilinitisha kama nini, hoja yenyewe niliyoitoa ni kama vile ninawaponda hao Jeidaba, nilipoona umejibu kabla sijaisoma vizuri niliminimaizi peji. angalao sasa napumua baada ya kuisoma vizuri post yako.
 
ha ha ha haaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!! Uuuuuhhhhhhhhh!!!!!!!!! Kumbe wanatisha eh?
 
Taarifa za habari leo zimesheheni Tamko la Waziri Mkuu akiwa Bunda: kuwa Jeshi la Wananchi (JW) watumike kudhibiti utoroshaji wa sukari kwenda nchi za jirani kwani kuna taarifa kuwa sasa polisi wanasaidia utoroshaji huo.

Majuzi tu tulimsikia JK akihimiza Wizara ya Maliasili na utalii watumie JW kupambana na majangili sitashangaa na Magufuli akianza kutumia JW kusimamia ubomoaji na Mathayo akawatumia kudhibiti uvuvi haramu na Nundu akawatumia kudhibiti utoroshaji wanyama pori airpoti na Mkulo akawatumia kukusanya kodi na ... Orodha inaweza kuwa ndefu sana ila moja ni hakika haya ni majibu mepesi kwa maswali mazito na uvivu wa kufikiri na kutafakari.

Hivi matamko kama haya yanapotolewa na kiongozi wa ngazi inatuambia nini ikiwa tunajua na wizara ya mambo ya ndani na jeshi la polisi ni sehemu uongozi wake?

Hivi kama somo la uwajibikaji siyo sehemu ya semina elekezi zinazotolewa kila uchao ni kipi kingine kiko huko?

Inanikumbusha kituko kingine cha Sumatra walipoona askari wa usalama barabarani wanazembea wakaajiri Majembe Auction kushika magari mabovu huku wakisindikizwa na askari wa usalama barabarani

Si ingekuwa vema Pinda badala ya kukwepesha wajibu akwataka Waziri Nahodha na IGP wajibu tuhuma za polisi kusindikiza magendo na wakishindwa wawajibike?

Uamuzi huu wa PM nafikiri utakuwa ni mzuri kama serikali itawatumia Jw kusimamia mambo walioshindwa kuyasimamia. Nasema ni mzuri kwa ustawi wa walala hoi wa nchi hii. Kuwa tumia jw kutawapa fursa wapiganaji wa ngazi za chini na maofisa wa ngazi za chini ambao ndio watakao tumiwa katika operationns hizi kujua kuwa viongozi wa serikali na makamanda wa ngazi za juu ndio hasa tatizo la nchi hii. Hivyo basi pengine kuamua kuwaondoa kwa faida yao na watz wengine wanaoteseka kwa sababu ya uongozi huu mbovu. Naunga mkono 100 kwa 100 wa wape kazi hii jwtz
 
Basi hiyo avata yako ilinitisha kama nini, hoja yenyewe niliyoitoa ni kama vile ninawaponda hao Jeidaba, nilipoona umejibu kabla sijaisoma vizuri niliminimaizi peji. angalao sasa napumua baada ya kuisoma vizuri post yako.

Hii avatar yako mbona inataka kufanana na paa la nyumba moja hapa igunga mjini jirani na ofisi ya dc
 
Uamuzi huu wa PM nafikiri utakuwa ni mzuri kama serikali itawatumia Jw kusimamia mambo walioshindwa kuyasimamia. Nasema ni mzuri kwa ustawi wa walala hoi wa nchi hii. Kuwa tumia jw kutawapa fursa wapiganaji wa ngazi za chini na maofisa wa ngazi za chini ambao ndio watakao tumiwa katika operationns hizi kujua kuwa viongozi wa serikali na makamanda wa ngazi za juu ndio hasa tatizo la nchi hii. Hivyo basi pengine kuamua kuwaondoa kwa faida yao na watz wengine wanaoteseka kwa sababu ya uongozi huu mbovu. Naunga mkono 100 kwa 100 wa wape kazi hii jwtz

Na vipi walioshindwa kusimamia ambao ndiyo walipewa dhamana ya kusimamia?
Inamaana waachwe hivihivi bila kuwajibishwa? Nchi hii tunaipeleka wapi kama
inafikia hatua ya kiongozi wa juu serikalini (wa tatu kwa ukubwa kwa mujibu wa
katiba ya nchi) anawaonea haya?
 
Inanipa shaka sana kuwashirikisha JW kwenye ishu ndogo za uzembe wa watumishi wengine. kwa sehemu naelewa nidhamu ya jeshi iko juu. Kuanza kuwashirikisha sana kwenye maeneo ya rushwa ni kuwatia kwenye vishawishi tu. Nadhani tutapoteza hata maana halisi ya majukumu yao, na hao wazembe ndo wapokee mishahara bure? au fedha yao watapewa hao wajeshi? Tangu wakati alipojiuzuru Mwinyi uwaziri wa mambo ya ndani, sijui nani tena ameshawajibika kwa hiari yake mwenyewe. Waliofuata karibu wote ni kwa mbinde mno huku wakishikiwa mabango.
Pinda anapiga kelele na kuwaumbua hawa polisi wadogo, tusikie ana neno gani kwa viongozi wao?
 
Na vipi walioshindwa kusimamia ambao ndiyo walipewa dhamana ya kusimamia?
Inamaana waachwe hivihivi bila kuwajibishwa? Nchi hii tunaipeleka wapi kama
inafikia hatua ya kiongozi wa juu serikalini (wa tatu kwa ukubwa kwa mujibu wa
katiba ya nchi) anawaonea haya?

Mhashamu askofu, naona kama hukusoma na kuilewa post yangu. Kwa kawaida jeshi likishachukua nchi polisi wote ni raia. Na kwa defn ya kule jeshi polisi si wanajeshi ila ni kikundi cha watu kinachofanya mambo yake kwa kufuata baadhi tu ya taratibu za kijeshi. Ndio maana kwenye majeshi yote duniani sina hakika kwa tz kunakaribu kila taaluma muhimu kwa maisha ya kila siku ya serikali (nchi). Kwa mfano walimu wakigoma leo wanajeshi kwa wenzetu wanaweza wakachukua chaki au overhead projectors na watoto wakasomeshwa vilevile, vivyo hivyo kwa madaktari, waongoza ndege n,k. Kwa hiyo walioshindwa kusimamia watawajibishwa accordingly.
 
Back
Top Bottom