Pinda akimsaidia Malima: Tutabadilisha kanuni tuweze kununua mitambo iliyotumika

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Mbunge mmoja alitaka kujua kwanini serikali haibadilishi sheria na taratibu zake ili kuwezesha ununuzi wa mitambo ya kuazlisha umeme ambayo imeshatumika ili iweze kuingia nchini kwa haraka? Naibu Waziri Malima (Nishati na Madini) anajibu kwanza, na Waziri Mkuu anaingilia kati kuongezea uzito...

Last edited by a moderator:
Mzee Mwanakijiji tupe data majibu yakoje na Pinda kasaidiaje, wengine tupo vijijini saa hizi kulijenga taifa hata tv hakuna
 
Nimependa anaposema " swala la upungufu umeme ni nyeti na lazima lichukuliwe na udharura wa pekee"

sasa huu udharura wa pekee ndiyo hugeuka kuwa ulaji wa warafi wachache, na ni kwa nini udharura huu bado upo wakati tatizo hili lina zaidi ya miaka 8?

mi naona hili la umeme si dharura tena bali ni vyema wakubali kuliita janga la taifa.
 
Kwa welewa wangu mdogo, nilifikiri ni rahisi (kiutaratibu na kiuwezo) kwa serikali kununua mitambo mipya (kama wanavyonunua mishangingi mipya) kuliko kusaka hiyo mitambo ya kafa ulaya!! Tatitizo la umeme limekuwa ndio legacy ya utawala wa awamu ya nne, kwa nini watawala wameamua kulifanya suala la dharura na hivyo kutaka kujiingiza mkenge kama sio kuwaingiza walipa kodi mkenge kwa KUPINDA PINDA kanuni ili kununua mitambo KAFA ULAYA. Hapa ninahoji kama mwananchi mbumbumbu (ignorant), pengine wenzetu wateule wana welewa mwingi wa masuala haya.
 
hivi mbona ccm wanakingiaNA vifua nimemsikia PM akiendelea kutoa majibu yake ya faraja kwa watu waliokata tamaa . kweli jamani leo naomba WABUNGE WA JMT WAWEKITU KIMOJA WAMSHINIKIZE NGEREJA AACHIE NGAZI . KWANI AMESHINDWA KUWA ACCOUNTABLE HUYU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MAJIBU YAKE YA KISIHASA ZAIDI
 
Serikali hii ya CCM kupitia Waziri wake anaeshughulikia Umeme, alishatamka kwamba Umeme ni JANGA LA KITAIFA.
kwa uelewa wangu mdogo Suala linapofikia kuitwa Janga la Kitaifa manake ni kwamba njia zote za kulikabili kwa kutumia Akili ya
Binadamu zimeshindikana. Kilichobaki ni aidha zitumike Nguvu za Giza ama Tumgeukie Mwenyezi Mungu tusali.
Kwa sababu haiingii akilini kila siku Viongozi hawa wanatusomea mipango tu ktk karatasi ya Kuwekeza ktk Umeme lkn kinachofanyika ni SIFURI TOA O
 
Hivi, haya ya umeme ni uwekezaji, kwa nini na nyinyi hamnunui mitambo muipendayo mkaja kuwekeza? Kama mmeona serikali imeshindwa na hii ni biashara kama biashara zingine, mnangoja nini badili ya kupika majungu kila siku?
 
ZOMBA we kweli zoba kama jina lako,we wanataka umeme unasema tukawekeze ? na watanzania wangapi wanahitaji umeme na hawana uwezo wa kununua hata jenereta dogo tu,we unaangalia wakubwa tu.Nyie ndo wale watanzania masikini wa akili kazi kutetea matumbo yenu kwa kupitia serekali yenu ya ccm,HATUTAKI POROJO TUNATAKA UMEME.KAMA WAMESHINDWA WAPISHE CHAMA KINGINE KITAKACHO TUHAKIKISHIA HUDUMA YA UMEME INAPATIKANA BASI..huo uzumbukuku wenu bakini nao nyie wachache mnao neemeka sasa
 
Upo sahihi kabisa ndugu yangu, walafi uelewa wao ni mdogo sana
 
Hivi, haya ya umeme ni uwekezaji, kwa nini na nyinyi hamnunui mitambo muipendayo mkaja kuwekeza? Kama mmeona serikali imeshindwa na hii ni biashara kama biashara zingine, mnangoja nini badili ya kupika majungu kila siku?
Kweli wewe hamnazo
 
Back
Top Bottom