picha ya Lord Eyes baada ya kukamatwa pia bado yuko ndani

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,054
6,281
Eyez.jpg abari kubwa weekend hii kwenye website, blogs za burudani na mitandao ya kijamii nchini ni kuhusiana na tukio la rapper wa kundi la Nako 2 Nako, Lord Eyez kudaiwa kuhusika kwenye wizi wa baadhi ya vifaa vya gari la msanii mwenzie Ommy Dimpoz. Habari tulizonazo zinadai kuwa bado polisi wanamshikilia rapper huyo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na kwamba tukio hilo lilitokea jana maeneo ya Kinondoni Manyanya.
Pia kuna taarifa kuwa Lord Eyez alikuwa pamoja na kijana ambaye husema ni mtoto wa aliyewahi kuwa rais wa Zanzibar Salmin Amour (ukweli ni kuwa si mwanae bali aliwahi kuishi na familia hiyo) ambao wote wanashikiliwa. Kijana huyo amewahi kuhusika katika matukio mengine kama hayo ya wizi wa vifaa vya magari.
Jana kupitia Twitter, Ommy Dimpoz aliandika, “Mwizi wetu kasema vitu viko chimbo tandale…naona km naota#LordEyesMwiziWaPowerWindow.”
“Kinachoniuma alidhamiria coz gari yangu anaijua na mizinga akinipiga huwa namtoa.”
“Sio mm tu wiki iliyopita alimuibia kerry mfanyakazi wa clouds tv huku akishirikiana na mtoto wa kigogo mkubwa ambae wanavuta nae madawa.”
Tukio hilo limevuta hisia za wengi hususan wasanii wenzie ambao wengi wanashindwa kuamini iwapo rapper huyo amefikia hatua ya kuhusika na matukio ya wizi.
 
wasanii wa leo njaa tu,huyo ommy mwenyewe kasaidiwa freemasin ndo nafuhu yake leo anamwona mwenzie hovyo sana mla unga.
 
Ila uyo Dogo atemane na iyo ishu cz ikifanya mchezo itamcost mbaya cz uyo Lord nimfalme wa mtaa....!!
 
Ila uyo Dogo atemane na iyo ishu cz ikifanya mchezo itamcost mbaya cz uyo Lord nimfalme wa mtaa....!!

hapana, hili jambo sio la kuweka ushabiki..kama kaiba ni sawa kulaumiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.. binafsi nimesikitishwa na hii habari.
 
anashitakiwa kwa makosa 30 tena yanaweza kuongezeka,ndio kamanda wa polis wa kinondon alivyosema,anausishwa na wiz sehemu zote za parking kama mliman city na kazalika,sijui kama atasalimika
 
hao watoto wa kigogo kama wanavyo jiita waliwahi kumwingiza mjini dada mmoja kwenye nyumba ya amour wakijifanya kuwa inapangishwa akatoa mil 4 wakampeleka kwa mwanasheria fake na kampuni iliyokuwa imefungiwa miaka mingi yule dada alikuja kushituka kuwa ameibiwa baada ya wiki..alikomaa nao angalau aliambulia mil 2..
 
anashitakiwa kwa makosa 30 tena yanaweza kuongezeka,ndio kamanda wa polis wa kinondon alivyosema,anausishwa na wiz sehemu zote za parking kama mliman city na kazalika,sijui kama atasalimika

Mkuu uyo kamanda kaongea kisiasa zaidi, hayo mambo hayaendi ivyo hata siku moja.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Uyu lord eyes kwanza hata kuendesha gari hajui!! Last summer alitaka kunigonga pale njiro complex haliwashi hata andicator linakata tuuu kama shelly ya babaake
Funga uyo!! Asije akakwangua harrier yangu uyo
 
Mbona na wewe kuandika haujui?
 
Back
Top Bottom