Picha Wosia wa Nyerere, Kikwete unavyoakisi mabadiliko ya JPM

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019
MOJA ya mambo ambayo yameacha maswali kwa wadadisi wa masuala ya siasa nchini, ni jinsi Rais John Magufuli anavyosafisha uozo katika sekta mbalimbali serikalini na ndani ya CCM.

Katika mwendelezo wa makala yangu, leo naangalia jinsi Rais huyo anavyofanyia kazi wosia wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na pia Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kuhusu uendeshaji wa serikali na unyooshaji mambo yasiyo sawa.

Wakati Mwalimu Nyerere aliwaasa viongozi waliomfuatia kuchukua yale mazuri ambayo serikali ya awamu ya kwanza ilifanya na kuacha mabaya, Rais Kikwete pia alizungumzia mambo aliyoamini mrithi wake, Rais Magufuli huenda asiyafanye kama alivyokuwa akifanya yeye na kuwapa angalizo watumishi wa serikali alipowaaga pale Mlimani City, Dar es Salaam na kuwataka wajiandae kwa mabadiliko hayo. “Msije mkasema mbona JK alikuwa hafanyagi haya,” Kikwete alisema akiwapa angalizo wafanyakazi kuhusu mabadiliko waliyopaswa kuyatarajia katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Ni mabadiliko hayo aliyoyatabiri Rais Kikwete na Mwalimu Nyerere yanayompambanua Rais Magufuli na viongozi wengine waliomtangulia. Kwa maoni yangu, JPM amejipambanua kwa maamuzi yaliyo kinyume na watangulizi wake si kwa sababu anawabeza au anapingana na watangulizi wake, bali ananyoosha baadhi ya maeneo yaliyokuwa na kasoro kurudisha imani ya wananchi kwa CCM iliyoanza kutoweka kiasi cha kufanya watamani upinzani utawale.

Wengi watakumbuka hali ya CCM ilipokuwa imefikia na kumfanya Rais Kikwete amteue Katibu Mkuu mstaafu, Abdulrahman Kinana kuokoa jahazi kwa kuhuisha chama. Kinana alifanya ziara nchi nzima akiwa na Mkuu wa Idara ya Siasa na Uenezi wa NEC, Nape Nnauye ambaye aliwahi kukaririwa akisema ‘aliitoa CCM shimoni’ kipindi hicho.

Ni katika muktadha huo, Rais Magufuli hakuwa na namna bali kuja na staili tofauti akianza kuomba kura kwa kujinadi binafsi akisema ‘mimi Magufuli, nipeni kura, mkinichagua, serikali yangu… jambo ambalo wengine waliliona kama lilikuwa njia ya kumsaidia kupata kura kwa haiba binafsi kutokana na hali ya chama ilivyokuwa imefikia kiasi cha kufanya wana CCM watembee wameficha fulana zao.

KUONDOA KASORO Ni wazi baada ya kushinda, JPM alipaswa kuondoa kasoro zilizokuwepo ambazo Nyerere aliziita ‘mabaya’ yake au ya uongozi wowote ule (kwani hakuna kiongozi ambaye atakuwa sahihi kwa asilimia 100) na kuendeleza mazuri. Katika moja ya mikakati, JPM ameteua wapinzani wenye sifa kuwa watendaji wa serikali. Mfano ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, waliokuwa ACT-Wazalendo.

Mwingine ni Dk Wilbroad Slaa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania, Sweden na kurudi CCM. Kwa hili JPM amekwenda mbali zaidi ya Rais Kikwete na Benjamin Mkapa ambao waliteua wapinzani kuwa wabunge, Hamad Rashid na James Mbatia lakini hawakuwahi kuwapa vyeo wapinzani ndani ya Serikali Kuu kama sasa.

Kwa jumla, JPM amekuwa Rais asiyetabirika kirahisi na kufanya watendaji wake wawe na wakati mgumu na kuhitaji akili ya ziada kuelewa anataka nini hasa na hivyo kujiongeza. Kwa mfano, watendaji ambao wamekuwa wepesi wa kuomba fedha kwa JPM bila kwanza kuangalia wao wamefanya nini kutumia rasilimali walizo nazo, wameishia kuumbuka. Mfano, hivi karibuni, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa walinyimwa fedha za kujenga mabweni hadi kwanza JPM aone hatma ya waliodaiwa kufanya ubadhirifu katika ujenzi wa bwalo la chuo kwa Sh bilioni 9.

Hata wale wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Morogoro walishangaa JPM alipowaambia wafunge hata taulo kujisetiri wanapooga kama mabafu hayana milango akihoji kama maji yanatoka, nani aliing’oa. KUJENGA NIDHANI YA FEDHA Nionavyo ni kuwa, anachotaka JPM ni nidhamu ya fedha, uzalendo, kulinda raslimali za umma.

Ni wazi anafanya hayo yote katika kuwapa wahusika, changamoto ya kufuata nidhamu ya matumizi ya fedha, muda, rasilimali za nchi na zao kabla ya kuitaka Serikali iongeze nguvu. Ukiacha kwa watendaji wa Serikali, viongozi na wana CCM nao walipaswa kujua kitu ambacho kingetokea baada ya Kinana kustaafu, mtu ambaye angemrithi asingetoka miongoni mwa vigogo wa siku nyingi tuliowazoea bali mgeni.

Nasema hivyo kwa sababu, nionavyo, dhamira ya JPM kama Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa ni kujenga Serikali mpya na chama kipya kwa maana ya sera, dira, katiba, ilani, watendaji, viongozi, staili ya uendeshaji chama ili kufikia malengo yaliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere.

Anataka kurekebisha mabaya yaliyojitokeza katika uongozi wa Mwalimu Nyerere na viongozi wengine waliofuata, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Mkapa, Kikwete na kuendeleza mazuri yao. Ndio maana tumeshuhudia akifumua mikataba ya madini, akiendeleza ujenzi wa Stieglers Gorge tupate umeme, akijenga reli mpya, akifufua shirika la Ndege Tanzania (ATCL), akirejesha viwanda, kuvifufua vilivyokufa na kuwapoka wafanyabiashara wasioviendeleza.

Kwa kufanya haya, huwezi kusema ana chuki binafsi na Mzee Mwinyi au Mkapa ambao walitumia muda wao kumpigia kampeni pia au Dk Kikwete ambaye haachi kumshukuru kwa kufanikisha awe Rais wa awamu ya tano sasa. Yako mengi mazuri anayaendeleza kama elimu bure kwa watoto maskini, ujenzi miundombinu, kwa kiasi kikubwa, amefanikiwa kuisuka upya Serikali kwa kusafisha wezi, wenye vyeti feki, wafanyabiashara ya dawa za kulevya, mikataba mibovu, mishahara hewa na stahili za likizo.

MWELEKEO WA CCM Ni wazi sasa mwelekeo ni CCM ambako tayari amerekebisha Katiba akipunguza wajumbe wa mikutano na ngazi za uongozi akifuta wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) wilaya, kupunguza wajumbe wa NEC, Kamati Kuu (CC) na mkutano mkuu wa Taifa na vikao vingine.

Anatarajiwa kuja na mageuzi zaidi CCM baada ya kukamilisha safu yake kwani kati ya wateule wa zamani, alikuwa amebaki Kinana pekee. KUONDOKA KWA KINANA Ni wazi kuondoka kwa Kinana kutampa fursa nzuri ya kutekeleza ajenda zake, sera, dira na maono yake kufikia dhamira ya Nyerere kujenga Taifa lenye uchumi imara kwa njia ya kujitegemea kwa kutumia raslimali zake, badala ya misaada ya wafadhili yenye masharti lukuki.

Na kama hayo ndiyo maono yake, baadhi ya waliotajwa kumrithi Kinana hawangeweza kufikiriwa naye kwani wanawakilisha muktadha tofauti na wake kwani tayari wana na mizizi ndani ya CCM katika uongozi wa awamu zilizopita. Kwa mfano, Pinda aliwahi kushiriki vikao vya vya juu CCM alipokuwa Waziri Mkuu akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu, NEC huku Nape akiwa amewahi kuwa kwenye Sekretarieti ya Kinana hivyo kuwa vigumu kuendelea naye. Ni kawaida viongozi wapya kuchagua timu yao.

PINDA ‘KIBUBU’ KWA JPM Hata hivyo, kwa utamaduni wa CCM, Pinda anaweza baadaye kuwa silaha ya akiba (kibubu) kwa JPM siku Makamu Mwenyekiti wa sasa, Phillip Mangula atakapostaafu kwani JPM amemtaja kama mtu anayemvutia kwa kutopenda kusemasema tangu alipostaafu.

Ni wazi Pinda kwa umri wake, haiba yake ya upole na historia ya kufanya kazi Ikulu na Nyerere na kuishia maisha ya kijamaa kama mtoto wa mkulima, anaweza kumfaa JPM kama Makamu kwani maisha yake yanaakisi hayo.

JPM anataka waadilifu, wasio na makuu, wasio na mawaa katika maisha yao na ya uongozi, wenye elimu ya kutosha jambo linalofanya mara kadhaa ateue watu wenye elimu ya shahada za uzamivu (phd), shahada ya uzamili, wazalendo, wanaoelewa visheni yake akiakisi unabii wa Nyerere aliyesema ‘watu wazuri (viongozi wasio na doa) wapo wengi tu’ ndani ya CCM.

MWELEKEO CCM YA JPM Ni wazi baada ya Katibu Mkuu mpya wa CCM, Dk Bashiru Ally kuanza kazi kwa kusema hatajihusisha na siasa za jukwaani, bali hizo anawaachia Mwenyekiti (JPM) na Mangula na kujikita katika utendaji, anaonesha mwelekeo ambao JPM anataka kuipeleka CCM na Serikali.

Nionavyo, JPM anataka watu wanaotoa matokeo kutokana na utendaji wao na siyo wanaotumia muda mwingi kupiga siasa. Ndiyo maana alipoingia madarakani alipiga marufuku siasa za majukwaani zisizo na tija akitaka zaidi watu watumie muda huo katika uzalishaji mali.

TANZANIA MPYA Nionavyo, mawazo, malengo na matamanio ya JPM ni kutengeneza Tanzania ya Mwalimu Nyerere ambayo utu wa kila mtu unaheshimiwa, rasilimali zinalindwa na kuwanufaisha wote. Anataka Tanzania ambayo haitategemea wafadhili kuendelea na kuuza uhuru wake, yenye uhusiano mzuri na majirani zake, inayoweza kuwa mhisani na si tegemezi, yenye watu wenye afya, uchumi mzuri ndiyo maana anahimiza ujengaji viwanda na uwekezaji katika gesi asilia, umeme kufikia uchumi wa kati 2025.

Hata hivyo, yote hayo kufanikiwa yatategemea jinsi gani wananchi, wana CCM, wapinzani watakavyomwelewa na kumuunga mkono katika vita ya uchumi kwa uadilifu, kuchapa kazi, kudhibiti fedha, heshima na utu, uzalendo anayohubiri. Kinyume chake, itakuwa vigumu. Hatua za JPM kusafisha nchi zimelenga kutengeneza Tanzania mpya, ya enzi za Nyerere ambapo Ujamaa na Kujitegemea ilikuwa falsafa ya heshima, utu wa mtu, kulinda raslimali zetu.

Ndio maana alimteua Dk Bashiru ili aweze kutekeleza kwa vitendo, falsafa hiyo wakati akiisimamia katika Serikali na kuleta uwiano utakaokamilisha dhamira yake ya kuwa na nchi ya watu sawa, wenye maadili, utu, wazalendo, wanaolinda rasilimali na kuzitumia kwa manufaa ya wote badala ya wachache, mafisadi. JPM ATAFANIKIWA? Ziko sababu nyingi za msingi zilizomfanya JPM aishawishi CC na NEC ya CCM kumteua Dk Bashiru.

Hulka ya JPM, umri mdogo wa Dk Bashiru na kurithishana kijiti kwa vizazi, elimu, umakini, uzalendo, usafi vilichangia apate. Dk Bashiru anaelezwa kutokuwa na makundi zaidi ya kujiegemeza katika siasa za mrengo wa mafundisho ya ujamaa wa Mwalimu Nyerere akiwa mwanajopo wa Kavazi la Nyerere.

Ni wazi, kati ya wateule wachache waliokuwa wanatajwa, Dk Bashiru alikuwa na alama za ziada kutokana na sifa za uadilifu, msimamo wa kutoyumba, uvumilivu, uzalendo na muumini wa ujamaa mambo ambayo yanarandana na JPM.

Hivyo, ni matumaini yangu Dk Bashiru kwa kushirikiana na viongozi wengine wa CCM atakaowateua katika safu yake mpya ya utendaji mikoani hadi wilayani, ana uwezo wa kumsaidia JPM kufikia malengo yake ukizingatia siasa za kimataifa zimebadilika na Tanzania iko imara. - Hali hiyo inaweza kumpa JPM unafuu wa kutekeleza maono yake na kukamilisha hata ndoto za Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete hivyo kuondoka akiwa amejenga Tanzania mpya.

Hata hivyo, aombe Dk Bashiru asipwaye kwani ikitokea hivyo, wahafidhina watapata sababu ya kuanza siasa za makundi na kumsumbua kama Katibu Mkuu, Wilson Mukama alivyowahi kushindwa kutimiza ndoto ya kuisafisha CCM na kuambiwa gamba hilo ‘limeishia kiunoni’. Mukama kama alivyo Dk Bashiru, alikasimiwa kutekeleza ripoti yake.

CCM ilimpa Mukama Ukatibu Mkuu baada ya kuandaa mkakati wa kusafisha uozo uliopewa jina la kuvua gamba. Kilichomsghinda Mukama Kinachoonekana ni kwamba Mukama alishindwa kufikia malengo kutokana na kuathiriwa na siasa za makundi ambazo hitimisho lake lilikuwa kwenye uteuzi wa mgombea urais wa CCM mwaka 2015 ambapo kundi moja liliasi na kuhama CCM.

Ni matarajio yangu, Dk Bashiru atamudu mabadiliko ndani ya CCM kwa kusimamia mapendekezo yote bila kutetereka kwa sababu CCM sasa haina makundi yanayotisha uhai. MAKONGORO KIMATAIFA Hata hivyo, Dk Bashiru bado anahitaji nguvu za watu wenye haiba ya Nyerere kuiuza CCM zaidi kimataifa kama nia ni kuendeleza sera zake.

Hapo mtoto wa Nyerere, Makongoro angefaa. Atakuwa kielelezo kizuri cha kazi ya baba yake inayokamilishwa na JPM kudhihirisha kwamba ujamaa nao unaweza kufanya vyema dhidi ya ubepari. Tusubiri tuone.
 
Last edited by a moderator:
Nyumba yoyote inayobomoka inaanza vizuri kwa kupakwa rangi na kutiwa nakshi na mapambo anuwai..!!
 
Hapa hamna kitu naona shida ni u DC tu.
 
Mwandishi wa makala hii anaweza kuwa Dr.Bushiru mwenyewe. Ushauri wangu, huko bungeni na mahakamani akuache kujisimamie, kama katiba inavyosema.
 
Umechambua vizuri sana
 
Mkuu, unawania nafasi hipi kwenye awamu hii?
 
Back
Top Bottom