PICHA: Waziri wa Ujenzi na Rais Kikwete wazindua barabara za lami mikoa ya kusini 60 km Lindi

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
RAIS Kikwete AFUNGUA BARABARA YA NDUNDU-SOMANGA YENYE UREFU WA KILOMETA 60 MKOANI LINDI



_MG_3181.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Ndundu – Somanga yenye urefu wa kilomita 60, hafla hiyo imefanyika jana Agosti 7 2015 mkoani Lindi.Wengine pichani ni Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najem,Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait, Abrahman Al- Hashim,Mkuu wa Mkoa wa Pwan, Eng. Evarist Ndikilo, wengine kushoto ni Waziri wa ujenzi Mhe.John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza.

_MG_3196.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazia Dkt.Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufunguarasmi barabara ya Ndundu – Somanga.
_MG_3120.jpg
Rais Kikwete akimshukuru Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara baada kuweka jiwe la msingi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
_MG_3149.jpg
Rais wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa pamoja na mkewe Salma Kikwete akimwagia maji mti wa kumbukumbu alioupanda baada ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu – Somanga mkoani Lindi.

_MG_3156.jpg
Wafadhili wa ujenzi wa barabara ya Ndundu-Somanga, Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najim na Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara kwa pamoja wakishiriki kupanda mti wakati wa sherehe fupi zilizofanyika kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
_MG_3220.jpg
Rais Kikwete akiwasalimia na kuwaaga wananchi wa kijij cha Nangurukulu na kumtambulisha Mgomea Urais kwa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akielekea mkoani Lindi.
_MG_3248.jpg
Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akijitambulisha kwa wakazi wa mji wa Nangukurulu,mara baada ya sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga kukamilika mkoani Lindi.
_MG_2860.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mgombea mteule wa Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kufungua barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
_MG_2702.jpg
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa na Mkuu wa mkoa wa Lindi,Mh.Mwantumu Mahiza mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kushiriki ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
_MG_2728.jpg
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh.Bernad Membe mara baada ya kuwasilia katika kijiji hicho Marendengo,ambapo sherehe za uzinduzi wa barabara ya Ndundu-Somanga zilifanyika na mgeni Rasmi alikuwa ni Rais Dkt Jakaya Kikwete.
_MG_2746.jpg
Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akiwa sambama na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh.Mwantumu Mahiza.
_MG_2753.jpg
Wananchi kutoka kijiji cha Marendego na vijiji vyake wakishangilia jambo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu –Somanga yenye urefu wa kilometa 6,inayojengwa na Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa mfuk wa Kuwait pamoja na Opec.Katika unziduzi huo viongozi mbalimbali wa chama na serikal,viongozi wa dini pamoja na watu wengine walishiriki kushuhudia tukio hilo adhimu hapa nchini.
_MG_2758.jpg
Wananchi wakifuatilia tukio hilo
_MG_2759.jpg
Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakati wa ufunguzi wa barabara hiyo ya Ndundu -Somanga yenye urefu wa kilometa 60
_MG_2775.jpg
Wananchi wakifurahia ufunguzi wa barabara hiyo iliyokuwa kero kubwa kwa wananchi wa Mtwara na Lindi
_MG_2827.jpg
Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga iliyojengwa kwa kiwango cha lami na yenye urefu wa kilometa 60 ,Somanga mkoani Lindi.
_MG_2870.jpg
Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh Bernad Membe
_MG_2916.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu – Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.
_MG_2937.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu – Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.
_MG_2987.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu – Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.
_MG_3075.jpg
Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika kwenye kijiji cha Marendego kata ya Somanga za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
_MG_3101.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
 
Kazi anayo ndo kampeni meneja wake ama?
JK jamaa ako Magufuli yani HAUZIKI mbele ya LOWASSA.... Hivi KIKWETE tuambie CCM yako ndani ya miaka 50 Bado tunamgao wa umeme?
Na amini km ukiacha cheap popularity FEDHA ulizotumia kuwaalika machangudoa na wavuta sembe na wasanii wachache kucheza nao DISCO na kupiga mapicha zingetosha japo ata kununua jenerator moja kubwa lenye capacity ya One Megawatt...Au zingetosha kununua vitanda 500 vya wagonjwa....vyovyote vile itakavyokua ni imani yangu kua rais ajae awe CCM au CDM atakua hajitambui km huyu...
 
Kazi anayo ndo kampeni meneja wake ama?
JK jamaa ako Magufuli yani HAUZIKI mbele ya LOWASSA.... Hivi KIKWETE tuambie CCM yako ndani ya miaka 50 Bado tunamgao wa umeme?
Na amini km ukiacha cheap popularity FEDHA ulizotumia kuwaalika machangudoa na wavuta sembe na wasanii wachache kucheza nao DISCO na kupiga mapicha zingetosha japo ata kununua jenerator moja kubwa lenye capacity ya One Megawatt...Au zingetosha kununua vitanda 500 vya wagonjwa....vyovyote vile itakavyokua ni imani yangu kua rais ajae awe CCM au CDM atakua hajitambui km huyu...

kachukue pesa;


umejitahidi BAVICHA , 4UM AU TEAM LOWASSA AU FRIEND OF LOWASA

DG KAPATA 10 BILIONI ; 2 BILION KWA WENYEKUONYESHA JITIHADA
 
Barabara mbovu hiyo hata miezi haitaisha imeharibika,, Magufuli kaanza kampeni kabla ya muda achukuliwe hatua
 
Jamani jamani! Mwacheni mzee Mamvi...mtaua jamani, afya yenyewe ndiyo hivyo tena Tia maji Tia maji!!
 
jk ana kazi sana mwaka huu kumuuza huyu jamaa...

kanda ya ziwa;
kagera
shinyanga
mwanza
musoma
tabora
geita

ushindi.......................
90% kwa magufuri
lowasa 17%

nyanda za juu kusini ,
magufuri 65%
lowasa 32%

coastal
magufuli 60%
lowasa 21%


zanzibar
magufuri 60%
lowassa 39%

kaskazini

lowasa 60%
magufuri 32 %


kanda ya kazi;
magufuri 59 %
lowasa 32%

ziwa magharibi

magufuri 80 %
lowassa 12 %

ndo maana kwa mara ya kwanza ccm wapiga mwizi kimya kimya;

ccm 72 %
ukawa 28 %
 
Haya mambo ya kuomba omba mpaka hela za kujenga ofisi za serikari ndo Lowassa hayapendi
 
haya mambo ya kuomba omba mpaka hela za kujenga ofisi za serikari ndo lowassa hayapendi

no maana kawambia hana msamiati wa kushindwa ; kuzima kashfa ya richmond- pesa kawapa msafisheni badala ya kunadi sera

elimu bure- mko mnaangaika na fisadi wenzenu act - wanavuna wanachama , ccm wanafungua miradi
 
no maana kawambia hana msamiati wa kushindwa ; kuzima kashfa ya richmond- pesa kawapa msafisheni badala ya kunadi sera

elimu bure- mko mnaangaika na fisadi wenzenu act - wanavuna wanachama , ccm wanafungua miradi

Hizo barabara ni kodi zetu
 
kanda ya ziwa;
kagera
shinyanga
mwanza
musoma
tabora
geita

ushindi.......................
90% kwa magufuri
lowasa 17%

nyanda za juu kusini ,
magufuri 65%
lowasa 32%

coastal
magufuli 60%
lowasa 21%


zanzibar
magufuri 60%
lowassa 39%

kaskazini

lowasa 60%
magufuri 32 %


kanda ya kazi;
magufuri 59 %
lowasa 32%

ziwa magharibi

magufuri 80 %
lowassa 12 %

ndo maana kwa mara ya kwanza ccm wapiga mwizi kimya kimya;

ccm 72 %
ukawa 28 %
kazi unayo!...
 
no maana kawambia hana msamiati wa kushindwa ; kuzima kashfa ya richmond- pesa kawapa msafisheni badala ya kunadi sera

elimu bure- mko mnaangaika na fisadi wenzenu act - wanavuna wanachama , ccm wanafungua miradi

Yaani wewe utahangaika peke yako na Bahari mbaya Leo Lizaboni amelala kwa uchovu
 
Back
Top Bottom