PICHA: Vijana Singida wahamasishwa kujiunga na SACCOS (Hakuna Vijana ni Watoto kazi kweli CCM)

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
* CCM ZAWADI ZIKO WAPI? NAPE ALIKUWA SINGIDA ALIONDOKA NA ZAWADI ZOTE?



Mgeni rasmi Katibu wa Uchumi na Fedha Taifa wa CCM Mwigullu Nchemba (Mb) akizungumza na wana CCM na wananchi wa kata ya Itigi na Majengo katika hafla ya mapokezi ya kumpongeza Mbunge Lwanji baada ya kushida kesi yake ya kupinga ushindi wake.



Mbunge wa jimbo la Manyoni Magharibi (CCM) mkoani Singida Mh. John Lwanji amewataka vijana kujiunga kwenye vikundi vya SACCOS ili kujijengea mazingira mazuri ya kukopesheka na taasisi za kifedha.
Mh. Lwanji amesema vijana wakipata mikopo hiyo isiyokuwa na masharti magumu, wataboresha kwa kiwango kikubwa hali zao za kiuchumi na kwa njia hiyo hawatakuwa tena madaraja ya baadhi ya watu wasiokuwa na sifa za uongozi ,kuwatumia kufanikisha malengo yao binafsi.
Mbunge huyo amesema hayo wakati akizungumza kwenye mapokezi makubwa yaliyoandaliwa na wana CCM wa kata ya Itigi na Majengo kwa ajili ya kumpongeza, baada ya kesi iliyokuwa ikimkabili ya kupinga ushindi wake kutupiliwa mbali na mahakama kuu kanda ya Dodoma Mei 20 mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Mh. Lwanji alitumia fursa hiyo kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumpigania wakati wote kesi yake ya kupingwa ushindi wake ilipokuwa ikiendelea na hatimaye kuibuka kidedea kwa kesi hiyo kutupiliwa mbali na mahakama kuu kanda ya Dodoma.
"Huyu mtu ni ndugu yangu (binamu),nimemgaragaza kwenye kura za maoni za CCM, akaamua kutimkia CHADEMA, huko nako nikampiga mwaleka wa nguvu, akaona haitoshi, akakimbilia mahakamani, huko nako kashindwa kupata ushindi, Sasa nadhani atakata rufaa mbinguni, lakini huko ni mpaka mtu ufe ndio unaweza kupata nafasi ya kukata rufaa", alisema na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi.
Mh. Lwanji alifunguliwa kesi ya kupinga matokeo namba 2/2010 na aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia tiketi ya CHADEMA Donald Madeje Lupaa. Kesi hio imetupiliwa mbali na Jaji Mary Shangali kwa madai kwamba ilifunguliwa kwa makosa, kwani sheria iliyotumika kuifungua ilikuwa ni ya mwaka 1971 ambayo ilishapitwa na wakati kufuatia sheria mpya ya mwaka 2010.


Mbunge Lwanji akipokelewa na wana CCM wa kata ya Itigi na Majengo.






 
hivi hiki chama kina matatizo gani...hahaaa madogo wanahamasishwa kujiunga na SACCOS???
 
Haya ndiyo matatizo ya watanzania!
Unapewa scuff ili uende kwenye mkutano huku usoni unaonekana hujala na wala hujui kama utapata mboga ya nguna usiku!!!
 
CCM kila mtu na vyake hata wanachama. Wakati bango moja linasema wabunge mafisadi wajiondoe CCM, lingine linasema tunaimani na viongozi wetu! Kazi kweli kweli
 
dah hii kali mbona mkutano umejaa watoto tu? alafu wamechoka kweli ccm kwishney
 
CCM kila mtu na vyake hata wanachama. Wakati bango moja linasema wabunge mafisadi wajiondoe CCM, lingine linasema tunaimani na viongozi wetu! Kazi kweli kweli

Mmmmh kweli ni jukwaa la ma great thinkers..!
 


Mbunge Lwanji akipokelewa na wana CCM wa kata ya Itigi na Majengo.







huyu dogo wa kulia anaomba nini? uso wake unaonekana kukata matumaini ya kuwa na maisha bora, kinachosikitisha na kushangaza bado anamwabudu shetani asiyemfahamu
 
CCM kila mtu na vyake hata wanachama. Wakati bango moja linasema wabunge mafisadi wajiondoe CCM, lingine linasema tunaimani na viongozi wetu! Kazi kweli kweli

Afu kama mwandiko unafanana katika mabango yote..,
 
dah hii kali mbona mkutano umejaa watoto tu? alafu wamechoka kweli ccm kwishney

Hata hao watoto unaosema wamejaa wako wapi? Mbona ni watoto wachache tu, tena inawezekana walikuwa wanacheza CHANDIMU kwenye hilo eneo ikabidi wawaangalie tu. Na hao vijana wanaohamasishwa kujiunga na SACCOS mbona hawakuhudhuria? au hao wazee watawapelekea ujumbe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
huyu dogo wa kulia anaomba nini? uso wake unaonekana kukata matumaini ya kuwa na maisha bora, kinachosikitisha na kushangaza bado anamwabudu shetani asiyemfahamu

Hizo ni njaa! unadhani yupo hapo kwa hiari ya moyo? hapo kashapata tshirt mwaka huu hanunui tena nguo. sasa anasubiri buku mbili walao leo akabadili mlo. Masikini mtizame alivyochoka kaka wa watu! na hao wabibi Je?? Ee mungu tupe maarifa na ufumbuzi wa matatizo ya taifa hili
 
Mpiga picha nae nadhani ni agent wa magwanda! ka-manipulate hiyo picha ili kuwalenga hao watoto. Nadhani huyo anayehutubia audiance yake iko mbele na sio side kama picha inavyotaka kulazimisha!
 
Back
Top Bottom