Picha: Sheikh fadhil soraga wa zanzibar amwagiwa tindikali na watu wasiojulikana

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
SHEIKH FADHIL SORAGA WA ZANZIBAR AMWAGIWA TINDIKALI NA WATU WASIOJULIKANA - APELEKWA MUHIMBILI KUTIBIWA.





DSC_0011.JPG



DSC_0012.JPG

Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika Chumba cha Huduma ya Mwanzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
DSC_0016.JPG

Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akipandishwa kwenye Gari ya Wagonjwa kwa lengo la kuwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili Dare es Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
DSC_0025.JPG

Wananchi mbalimbali wakishuhudia Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akiwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili Dare es Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar

 
Sio kanisa linahusika kweli

Japokuwa mie ni muislam, wenzetu wa kristu hawana mambo kama haya! Haya ya kwetu sisi tuliozoea majambia na kumwagiaana tindikali. Wakristo wana agenda gani na Sheikh hadi wammwagie tindikali? Huko Arusha si Imam/Sheikh alimwagiwa na vijana waislam? Tuache kuwapakazia wakristo bure! Wenzetu wakiudhika huishia kusema "Bwana asifiwe".
 
Japokuwa mie ni muislam, wenzetu wa kristu hawana mambo kama haya! Haya ya kwetu sisi tuliozoea majambia na kumwagiaana tindikali. Wakristo wana agenda gani na Sheikh hadi wammwagie tindikali? Huko Arusha si Imam/Sheikh alimwagiwa na vijana waislam? Tuache kuwapakazia wakristo bure! Wenzetu wakiudhika huishia kusema "Bwana asifiwe".

Waislamu hawadanganyiki kwa hoja za kitoto kama hizi. Sio vibaya kuutafutia soko mtandao wenu lakini musitumie uislamu katika kujitafutia UMAARUFU!
 
Pole sana sheikh Mungu awe pamoja nawe. Inshallah atakupa wepesi na uweze kupona haraka.
 
Ni mapema kuanza kunyosheana vidole. Kama polisi watafanya kama walivyofanya kwa Barlow basi wawakamate wahusika ili tujue ni akina nani? Hadi hapo huwezi kuanza kushutumu waislam au wakristo. Mchezo huu usipotafutiwa dawa tunaelekea kubaya tena haraka.
 
pole sana kwake mungu atampa nguvu.
na akipona afunguke kama anajua chochote kuhusu hilo.
 
haya si matendo ya nchi inayoitwa ya amani maana amani yenyewe inaanza kuwa ya mashaka.
mungu aisaidie tz yetu.
 
Back
Top Bottom