Picha rasmi ya rais na bango la baraza la mawaziri

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
764
Kuna picha rasmi ya Mh Rais imetoka kwa ambaye anahitaji kwa ajili ya kuweka ukutani. Sambamba na hiyo liko pia bango jipya la baraza lote la mawaziri ambalo liko na kalenda. Vyote vimeshambazwa mikoani hivyo kama unahitajiili fuatilia utavipata.
 
Hivi nchi hii ina baraza la mawaziri. au ina waziri mmoja au wawili tu?
 
Picha rasimi ya Diwani (JK), ya kazi gani kwangu mkuu?
Jamaa amepwaya utendaji wake siku hizi kama Diwani wa kata halafu anachakaa ghafla, na bado!
 
Kwani TZ kuna Rais????????????

Iko figure ya rais tu lakini ndani yake kuna uwazi mtupu. Amepoteza haiba kabisa. Ni product mbaya kabisa tumewahi kuproduce Tanzania. Lakini tusilaumu sana maana Avumaye baharini ni papa ........... 2015 anakuja Lowasa pia mpaka 2025. Baada ya hapo January Makamba hadi 2035 kama haitoshi baada ya hapo Ridhiwan Kikwete hadi 2045. Miaka 35 hiyo, tutakuwa na umri gani?

Baada ya Ridhiwan Mdogo wake Hussein Mwinyi atachukua hadi 2055. Kutakuwa na attempt ya mapinduzi mwaka 2050 lakini yatazimwa kwa umwagaji damu mkubwa.
 
Sisi sio Somalia bwana. Tunaye Rais na Baraza lake la Mawaziri. Kuukataa ukweli huu ni upofu ulioje! Hafai, hawezi, haumtaki, haukumchagua, hilo suala jingine. Tutaziona picha hizi kwenye ofisi zetu za UMMA. Kuinunua niipeleke nyumbani sio rahisi maana kule mimi ndiye "rais" ati! Iko picha yangu kule.
 

Yaani picha ya JK kwangu mmmh ngumu mno. Alafu mbona unamdalalia, au wewe ndio mtengenezaji unataka kurudisha?

Kweli chema chajiuza kibaya chajitembeza, mbona ya Wabunge wa CDM na uongozi wao haikuppigiwa debe lakini inaweza kuvunja rekodi ya manunuzi ya awamu zote mbili za raisi wenu
 
Back
Top Bottom