Picha: Kundi la wananchi wafanya vurugu na uharibifu mtaa wa Isengo kata ya Iziwa. Mbeya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
TUESDAY, JANUARY 29, 2013

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA ATHUMANI DIWANI ENEO LA TUKIO

WANAKIJIJI ISENGO IZIWA WAKIWASIKILIZA WANAUSALAMA HUKU WAKIWA NA SIRAHA ZAO ZA JADI

CHANZO CHA MAJI IZIWA

MAMA WA KISAFWA AKIWA AMEFICHA PANGA

SIRAHA ZA JADI ZILIZOKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA

MNAMO TAREHE 28.01.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS MAAFISA WA HIFADHI YA MALIASILI NA UTALII WAKIONGOZWA NA MENEJA WA HIFADHI HIYO KASMIR S/O NGOWI NA AFISA MISITU WA JIJI LYOWA S/O WAYANGA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA WALIFIKA KATIKA MTAA WA ISENGO KATA YA IZIWA KWA AJILI YA KUENDELEA NA OPERESHENI YAO YA KUWAONDOA WATU WALIOVAMIA NA KULIMA NDANI YA HIFADHI YA SAFU YA MLIMA MBEYA [MBEYA RANGE FOREST RESERVE] ENEO AMBALO NI CHANZO CHA MAJI NA VIUMBE HAI ZOEZI LILILOANZA TANGU TAREHE 28.12.2012.

HATA HIVYO KABLA ZOEZI HILO KUANZA KUNDI KUBWA LA WANANCHI WA ENEO HILO WAPATAO 400 WAKIWA NA SILAHA ZA JADI WALIFIKA ENEO HILO WAKIWA WAMEJIANDAA KUFANYA VURUGU WAKISHINIKIZA KUTOFANYIKA KWA ZOEZI HILO.

KATIKA VURUGU NDOGO ILIYOTOKEA YOHANA S/O MDEWA,MIAKA 54,MSAFWA,MWANACHAMA WA ASASI YA KIRAIA YA KUTUNZA MAZINGIRA MKAZI WA KIJIJI CHA IHOMBE , ALIJERUHIWA KWA KUKATWA PANGA KICHWANI , WAKIDAI NDIYE MSALITI ALIYEWALETA WATU HAO ,HIVYO POLISI WALIMUOKOA NA KUMHIFADHI KATIKA OFISI YA MTENDAJI KATA.

PIA KATIKA VURUGU HIZO KULITOKEA UHARIBIFU KATIKA GARI STJ 1830 MALI YA WAKALA WA HIFADHI YA MISITU NYANDA ZA JUU KUSINI KWA KUPASUKA WIND SCREEN YA MBELE NA SIGHT MIRROR YA KUSHOTO NA MAGARI MENGINE YA IDARA HIYO STJ 1821 NA STJ 1832 KURUSHIWA MAWE PIA KUBOMOA MADARAJA MAWILI YALIYOPO KIJIJINI HAPO. KUFUATIA HALI HIYO KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA MKOA WA MBEYA WALIFIKA ENEO HILO HATA HIVYO WANANCHI WALITAWANYIKA KWA KUKIMBIA.

POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA ENEO HILO WALITOA WITO KWA WANANCHI KUTOJICHUKULIA SHERIA MKONONI AMBAPO WALIKIRI NA KUDAI HAWAKUELEZWA JUU YA ZOEZI HILO NA WAMEAHIDI KUJENGA WAO WENYEWE MADARAJA WALIYOKUWA WAMEBOMOA.

UONGOZI WA SERIKALI YA WILAYA YA MBEYA CHINI YA MKUU WA WILAYA DR NORMAN SIGALA NA MSTAHIKI MEYA WA JIJI ATHANAS KAPUNGA NA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIWEMO MHE DIWANI NA MTENDAJI KATA YA IZIWA KATIKA KIKAO KILICHOFANYIKA BAADAE WAMEKUBALIANA KUWA WATU WOTE WALIOVAMIA ENEO HILO WAHAKIKISHE WAMEHAMA KABLA YA MWEZI AGOST – 2013. KWA SASA HALI IMEREJEA KUWA SHWARI KIJIJINI HAPO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAHESHIMU NA KUTII SHERIA PASIPO KUSHURUTISHWA.

PIA ANAZIDI KUSISITIZA KUWA MAZUNGUMZO NDIO NJIA MUHIMU NA SAHIHI YA KUWASILISHA MALALAMIKO/KERO BADALA YA FUJO NA VURUGU ZISIZOKUWA NA TIJA KWANI ZINAWEZA KULETA MADHARA NA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO YAO.

KAMANDA AMEAHIDI KUWA WALIOVUNJA SHERIA KWA KUMJERUHI YOHANA S/O MDEWA NA KUFANYA UHARIBIFU WA MADARAJA WATAFUATILIWA ILI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Tulimchukia NYERERE sababu kila mtu alinyimwa MOJA ya UHURU kwenye jamii yake WENGINE wakakubali WENGINE hakukubali... lakini tulikuwa na amani asilimia 90%...

Sasa; Tunataka kuwapa kila MTU UHURU wake... HAIWEZEKANI ndio Maana inaitwa DEMOKRASIA ya KATIBA; NENDA MAREKANI UONE katiba yao ni ya 1870 lakini hadi leo nenda barabarani mkiwa kumi muanze kuitukana serikali MUONE MTAISHIA wapi; hata hamtapata MAHAKIMU wa kuwatetea...

Angalia sasa hivi kila mtu anadai chake kwa nguvu... hii ni sababu ya MADARAJA MATATU nini???
 
Kwa hili sina budi nikupongeze. Umeongea point pamoja na kwamba wakati mwingine huwa unaongea kama hufikilii vile.

Mimi nafikili nchi iko kwenye mpitio wa jamii kuelekea kufahamu mipaka ya uhuru wao kidemokrasia. Na kwa kufanya hivyo, tutaona vituko vingi sana.Watanzinia walio wengi kwa sasa kama ndiyo wanafumbua macho na kukuta vitu vingi mezani vinavutia na wanashindwa kuchagua kipi kizuri na kipi kibaya.

Somo la uraia lisilokuwa distorted ni muhimu sana kwa sasa Tanzania otherwise, nguzo zote za ulinzi nchini zitatikiswa sana.

Cha kushangaza, eti watu wanaandamana kwenda polisi kupata maelezo. Hii kwenye nchi waasisi wa demokrasia huwezi fanya utaishia mikononi mwa polisi halaka sana. Kesho yake unapelekwa mahakamani, unasomewa shitaka na kusubiri huruma ya hakimu.
Tutafika tu.
 
Sumu ya Mtwara sasa inaenea kila mahali.Hakika nguvu ya umma si ya kuchezea
 
Tulimchukia NYERERE sababu kila mtu alinyimwa MOJA ya UHURU kwenye jamii yake WENGINE wakakubali WENGINE hakukubali... lakini tulikuwa na amani asilimia 90%...

Sasa; Tunataka kuwapa kila MTU UHURU wake... HAIWEZEKANI ndio Maana inaitwa DEMOKRASIA ya KATIBA; NENDA MAREKANI UONE katiba yao ni ya 1870 lakini hadi leo nenda barabarani mkiwa kumi muanze kuitukana serikali MUONE MTAISHIA wapi; hata hamtapata MAHAKIMU wa kuwatetea...

Angalia sasa hivi kila mtu anadai chake kwa nguvu... hii ni sababu ya MADARAJA MATATU nini???

usiwe mtumwa wa mawazo wa nchi za kigeni huo ni ujinga unajilinganisha na marekani nchi iliyoendelea na wewe ukiwa bibi, kaka, mama, dada,baba wanatumia kibatari na wewe ukiwa naumeme wa mawazo huku njaa kama kawaida watu wanakufa kila kona, elimu ndio usiseme form 4 nikama darasa la 7 acha ujinga kabisa mkuu
 
Kwa hili sina budi nikupongeze. Umeongea point pamoja na kwamba wakati mwingine huwa unaongea kama hufikilii vile.

Mimi nafikili nchi iko kwenye mpitio wa jamii kuelekea kufahamu mipaka ya uhuru wao kidemokrasia. Na kwa kufanya hivyo, tutaona vituko vingi sana.Watanzinia walio wengi kwa sasa kama ndiyo wanafumbua macho na kukuta vitu vingi mezani vinavutia na wanashindwa kuchagua kipi kizuri na kipi kibaya.

Somo la uraia lisilokuwa distorted ni muhimu sana kwa sasa Tanzania otherwise, nguzo zote za ulinzi nchini zitatikiswa sana.

Cha kushangaza, eti watu wanaandamana kwenda polisi kupata maelezo. Hii kwenye nchi waasisi wa demokrasia huwezi fanya utaishia mikononi mwa polisi halaka sana. Kesho yake unapelekwa mahakamani, unasomewa shitaka na kusubiri huruma ya hakimu.
Tutafika tu.

Itakuwa KOSA KUBWA sana tena la MAUTI kuwaachia WANANCHI kuchagua UHURU wautakao kama ni HIVYO basi kwanini kuwa na POLISI na USALAMA wa TAIFA? hata siku moja Mwananchi yoyote hatakuwa na FURAHA kwa UHURU alionao NDIO MAANA kuna KATIBA yenye PINGAMIZI ya kumsitiri huyo MWANANCHI sasa kama wewe unavyosema Unawawekea MEZANI cha kuchagua kipi ni BORA AAAH kila mtu hatafaidika...

Angalia MFANO MZURI ni Zanzibar na MUUNGANO wa MKATABA; kila MMOJA wao Anauongelea lakini Hawajui vipengele vyake Watavitoa Baadaye... LINI BAADAYE? kwahiyo IKUBALIKE kwenye KATIBA kitu kisichona kipengele na uweleweke wowote wa nini ni MUUNGANO wa MKATABA??? na imeuzwa kwa karibia asilimia 80 ya wananchi wa Zanzibar lakini hawajui ukoje... UMEONA hao??? kila kitu kiko MEZANI Mmmm

Angalia KATIBA ya KENYA Group of Lawyers na Watu Maarufu waliifanyia kazi sio kuchukua MAONI ya Wananchi wooote ANgalia ilivyo SAFI inaanza kazi MWAKA HUU it is fair and square...

*** Unafanya kosa kubwa kweli ku-judge a human being, it is a sin... a human being brain is sacred... never under estimate a HUMAN NATURE...
 
usiwe mtumwa wa mawazo wa nchi za kigeni huo ni ujinga unajilinganisha na marekani nchi iliyoendelea na wewe ukiwa bibi, kaka, mama, dada,baba wanatumia kibatari na wewe ukiwa naumeme wa mawazo huku njaa kama kawaida watu wanakufa kila kona, elimu ndio usiseme form 4 nikama darasa la 7 acha ujinga kabisa mkuu

Kwasababu sisi AFRICA KATIBA zetu zina egemea upande fulani --- MFANO ATI MFANO wa Zanzibar kutaka MUUNGANO wa MKATABA lakini woote waliopendekeza hawajui vipengele VYAKE na MIFANO yake... na TULIVYO wajinga tutaweka kwenye katiba ili kunyamazisha Malalamiko... HAKUNA anayejua UKOJE na UTAKUAJE na UTAISHIJE... ndio sisi Waafrika na asilimia 80 ya Wazanzibari wameshauziwa huo MKATABA na hawaujui ukoje... sasa MIFANO mizuri toka bara letu niitoe wapi? MALI? LIBYA? RWANDA? UGANDA?
 
Asante kwa taarifa mkuu nngu007 ,nimepita kitambo kipande hiyo nikitokea juu mlimani Loleza.
 
Last edited by a moderator:
MKUU nngu007 umenena tuache ushabiki, unajua uhuru ambao hauna mipaka matokeo yake ni kama haya tunayoyashuhudia na ambapo amani ikitoweka tu ghalama ya kuja kuirudisha ni ghali sana kuliko kuilinda hii iliopo ivo ushabiki tuuweke pembeni
 
Back
Top Bottom