Picha: Kuchapa Kazi ni wakati wowote na mahali popote... RAIS KIKWETE SAFARINI DODOMA

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
THURSDAY, MARCH 20, 2014

Kweli Urais hauna ubia wala muda ama sehemu ya kuchapa kazi. Wakati wowote na mahali popote ni sehemu ya kazi, kama inavyoonekana hapa ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametulia ndani ya ndege akisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma huku akiifanyia kazi hotuba yake ambayo ataitoa katika Kikao cha Bunge Maalum la Katiba, Ijumaa, Machi 21, 2014.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amealikwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa Kanuni 7(1)g na Kanuni 75(1) la ya Kanuni za Bunge Maalum.

PICHA NA IKULU.

: MICHUZI
 
JK kama yupo kwenye Air force one ya US. Ila kama hizo nondo alizoshika ndiyo za kuisambaratisha ripoti/matakwa ya wananchi iliyowasilishwa na Jaji Warioba atakuwa anatumia vibaya kodi zetu.
 
Ole wake alete dharau zake kwa wananchi tutazomea mbayaaa,tena sana hatishwi mtu hapa
 
Juu ya meza mbona kuna magazeti ya katuni tu?

Anatafuta kick za kitoto angalia Uhuru Kenyatta anachokifanya, sifa na kazi siyo picha za kutaka kick za kitoto...
 
JK kama yupo kwenye Air force one ya US. Ila kama hizo nondo alizoshika ndiyo za kuisambaratisha ripoti/matakwa ya wananchi iliyowasilishwa na Jaji Warioba atakuwa anatumia vibaya kodi zetu.
Matakwa gani ya wananchi?.

Kama rasimu ya pili ya katiba ndiyo "alpha na omega" ya matakwa ya wananchi, kuna haja gani tena ya kuwauliza wananchi hao hao kama matakwa yao wanayakubali au hawayakubali. Hii ina maana kuwa, hakuna uhakika kama haya ndiyo matakwa yao na ndiyo maana wataulizwa tena kusema ndiyo au hapana katika kura ya maoni.

Hoja yako haisimami katika mantiki na ukweli.
 
Babu akiona picha hii roho inamuuma sana! Anatamani angekuwa yeye na mwenza wake Msumbushi.
 
Makamanda mbona ujumbe wangu nilio changia siuoni?
Kuna mapinduzi gani tena?
Jf vipi?
Ok! "sawa mungu ibariki chadema"
 
Matakwa gani ya wananchi?.

Kama rasimu ya pili ya katiba ndiyo "alpha na omega" ya matakwa ya wananchi, kuna haja gani tena ya kuwauliza wananchi hao hao kama matakwa yao wanayakubali au hawayakubali. Hii ina maana kuwa, hakuna uhakika kama haya ndiyo matakwa yao na ndiyo maana wataulizwa tena kusema ndiyo au hapana katika kura ya maoni.

Hoja yako haisimami katika mantiki na ukweli.

kazi YAKE NI KUFUNGUA BUNGE MAALUM TU , AKILETA TAARABU ZA MSOGA ATAADHIRIKA VIBAYA SANA !
 
unataka kusema wamehujumu andishi lako ? Hii sasa hatari !

huwezi amini kamanda nilikuwa mtu wa tatu kuchangia baada ya kamanda lyimo, ukaingia vizuri tu lakini cha kushangaza baada ya muda mfupi sijauona hadi sasa?
Ok! Siyo mbaya tutapambana humu humu!
Kwa kunebea emu efu nitaenda wakinikwaza hadi nukta ya mwisho?
Adui haogopwi ila ni kukutana naye macho kwa macho!
"nakupenda sana chadema"
 
Juu ya meza mbona kuna magazeti ya katuni tu?

Anatafuta kick za kitoto angalia Uhuru Kenyatta anachokifanya, sifa na kazi siyo picha za kutaka kick za kitoto...
Mijitu mingine bana amia Kenya kama unampenda Kenyatta.
 
huwezi amini kamanda nilikuwa mtu wa tatu kuchangia baada ya kamanda lyimo, ukaingia vizuri tu lakini cha kushangaza baada ya muda mfupi sijauona hadi sasa?
Ok! Siyo mbaya tutapambana humu humu!
Kwa kunebea emu efu nitaenda wakinikwaza hadi nukta ya mwisho?
Adui haogopwi ila ni kukutana naye macho kwa macho!
"nakupenda sana chadema"

safi sana , umeandika kikamanda sana !
 
Back
Top Bottom