Peter Zakaria asomewa mashtaka mawili ya kujaribu kuua, anyimwa dhamana

Nenda mahakamani kama una ushahidi kweli zacharia ni jambazi...pia nimejaribu kupitia maoni yako mbali mbali humu jf unaonekana wa lumumba hata penye ukweli kuhusu srkl unapindisha ....
Bora umewahi kulijua hilo kwani ungepoteza muda kujibizana naye
 
mkuu endelea kutuhabarisha hili tukio, tunataka kujua mengi kwa faida ya Watanzania waliochoka.
 
nasubiri mahakamani wkati wa kedsi tutawajua zaidi,
kama nawaona vile wakijitetea
hutawaona mahakamani, ni aibu sana kwa kiongozi kutamka wale ni usalama wa Taifa, sijui kwa nini bado yupo madarakani, usalama wa taifa gani huyo anayejulikana na kila mtu, kuna usalama hapo tena.
 
Acha unafiki. Zacharia alikuwa na maadui wengi. Ni jambazi.
Wafrika katika ubora wao,hivi serikali inampa jambazi silaha?na kama ni jambazi siyo kazi ya usalama wa taifa kumkamata ni kazi ya polisi,huo ni ukweli,kamati ya ulinzi ya mkoa ndio wanatoa kibali cha silaha na katika kamati hizo usalama wako ndani,ukiwa na tuhuma za uhalifu haulewi kibali.
 
Mfanyabiashara maarufu na Mmiliki ya Mabasi ya Zakaria, Peter Zakaria amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka mawili ya kujaribu kuua, amenyimwa dhamana hadi Julai 10 Mahakama itakapotoa uamuzi mdogo kuhusu dhamana.

---
Hayo yamebainishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Musoma hii leo Julai 05, 2018 na kumnyima dhamana mtuhumiwa huyo kwa kile kilichoelezwa kwamba wale waliojeruhiwa hali zao kiafya kuwa ni mbaya katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo wanapatiwa matibabu.

Mbali na hilo, Mahakama imesema sababu nyingine za mtuhumiwa huyo kutopewa hati ya dhamana ni kutaka kulinda usalama wake lakini Mawakili wa upande wa utetezi wakapinga hoja hiyo kwamba hakuna ukweli wowote kama mteja wao akiachiwa ataweza kudhurika.

Vile vile, Mawakili wa upande wa utetezi wamesema hakuna hati yoyote iliyowasilishwa Mahakamani ya kuonesha kwamba hao majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Muhimbili na kama kweli wametibiwa.

Baada ya mvutano huo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu mkazi Musoma, Rahim Mushi amesema Mahakama ipewe muda mpaka Julai 10 ili waweze kupitia uamuzi mdogo kuhusiana na suala la dhamana kama mtuhumiwa anastahili au laa.

Peter Zacharia alikamatwa na Jeshi la Polisi mnamo Juni 29, 2018 akidaiwa kuwajeruhi kwa risasi watu wanaodaiwa kuwa ni maofisa Usalama wa Taifa, tukio lililotokea katika kituo cha mafuta kinachomilikiwa na mfanyabiashara huyo.

Pia soma
>Kesi ya Zakaria: Polisi washindwa kumfikisha mahakamani. Wadai jalada halijakamilika. Ndugu wakesha mahakamani

>Tarime, Mara: Mmiliki wa mabasi ya Zacharia awapiga risasi maafisa wa Usalama wa Taifa, ashikiliwa na Polisi

>Mmiliki wa mabasi ya Zakaria amenidhulumu mali yangu na kutishia kuniua

Kinacho furahisha ni kwamba hatimaye wasiojulikana wamejulikana
 
Back
Top Bottom