Peter Msigwa (CHADEMA) ni mbunge aliyelisemea Jimbo la Iringa Mjini

Amefanyaje yule madam?
Duh.jpg
 
View attachment 2188789

Wakati Chadema ikiwaletea Mbunge wa Taifa , ambaye pamoja na kujenga hoja nzito mno bungeni kwa kutetea maslahi yenu na ya nchi kwa ujumla , hakuwahi kuwadhalilisha , Kwa kipindi chote Mchungaji Msigwa alipokuwa bungeni , amekuwa heshima kubwa kwa Mkoa mzima wa Iringa , ndiye Mbunge aliyenukuliwa mara nyingi zaidi akitetea Mkoa wa Iringa , Alimbana Dr Mpango bungeni alipokuwa Waziri wa fedha kuhusu kuporomoka kwa uchumi wa Tanzania hadi ikawa Aibu ! huku Wabunge wengine wa Mkoa wa Iringa wakiishia kuhonga wananchi viberiti na Ulanzi , ambapo Deo Sanga wa Makambako akitia aibu zaidi kwa KUKATA VIUNO Katikati ya Ukumbi wa Bunge ili kumshangilia Dr Magufuli (Astaghafillullah) , Kimsingi Dr Mpango alikosa majibu ya Maswali ya Mh Peter Msigwa hadi alipopata corona na kusamehewa .

Mchungaji Msigwa na Baraza la Madiwani wa Chadema ndio wamewezesha Stendi mpya Iringa , ndio waliowezesha mambo yote mazuri mnayoyaona hapo kwenu , Iringa ilivunja rekodi ya Usafi kwa sababu ya mipango kabambe ya Msigwa na Mstahiki Kimbe .

Leo Iringa inapata Mbunge anayedhani wauza nguzo hela zao ni za kununulia wanawake kweli ! heshima ya Iringa nani atailinda ? yule kijana mwingine wa kufahamu Mikuyati na vumbi la Kongo alipoondoka bungeni tukajua haya mambo yataisha , kumbe ndio kwanza yanaibuka Upya !

Nakulilia Iringa .

Ndugu mleta Mada, Asante kwa maoni yako, .

Watu wa Iringa hatuishi kwa hisani za Wanasiasa.

hata akiwa mwanachama wa Jahazi asilia tukimuelewa tunampa tu nafasi,
Msigwa sio mbunge wa Kwanza wa upinzani Iringa na hatakuwa wa Mwisho.

Kusema kuwa iringa imepata stand sijui usafi kwa sababu ya mtu fulani ni kutufedhehesha watu wa Iringa.
Suala la usafi ni tabia za watu na kama kwenu huko mko wachafu msilaumu wanasiasa, Bali tabia zenu za uchafu.
Kwa ufupi serikali hii ya ccm pamoja na wanasiasa wengine wakiwemo upinzani ndio kwa sehemu kubwa wamekwamisha mkoa wa iringa kuwa na maendeleo tunayostahili.
Nevertheless, Iringa sio maskini.
 
Back
Top Bottom