Pep Guardiola ndio Kocha Bora kwa sasa Duniani

Huyo ni manager wa Billion Pound Squad, kuchukua kombe na Leicester kama Ranieri, Blackburn kama Dalgish, Valencia kama Benitez, Arbedeen kama Ferguson, Porto kama Mourinho hawezi na hawezi hata kujaribu.
Mpira wa zama hizi ni uwekezaji mzee hiyo mifano ya Ferguson na Arbedeen ni ya zamani sana mpira umebadilika hizi zama bila uwekezaji na kutengeneza structure nzuri ya timu na kuweka mpunga huwezi kubeba mataji. Hata huyo Fergie mnayemsifia angekuwepo zama hizi bila uwekezaji angelambishwa mchanga.

Ancelloti mnayemsifia kwamba ni bora (kabeba mataji kila ligi kubwa) si alikuwepo Everton mbona hakuifanya imalize top four tu (achilia mbali kuipa ubingwa). Huyo Mourinho si alikuwepo United timu yenye hela mbona hakuipa ubingwa.

Kubalini tu Pep ana mbinu bora za kufundisha kiasi kaweka high standard ambayo ni ngumu kushindana naye na ukachukua kikombe mbele yake.

Hiyo hoja ya kusema Pep ni billion Pound coach au hawezi kufundisha timu ndogo ni dhaifu ni sawa na kusema kama Ronaldo au Messi ili tuwaone bora basi waende Crystal Palace na waipe ubingwa.
 
Umewahi kupitia budget ya PSG mbona hawana lolote la maana kwenye mashindano ya kimataifa ?

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Kwani huyo Pep toka alipotoka Barca amewahi kuchukua UCL? Ameenda kwa Bavarians kakaa misimu mingapi bila bila, kaenda Man City huu ni msimu wa ngapi ndio anaunusa ubingwa wa UCL!

Sikatai kuwa ni kocha bora sana, huenda the best, lakini angalieni bajeti anayopewa kila anapoenda.
 
Ancelloti mnayemsifia kwamba ni bora (kabeba mataji kila ligi kubwa) si alikuwepo Everton mbona hakuifanya imalize top four tu (achilia mbali kuipa ubingwa). Huyo Mourinho si alikuwepo United timu yenye hela mbona hakuipa ubingwa.

Kubalini tu Pep ana mbinu bora za kufundisha kiasi kaweka high standard ambayo ni ngumu kushindana naye na ukachukua kikombe mbele yake.

Hiyo hoja ya kusema Pep ni billion Pound coach au hawezi kufundisha timu ndogo ni dhaifu ni sawa na kusema kama Ronaldo au Messi ili tuwaone bora basi waende Crystal Palace na waipe ubingwa.

kuipeleka Everton top 4 ndani ya misimu msimu mmoja na nusu unaichukulia ni ishu nyepesi? Huyo Pep anaweza fanya hivyo?
 
Kwani huyo Pep toka alipotoka Barca amewahi kuchukua UCL? Ameenda kwa Bavarians kakaa misimu mingapi bila bila, kaenda Man City huu ni msimu wa ngapi ndio anaunusa ubingwa wa UCL!

Sikatai kuwa ni kocha bora sana, huenda the best, lakini angalieni bajeti anayopewa kila anapoenda.
Zama hizi mpira ni uwekezaji bila uwekezaji hutoboi. Ligi zote kubwa duniani timu zinazospend ndizo zinadominate. EPL City, La Liga Barca/Madrid, Bundesliga Bayern, Ligue1 PSG. HIzi hoja mnazotumia kumponda Pep ni dhaifu.
 
Zama hizi mpira nj uwekezaji bila uwekezaji hutoboi. Ligi zote kubwa duniani timu zinazospend ndizo zinadominate. EPL City, La Liga Barca/Madrid, Bundesliga Bayern, Ligue1 PSG. HIzi hoja mnazotumia kumponda Pep ni dhaifu.
Sijamponda, nimeongea uhalisia mkuu. Ni kweli ligi zote kuna giants ila pamoja na uwezo wake mkubwa, Pep budget yake pia sio ndogo, ili achukue UCL pale city, ametumia $$$ nyingi mno.
 
Haujajibu swali ndugu.
Pep hawezi kama walivyo Makocha wengine pia. Mpira ni uwekezaji huwezi kubeba ubingwa kwa kushindana na timu zenye budget kubwa ndio maana kila siku timu zenye mfuko uliotuna ndizo zinadominate.

Kwa maana hio kama unamuita Pep si kocha bora sababu ni billion pound coach na anafundisha timu kubwa tu nikakuuliza Ancelloti/Mourinho/Fergie ukawapa Crystal palace wanaweza ipa ubingwa?
 
Ancelloti/Mourinho/Fergie wakipewa Southampton kwa bajeti kiduchu kama hii walionayo na wakapewa muda wanaweza beba kikombe cha EPL?
Mourinho juzi kasema Roma imeingia fainali kwa very limited budget, alikuwa analinganisha na Pep, Fergie alikuwa na budget ndogo sana miaka yake, almost kama Wenger tu, unlike Man U ya sasa, wanaspend sana bila mafanikio uwanjani.
 
Budget ya clubs anazofundisha huwa unaipitia? Ji kweli ni kocha bora sana, ila nae anakuwa na budget kubwa sana. Hata jana Mourinho alisema, una bench lenye 200m, wakati huo upo na quality ya hali ya juu ndani ya uwanja. Huwezi kulinganisha na hawa wanaopewa limited budget.
Hawezi kukuelewa asilani!

Kwanza, hakuna timu aliyowahi kwenda Pep ikiwa haieleweki, anakuta timu imesukwa kwa mud mrefu, yeye anaingia kwenye timu iliyoiva, iliyokuza watu kwa muda mrefu kisha yenye mpunga usiomithilika.

Barca, nikumbushe msimu upi ilikuwa mbovu kabla ya Pep?

Bayern, ameikuta ikiwa moto na akaiacha hoi!

Akakaa mwaka nje ya game akitathmini ipi nyingine ina-team work baada ya watu kuzoeana kwa muda mrefu kisha PESA ya usajili kedekede, huyoooo City.

Jamaa kamtaja Fergie, achilia mbali Fergie, huyo Wenger tu, Pep hawezi vaa viatu vyake!

Mourhinho kabeba UEFA akiwa na kikosi cheap haswa! Analijua hilo?

Pep, apewe Newcastle saa hii tuone, si pesa ipo pale saa hii!
 
Pep hawezi kama walivyo Makocha wengine pia. Mpira ni uwekezaji huwezi kubeba ubingwa kwa kushindana na timu zenye budget kubwa ndio maana kila siku timu zenye mfuko uliotuna ndizo zinadominate.

Kwa maana hio kama unamuita Pep si kocha bora sababu ni billion pound coach na anafundisha timu kubwa tu nikakuuliza Ancelloti/Mourinho/Fergie ukawapa Crystal palace wanaweza ipa ubingwa?
Fergie aliichukua United ikiwaje mzee?

Mourhinho anabeba UEFA akiwa na Porto sio? Uliionaje Porto ile kwa wale manguli wote barani Ulaya enzi zile?
 
Ancelloti/Mourinho/Fergie wakipewa Southampton kwa bajeti kiduchu kama hii walionayo na wakapewa muda wanaweza beba kikombe cha EPL?
Umesahau Mourinho alibeba ndoo ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE akiwa na timu gani iliyo na hadhi ya Wachezaji wa kawaida sana kimasilahi lakini aliishangaza dunia ndipo akaletwa Chelsea FC na Tajiri Abrahamovich?

Pep kipara bila pesa hana ubora wowote, fatilia mafanikio yake alitembelea klabu zipi haswa na maranyingi anazikutaga ziko on .

Kwangu Ancelloti, Klopp, Mourinho na Conte ni Makocha bora mara 10 zaidi ya Kipara.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Hawezi kukuelewa asilani!

Kwanza, hakuna timu aliyowahi kwenda Pep ikiwa haieleweki, anakuta timu imesukwa kwa mud mrefu, yeye anaingia kwenye timu iliyoiva, iliyokuza watu kwa muda mrefu kisha yenye mpunga usiomithilika.

Barca, nikumbushe msimu upi ilikuwa mbovu kabla ya Pep?

Bayern, ameikuta ikiwa moto na akaiacha hoi!

Akakaa mwaka nje ya game akitathmini ipi nyingine ina-team work baada ya watu kuzoeana kwa muda mrefu kisha PESA ya usajili kedekede, huyoooo City.

Jamaa kamtaja Fergie, achilia mbali Fergie, huyo Wenger tu, Pep hawezi vaa viatu vyake!

Mourhinho kabeba UEFA akiwa na kikosi cheap haswa! Analijua hilo?

Pep, apewe Newcastle saa hii tuone, si pesa ipo pale saa hii!
Kwani kati ya hizo timu ulizataja na pep ,nani hua anaomba huduma kwamwezake
 
Back
Top Bottom