Pendekezo thabiti la Jinsi ya Kukomesha mauaji ya Albino

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,483
40,011
Albinooo.jpg
The most recent attack took place on October 21, 2011 in Mbizi Village, Kahama District, Shinyanga Region of Tanzania. A 15-year-old girl with albinism by the name of Kulwa was attacked just after midnight at her home by three masked men. They hacked off her arm above the elbow and the horrified and helpless parents saw them fleeing with the arm wrapped in one of the assailant's coat. Kulwa was treated at Kahama District Hospital and was terrified to return home

Na. M. M. Mwanakijiji

TUNAWEZA kukaa chini na kukubali mapendekezo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juu ya vita dhidi ya mauaji ya maalbino au kuyakataa; tunaweza kukubali kuwa waganga wote wa kienyeji wafutiwe leseni zao kwa kudhaniwa kuhusika na uhalifu au kukataa; tunaweza tukakubali waziri mkuu aseme maneno ya kichochezi na yenye kuhatarisha amani nchini au kumpinga. Yote yamo ndani ya uamuzi wetu na ndani ya uwezo wetu.

Natamani kuandika kwa kirefu juu ya kauli zinazodaiwa kutolewa na Waziri Mkuu juu ya wale wanaoshukiwa kufanya mauaji ya maalbino kama zilivyonukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari.

Sitafanya hivyo hapa lakini nataka nipinge tu kuwa kuhalalisha mauaji ya watu wengine kwa vile wanatuhumiwa kuua watu wengine, hakutatui tatizo la mauaji bali kunalithibitisha.

Hata hivyo nimeandika mawazo yangu kwa kina kwenye kijarida ninachotoka mtandaoni cha "Cheche za Fikra" na kuelezea kwa kina kwanini naamini kauli hizo za waziri mkuu ni za makosa, za hatari na ni lazima aidha zifutwe, zikanushwe au ziwekwe katika lugha ambayo inakubalika kisheria.

Haziwezi kupuuzwa au kuachwa zisimame kama zilivyo. Niandikie kupata nakala ya kijarida hicho kwa barua pepe bure.

Hata hivyo hapa nataka kusema tu kuwa kuja na sera ya ‘jino kwa jino' na kufuta leseni za waganga wa kienyeji wote nchini hakuwezi kamwe kuondoa mauaji ya maalbino, kwani msingi wake umekosewa tangu awali.

Watawala wetu wanataka watu waamini kuwa kinachochea mauaji ya maalbino ni imani za kishirikina.

Wanataka watu waamini kuwa ni ushirikina unaosababisha ndugu zetu maalbino kuuawa.

Nimeshaandika juu ya mauaji ya maalbino kwa kina huko nyuma, hata hivyo naamini serikali na vyombo vya usalama vinalikabili suala hili kwa makosa, kwani vinaoongozwa na tatizo ambalo si kichocheo cha mauaji haya.

Sisemi kwamba imani za kishirikina hazitumiki katika mauaji haya bali kuwa kiini hasa na kichocheo hasa siyo wacheza ndumba na wapiga ramli.

Kuweka mkazo katika hayo ni kujaribu kutwanga maji kinuni. Hakuhusiani na tatizo lililopo. Mpaka tutambue chanzo cha mauaji haya ndipo kwa hakika tutaweza kupambana nayo na ninaamini mapendekezoo nitakayoyatoa (kinyume na yaliyotolewa na Waziri Mkuu) yanaweza kabisa kukabiliana na tatizo hili.

Nitawakumbusha kitu hapa; ni jinsi gani aliyekuwa mtawala wa Iraq aliweza kusalitiwa maficho yake?

Je, watoto wake Uday na Qusay walisalitiwa kwa misingi gani? Je, ni kitu gani kinaweza kumfanya mtu amsaliti ndugu yake wa damu? Ndugu zangu jibu ni fedha!

Mauaji ya maalbino yameanza na kukolezwa kwa sababu ya tamaa za fedha (utajiri wa haraka haraka). Sasa hili limewahi kusemwa huko nyuma ingawa limesemwa katika maudhui ya matokeo ya imani hizi za kishirikina (kwamba mtu anaenda kwa mganga ili kupata utajiri wa haraka haraka).

Naamini kilichokosewa kwa muda mrefu katika miaka hii miwili ni kuingiza fedha katika vita hii. Niliwahi kuandika huko nyuma haja ya kuanzisha fungu maalumu la kuzawadia watakaowasaliti wenye kutafuta viungo vya maalbino.

Hadi hivi sasa kinachopimwa na wauaji hawa ni kipi kina faida zaidi kuliko kipi kinatisha zaidi.

Kwa wauaji hawa wazo kuwa wanaweza kupata utajiri wa haraka haraka wakifanya mauaji haya inapita kwa kiasi kikubwa kulinganisha na adhabu ya wao kukamatwa au tishio la wao wenyewe kuuawa. (rudia tena fungu hili).

Hivyo njia ya kwanza na kubwa zaidi ya kupambana na mauaji haya ni kuleta fedha kwenye mapambano haya. Je, serikali inaweza kutafuta kiasi cha shilingi milioni 200 au zaidi kuzawadia watakaofichua wanaotafuta viungo vya maalbino? (angalia nimesema wanaotafuta, sikusema wanaoua).

Wale wanaotafuta viungo vya maalbino ndio wenye tamaa ya utajiri wa haraka haraka na kutoka kwao wanatafuta wauaji. Kwa maneno mengine, wenye kudhania watatajirika kwa haraka si wauaji bali wenye kutaka viungo hivyo, ambao ninaamini ni wafanyabishara! Wauaji hawa ni watu wanaolipwa na sitashangaa wanalipwa vizuri mno kiasi cha kuweza kuingia nyumba ya mtu na kumkatakata vipande.

Njia pekee ya kuwanasa hawa ni kuhakikisha kuna dau kubwa zaidi pembeni.

Maana yake nini? Maana yake ni kwamba ukiweka fedha kwenye mapambano haya unalazimisha mtu kupima kipi bora.

Je, aende kuua mtu kwa sh milioni 10 wakati endapo akienda kuwatonya polisi na vyombo vya sheria na akaweza kumnatisha huyo mfanyabiashara na mtego ukapangwa na huyo mtu akatiwa mbaroni yeye ananyanyuka na sh milioni 15 ya halali, lipi alichague? Sasa hivi tunawataka watu hawa wasalitiane kwa sababu ya ‘uzalendo' tu.

Hilo halitoshi, kama kweli tunataka kukomesha mauaji haya hatuna budi kuweka fedha pia kwenye mapambano haya. Maneno ya vitisho hayatoshi na kelele za majukwaani hazitoshi. Kutoa matamko ya kulaani hakutoshi.

Kama tunataka kukomesha mauaji haya ni lazima tulipe gharama yake, naam! Hata gharama ya fedha.

Hili linanileta kwenye uamuzi wa kufuta leseni za waganga wote wa kienyeji. Najua serikali imechukua uamuzi huo kwa nia njema. Hata hivyo naamini imefanya kwa kukurupuka na kwa kuongozwa na hisia.

Kwamba, waganga wa kienyeji wote wanahusika kwa namna moja au nyingine na mauaji ya maalbino. Tatizo la hatua hii kwanza imepotoka kwa sababu haiwezekani waganga wote wa kienyeji kuhusika na mauaji ya maalbino. Na pili, haiwezekani kudhaniwa kuwa wote wanajuana na wamekula njama.

Kufuta leseni hizi, serikali na vyombo vya usalama vinakiri kuwa vimeshindwa kupenyeza (infiltrate) kazi hii. Hili halinishangazi kwani yaliyotokea kwenye sekta ya fedha na wizi mkubwa usingeweza kutokea endapo vyombo vyetu vingeweza kupenya humo na kuwa na watu wao.

Nilipofuatilia katika vyanzo vyangu jibu lilikuwa ni hilo hilo.

Chanzo kimoja cha kuaminika sana kimedokeza kuwa tatizo la TISS (Usalama wa Taifa) ni kuwa hakuna fungu la mitaani au limepunguzwa mno.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, fungu hilo la mitaani ndiyo ambalo linatumiwa na vyombo vingi vya usalama kukusanya habari za kijasusi kutoka mitaani.

Kwa kufuta leseni hizi zote serikali inakiri ya kwamba wameshindwa kupenyeza waganga wao wa kienyeji, wameshindwa kuwanunua na kuwaweka kwenye malipo yao waganga hao, na zaidi ya yote wameshindwa kupata wafanyabiashara ambao wangeweza kujipitisha kama wanatafuta wauaji.

Kwa maneno mengine, serikali inathibitisha kile ambacho nimekiandika kwa kirefu mwaka jana.

Usalama wetu wa Taifa unahitaji msaada wa haraka. Bila kuwa tayari kulipa watu katika kukusanya habari, hatuwezi kuzuia vitendo kama hivi. Hivyo jibu bado linarudi kwenye fedha. Sasa tufanye nini?

Naamini serikali inataka kweli kukomesha mauaji ya maalbino. Njia walizozichagua hadi sasa za kauli kali, vitisho, n.k havitoshi kuzuia mauaji haya.

Kunahitajika hatua za makusudi kupambana na uhalifu huu kwa njia za kisheria na si nje ya sheria. Tukikubali kufanya jambo lolote nje ya sheria kwa sababu ya kukerwa, kuchoshwa, kukasirishwa na ‘plight' ya maalbino, hatutendi haki kwa sheria zetu, na kwa hakika tutafungulia utawala wa mwituni ambapo vitendo vya kisasi vitatawala. Mimi suluhisho langu linarudi kwenye pesa na liko hivi:

a. Serikali itenge kiasi kisichopungua sh bilioni moja! Ndiyo nimesema bilioni moja kwa sababu naamini kabisa thamani ya maisha ya ndugu zetu waliouawa inazidi sana kiasi hicho kwa mara nyingi mno kiasi kwamba hakikadiriki.

b. Hivyo kutenga sh bilioni moja ni kidogo tu, kiasi tunachoweza kufanya sisi kama taifa tukizingatia kuwa serikali hiyo hiyo ililala wakati kina Kagoda wanachota sh bilioni 40! Kusema ukweli hata wakitenga sh bilioni 40 hizo kwa ajili ya kupambana na mauaji ya maalbino, binafsi sina tatizo hata chembe kwa kadiri ya kwamba wao na watoto wao hawawi kwenye mkono wa kuzipokea!

c. Kiasi hicho kitengwe katika mafungu mbalimbali kama zawadi na motisha kwa mtu yeyote yule ambaye (1) atafanikisha kukamatwa kwa mtu yeyote anayetafuta viungo vya maalbino, (2) mtu yeyote ambaye anajua mipango ya kumtafuta albino, (3) mganga yeyote ambaye amefuatwa na watu wanaotafuta viungo vya albino.

d. Serikali itenge namba maalumu za simu katika mikoa yote ambapo mtu mwenye taarifa za njama, mipango, au utafutaji wa albino au viungo vya albino ataweza kupiga simu na kutoa taarifa hiyo bila yeye kulazimishwa kujitambulisha.

e. Mtu huyo atapewa neno/alama ya siri ambayo ni utambulisho wake na utamsaidia kupata zawadi pindi habari alizozitoa zikifanyiwa kazi na kusababisha kukamatwa na hatimaye kutiwa hatiani kwa watuhumiwa. Katika kufanya hili iwe wazi kabisa kuwa kuchezea namba hizo kwa kumsingizia "baba mkwe" au "shemeji" na mambo haya ili kumkomoa, kutasababisha adhabu kali kwa mhusika.

f. Ili kuweza kufanikisha (b) naamini msaada wa utaalamu wa PCCB katika kunasa wala rushwa unahitajika. Naamini, PCCB wana utaalamu na ujuzi mkubwa wa kunasa watu kwa mitego hii.

Polisi hadi hivi sasa wamekuwa ni aibu kwa kweli. Kikosi kilichoundwa cha Usalama wa Taifa na wenzao kiongezewe utaalamu wa PCCB.

g. Kwa vile sasa leseni za waganga zimefutwa, serikali ifanye hima kuwaandikisha waganga wa Tanzania bila kuweka ugumu usio wa lazima wa tiba za jadi. Kipimo ambacho kinasemwa kuwa ati hadi dawa zao ziwe zimethibitishwa hospitali ni kipimo kisicho sawa kwani kinaondoa kabisa maana ya tiba za jadi. Imani kwenye tiba za jadi siyo suala la Waafrika tu na tusijione duni kuwa tunazo tiba hizo. Tiba za jadi ziko Ulaya, Marekani, Uchina, na karibu sehemu zote duniani tena Wazungu wao hadi wanajitangaza kwenye ma TV yao. Lakini zaidi ifanye haraka kwa sababu wakichelewa waganga wa nchi jirani wataziba pengo hilo la Tanzania na wauaji wataanza kwenda kwa waganga wa nchi jirani na kuanza kupewa maelekezo hayo. Tutabakia tunashangaa "mbona tumefutia leseni waganga wote lakini bado mauaji yanaendelea"?

h. Katika kuandikisha upya waganga hawa, msisitizo pia uwepo katika kutengeneza mtandao wa kiinteligensia miongoni mwa waganga hawa. Ninaamini kuwa kutokana na kuaminika kwao na nguvu zao katika sehemu mbalimbali waganga hawa wanaweza kutumika siyo katika kukusanya habari za mauaji ya maalbino tu bali pia kuwa kinga ya uhalifu mwingine ambao unapitia kwenye mikono hii ya wataalamu wa jadi.

i. Serikali iongeze fungu la mitaani (street fund) kwa Polisi na TISS ili liweze kutumika kukusanya habari za mitaani kama ilivyokuwa wakati ule wa vita baridi. Kama serikali isingekuwa bahili katika hili nina uhakika ya Richmond yasingefika hapa, ya EPA yasingefika hapa na haya ya maalbino yasingefika hapa. Serikali ingekuwa na watu inaowalipa kutoa habari ambazo ni muhimu kwa usalama siyo za umbea tu. Hofu yangu ni kuwa vyombo vyetu vyaweza kutumika kukusanya habari za wanasiasa na mambo yao kuliko zile za usalama wa nchi. Sitoshangaa kuna mtu yuko serikalini anajiuliza hivi "x,y" ni nani na kama ana mpango wa kugombea ubunge badala ya kukusanya habari za kijasusi kuhusu maalbino! Serikali ikiwa tayari kulipa, itapata habari zozote zile kwani fedha mara zote ni msaliti.


Haya ni mambo machache ambayo naamini yanawezekana kama kweli tunataka kupambana na mauaji haya ya maalbino. Tutaweza kuyakomesha tu kwa kuingiza fedha katikati siyo kwa vitisho vya "jino kwa jino" kwani ukishafanya vitisho hivyo unachofanya ni kuwaambia wauaji waanze kutumia silaha kali zaidi. Matokeo yake Tanzania haitakuwa tofauti sana na Baghdad au Kabul.

Tusikubali hata kidogo kwamba wakati wa matatizo ya kitaifa basi tunaweka pembeni sheria zetu. Tukikubali kuwa kiongozi yeyote wa nchi anaweza kutoa maelekezo ya kuvunja sheria na akaendelea na wadhifa wake bila kukosolewa tutakuwa tumekubali kuleta utawala wa kiimla nchini. Katika kupambana na mauaji ya albino, sisi kama taifa tusikubali kuruhusu mauaji mengine kwa kisingizio cha "kuchoshwa". Tukikubali kuwa wananchi wajichukulie sheria mikononi mwao, tutakuwa tumekubali utawala wa ubabe ambapo wale wanyonge katika jamii, wale dhaifu katika jamii, wale maskini katika jamii ndiyo tutawakuta wakitiwa viberiti kwa kisingio cha kutekeleza maagizo ya mkuu!

Hilo tunalikataa hata kama limesemwa kwa nia njema ya kuuleta ufalme wa Mungu duniani. Sheria zetu lazima zifuatwe wakati wote. Tunakataa kama vile Rais mpya wa Marekani Barack Obama alivyokataa "uchaguzi kuwa ni wa uongo kati ya usalama wetu na tunu zetu tunazozishikilia". Uchaguzi wa aidha kufuata sheria zetu hadi nukta ya mwisho au kufanya mambo kwa sababu ya hisia zilizoumizwa ni uchaguzi tunaoukataa.

Tumetaka kujenga taifa la demokrasia, basi gharama ya kwanza na kubwa zaidi ya utawala wa aina hiyo ni gharama ya kufuata sheria. Tukielekeza macho yetu pembeni, ni bora tujitangaze kuwa ni ufalme wa kiimla wa kundi la watu wachache.
 
Cuzin hivi ni kweli hata watu Tanzania bado wana believe in vodoo..at first i thought its only west Africa.How could you kill somebody kwa kisa cha kujitafutia utajiri?.

Huo ni unyama kwa kweli i think kama wakaandamana huko tanzania na kupinga hiki kitu hakitaendelea na hao watu wakamatwe na wahukumie kunyongwa maana hiyo ni first degree murder tena kwa kujitakia na wala siyo involuntary.

Its sad indeed to see how people could be that evil (ivo) huo ni uuaji wa kinyama kabisa kwa kweli cuzin hata mimi napinga kabisa.Me personally naona hao wanaojifanya waganga wa jadi wafungiwe hizo leseni zao (endapo wana leseni) na hao watu wanaokwenda kwa hao waganga na kutafuta utajiri that is unkunguful.


albino1.jpg
Naamini kila mtu mwenye akili timamu, kutoka ndani hata nje ya Tanzania lazima anaguswa kwa namna ya kipekee kabisa na Mauaji ya Albino ambayo yamekuwa yakiendela kwa miaka kadhaa sasa. Matukio haya yanatia uchungu zaidi pale yanapohusisha kundi la watu wanyonge, kundi la watu wenye mahitaji maalumu ambao walihitaji uangalizi na ulinzi wa hali ya juu.

Watanzania wenzangu na WanaJF wenzetu Albino ni watu wanaohitaji zaidi uangalizi upendo wa kila mmoja wetu, kwa zaidi ya miaka kumi sasa tangu kuanza kwa matukio haya wengi tumekuwa tumeweka matumaini yetu kwenye kauli nyingi za kisiasa na za kiutawala kutoka kwa viongozi wetu na kuamini mauaji haya yatamalizwa na vyombo vyetu vya usalama vyenye ustadi wa hali ya juu.

Ndugu zangu, Mambo hayapo kama tulivyofikiria, Hali ya vyombo vyetu vya usalama kila mmoja anaitambua, sio jambo la kulizungumzia, Kauli za viongozi wetu wa nchi hazina sapoti ya kimantiki kwenye utendaji,

Zaidi ya miaka 8 sasa albino wanaishi kama tembo wa serengeti hawajui wapi watanyofolewa kiungo gani, hawajui muda gani watapoteza uhai, hawaoni nia ya dhati ikiwa kwenye utekelezaji wa maadhimio ya kuwalinda.

Back to the point, Je! ni sawa kuendelea kuitupia madongo serikali, kwamba imeshindwa kuzuia mauaji ya albino? tuendelee kulaumu, na kuumia kuona wenzetu wanapoteza maisha?

Hapana, tunaenda kwenye uchaguzi na tunajua matukio haya yatazidi kuwa mengi, we have to take Action kama raia, kama wafanyakazi na wakulima we have to take a very strong and Effective action which will assure that,

kwanza hakuna Albino mwingine atakayekufa, lakini pia mizizi ya mauaji haya inangolewa, na kila aliyehusika awe mwanakijiji, awe mganga, awe mwanasiasa, wote wanawajibishwa. JamiiForums imeshafanya mengi kwenye maendeleo ya hii nchi, but now we have to move to the next buttle to serve our brothers life.

Mimi nimewaza njia moja tunayoweza kuitumia kama community, lakini naamini hapa kuna watafakuri kuntu wenye uwezo wa kutoa njia tunayoweza kuunganisha nguvu za pamoja kumaliza ushetani huu na kuufanya uwe historia kwenye nchi yetu.

Mapendekezo: Tutengeneze kikosi cha watu hata watano kutoka hapa jukwaani kiende kikafanye upelelezi wa kina juu ya matukio haya. Naamini maGreatthinker kama watu8, maundumula, the boss. wanaweza kabisa kufanya upelelezi wa Ki-FBI na kutuletea majina ya kuanzia, nani anaua, nani anatumwa kuua na nani ni mteja wa mwisho wa mauaji haya.

Hapa jukwaani tuchangishane hela za kutosha ili kufinance zoezi zima.

Wana JF jaribuni kupendekeza njia zingine hapa ambazo tunaweza kuzitumia kumaliza hili tatizo tuache unafki wa kutangaza tunaumia bila kuchukua hatua yoyote, Wakati wenzetu wanakufa na sisi tumekaa kimya bila kuchukua hatua yoyote wote tunakuwa wauaji, kama hujashiriki kuzuia basi ni mshiriki wa kutekeleza full stop.

Tukae kimya, leo zamu ya albino kesho utaambiwa zamu ya watu wenye vipara, wajomba zetu baba zetu hawatapona, mtondogoo watasema wenye mvi, mimi na wewe hatutapona.

Pendekeza njia gani tutumie kumaliza tatizo hili kabla mauaji zaidi hayajatokea.
 
Albino Mwanza waandamana kupinga Mauaji ya Maalbino;-

Wakati nasikiliza kipindi cha Dira ya Dunia katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC nimesikia habari hii ya Chama cha Albino mkoa wa Mwanza kufanya maandamano ya kuunga mkono mkono juhudi za serikali katika kupambana vita dhidi ya mauaji ya Albino.

Maandamano hayo yalihudhuriwa na watu kutoka kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali,wa dini,taasisi mbalimbali na wananchi wa kawaida.

Akiongea katika maandamano hayo kaimu sheikh mkuu wa mkoa wa Mwanza Sheikh Hamis Almas alishauri sheria ya kiislamu itumike kuwahukumu wale wote wanaojisughulisha na mauaji ya Albino,kauli ambayo iliungwa mkono na watu wengi waliokusanyika katika maandamano hayo,Sheikh Almas alisema:

"Mungu atajalia tutawakamata watu hawa,wakikamatwa ni kuwaleta stendi kama tulivyofika hapa,wanawekwa juu ya jukwaa,ndio Uislamu huo,inapigwa Risasi watu wote wanaona,na hivyo ndivyo itakavyokuwa kukomesha hilo".

Kwa upande wake Katibu wa chama cha Albino mkoa wa Mwanza bwana Mashaka Enos alisema(katika maandamano hayo) kwamba wale wanaolaani au kutetea watuhumiwa wa mauaji hayo kwa kudai kuwa kufanya hivyo ni kinyume za haki za binadamu ni vema kuangalia pande zote,"Tunapenda kuwaeleza wale wote wenye mawazo ama mtizamo huu kuwa mauaji haya ya Albino nayo pia ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" alisema Katibu huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dk. Alex Msekela YeYe amesema kuwa serikali haitawavumilia wauaji hao wanaodhani kuwa watatajirika kupitia njia hiyo ya mauaji,Dk.Msekela alisema: "Hatudhani na hatutegemei kwamba mmoja wetu atadhani njia yake ya maisha bora iko katika shingo ya mwenzake,mguu wa mwenzake,mkono wa mwenzake,hatutalivumilia hilo"

Kuhusu wazo la kuanzisha Mahakama maalum ya kushughulikia kesi za mauaji ya Albino Dk Msekela alisema kwamba(kwa maoni yake) utaratibu uliopo wa Mahakama unatosha.

Katika maandamano hayo binti Albino HAJRA SADRU alisema kwammba hana kabisa hamu ya kuwa na rafiki wa kiume,"Kwa upande wangu mimi hata mtu akija kunitongoza sitoamini kama ana mapenzi mema,kwa sababu nitaogopa atakuwa anakuja kuniua na vilevile hata akiniua nikafa atafukua kaburi langu kwa sababu juzi nimesikia wamefukua kaburi la Albini huko Bunda,kwa hiyo na mimi nina hofu kuwa hata kama mtu ana mapenzi mema atashawishika au mwingine anakuja kwa njia ya hivyo" alisema binti huyo Albino.

Mkoa wa Mwanza ndiyo unaongoza kwa mauaji ya Albina yaliyojitokeza takribani miaka mitatu iliyopita ambapo hadi hivi sasa watu(ALBINO) 32 wamekwishauawa.

Habari hii ni kwa mujibu wa ERICK DAVID NAMPESYA wa BBC,Mwanza
 
Naona Pinda ameanza kwa kuadopt mtoto Albino..je viongozi wengine nao waadopt watoto maalibino kama Pinda!

Je hili ni moja ya jawabu?

Nakosa uhuru katika nchi yangu, wananiwinda waniue, nimekua sina amani katika moyo wangu, giza linapoingia nakua na mashaka na maisha yangu.

Nafungiwa kama mfungwa eti kulinda usalama wangu, nakosa uhuru wa kujumuika na wanajamii wenzangu, nashindwa kutimiza ndoto zangu kwa kuhofia maisha yangu.

Namhofia hata baba yangu anaweza kuniua na kuchukua viungo vyangu mama yangu ndio tumaini langu,serikali hainijali, jamiii nayo imenitenga yena inataka kuniua.

Mimi albino nikimbilie wapi ili niishi kwa amani na upendo.
Mimi albino naitaji kuishi kama wewe.
Mimi albino naitaji kutimiza ndoto zangu kama wewe.
Mimi albino naitaji kuwa huru kama wewe.
Mimi albino naitaji kupata elimu bora kama wewe.

Tumekuwa na kilio cha muda mrefu,juu ya mauaji ya hawa ndugu zetu walemavu wa ngozi(ALBINO),wengi wamesema mengi,wengi wamelaani,wamelia pamoja na wanaolia(ALBINO),wamehuzunika nao,wapo waliosema ni bora kukimbia nchi,n.k.

Lakini leo mimi nimeona nije hapa na USHAURI wangu kwa SERIKALI,Japo baadhi ya mapendekezo yaweza kuwa ni magumu,lkn basi serikali iyachukue yale yanayowezekanika.

1.Serikali itenge maeneo maalumu ktk kila mkoa hapa nchini kwaajili ya makazi ya ALBINO,Aidha viwekwe vyombo vya ulinzi maeneo hayo kwaajili kuangalia usalama wao,aidha serikali kupitia bajeti yake iweke vifaa maalumu kwaajili ya kuwanasa watu wanaowanyemelea ALBINO,ktk maeneo yao.mfano wa vifaa hivyo ni RADA.

2.Serikali irudishe jeshi la Sungusungu,ambao watakuwa wakizungukazunguka usiku na punde watakapomwona mtu asiy
e wa kawaida ktk hali inayoleta mashaka,basi wamweke chini ya ulinzi na kuhakikisha kuwa wanamchukua maelezo.

3. Serikali ifanye sensa ya mara kwa mara ya ALBINO wote nchini na kisha kuwapa huduma ya mawasiliano kwa vyombo vya Dola,ili waweze kutoa taarifa za haraka pale wanapobaini njama za watu wabaya dhidi yao.

4. ALBINO,wenye sifa za kumiliki silaha kadiri ya sheria na taratibu za nchi waruhusiwe ili wajilinde,km ambavyo baadhi watu wanavyoruhusiwa kumiliki silaha kisheria.

5. Serikali iingize ktk mitaala ya shule za misingi,sekondari hadi vyuo,Somo linalohusu ALBINO,kwanini wako hivyo,na
kwamba wao ni binadamu wenzetu hatuna utofauti mwingine zaidi ya rangi;Aidha watu waelimishwe kuwa hakuna ma
husiano yoyote kati ya Viungo vya Albino na kufanikiwa kimaisha,wanafunzi wafundishwe kuwa mafanikio huletwa
kwa kufanya kazi kazi kwa Juhudi na Maarifa,Elimu ya ujasiriamali itiliwe mkazo tangu elimu ya msingi hadi sekondari,
hii itasaidia kuua fikra potofu zilizokwishajengeka miongoni mwa wanajamiii.

6. Serikali iunde chombo maalumu kitakachofatilia Nyendo za waganga wa jadi,Aidha serikali ifanye sensa yao na kuha
kikisha kuwa usajili unafanyika,kisha kufatilia ktk kazi zao.

7. Serikali iunde mahakama maaalumu itakayoshughulikia kesi za wauaji ya ALBINO,Kesi hizo ziendeshwe kwa haraka na Adhabu kali itolewe kwa watakaobainika kuhusika ili kuwa fundisho kwa watu wenye tabia km hiyo ya uuaji.

8. Mitandao ya simu kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi itoe taarifa za haraka pale inapobaini kuwepo kwa mazungu
mzo yanayoashiria kuwepo kwa maandalizi ya kutendeka kwa uovu unaoonyesha kuwa kuna mpango wa kumwua
ALBINO.

9. Serikali iwachukulie hatua kali za kisheria na kinidhamu watumishi wa vyombo vya Dola wanaoshirikiana na wahalifu
ili kuvuruga ushahidi wa kesi za mauaji ya ALBINO mahakamani.

10. Kama miongoni mwa wahusika wa mauaji ya ALBINO,ni viongozi wa juu wa Serikali au Wanasiasa ama Viongozi wa dini,basi uchunguzi wa kina ufanyike na kisha kuyataja majina yao hadharani,na hatua kali za kisheria zichukuliwe.

11. Kuwepo utaratibu utakao ratibiwa na mabalozi wa nyumba kumi wa kubaini wageni wanaoingia na kutoka ktk makazi
ya wananchi vijijini na mijini,na kujua taarifa zao kiundani,hii itawezesha kuwatambua watu wema na wabaya.Jambo
lihusishe na vyombo vya ulinzi vya eneo husika.

12. Serikali iwaingize baadhi ya ALBINO wanataaluma,wenye weledi(naamini wapo),ktk vyombo vya Dola,km vile Maha kama,ili kuchochea ufanisi wa kesi zinazohusu mauaji ya ALBINO.

Ninaomba kuwakilisha,na karibuni kwa maoni,nipo tayari kurekebishwa,pale nilipopotoka,ili niweze kwenda ktk mstari.
 
Naona Pinda ameanza kwa kuadopt mtoto Albino..je viongozi wengine nao waadopt watoto maalibino kama Pinda!

Je hili ni moja ya jawabu?

Sidhani kama tatizo la albino ni kukosa mahali pa kuishi. Tatizo lao ni usalama. Sasa kama Waziri akichukua watoto wote, kila afisa wa jeshi la polisi na wale wenye ulinzi wakifanya linaweza kuwa suluhisho. Kuna maalbino karibu laki moja na hamsini elfu hivi.

New+Document.jpg

10349156_840543802703306_4036374653500467270_n.jpg


kp23022015.jpg


Rais Jakaya Kikwete kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi amezungumzia tatizo la mauaji ya albino, akisema Serikali imelipa uzito mkubwa suala la kudhibiti na kukomesha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au kukatwa baadhi ya viungo vyao wenyewe wakiwa hai.

Akionyesha kuguswa na uhalifu alisema Serikali imefanya hivyo bila ya kuchoka tangu tukio la kwanza baada ya yeye kuingia madarakani Aprili 17, 2006, kule Nyahunge, Geita alipouawa Alfa Amon ambapo watuhumiwa wawili waliuawa na raia. Mwaka 2007 kulikuwa na matukio saba. Mwaka 2008 ndiyo ulikuwa mwaka mbaya sana walipouawa watu 18.

Tunaungana na Rais Kikwete katika jitihada zake za kulimaliza tatizo hili la wenzetu albino kuishi kwa hofu. Hatuna shaka na kauli ya Rais, ila tunaviomba vyombo vya dola vimsaidie kiongozi wa nchi katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo na wananchi nao wasaidie kwa upande wao.

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema akiwa mkoani Mwanza, aliwahi kunukuliwa akisema Jeshi la Polisi limetenga Sh20 milioni kwa ajili ya kuwazawadia watu watakaotoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa albino.

Hatuna hakika kama mbinu hiyo ya Mwema hadi anaondoka madarakani ilikuwa imefanikiwa kwa kiasi gani, na je, mrithi wake anaendelea nayo au zilikuwa juhudi binafsi ambazo haziko kimaandishi. Pia, hili linakuwa gumu kufahamu utekelezaji wake kwa kuwa hakuna utaratibu wa kutoa mrejesho kwa wananchi hasa kwa masuala mazito yanayowahusu kama mauaji ya albino. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu naye wakati wa uongozi wake aliwaomba wananchi, asasi za kiraia, viongozi wa dini na wanasiasa kutoa ushirikiano kwa Jeshi Polisi waweze kukamata mtandao wa watu wanaojihusisha na mauaji ya albino.

Kamanda Mngulu alifikia hatua ya kuwataka wananchi kupiga simu namba 0755,785,557 za Makao Makuu ya Polisi kwa ushirikiano zaidi. Juhudi hizo za Mngula hadi anaondoka katika nafasi hiyo hakuna mrejesho kwamba zilifanikiwa kwa kiasi gani, na je, aliyemrithi anaendelea nazo au ulikuwa mkakati binafsi ambao haukuwapo hata kimaandishi.

Sote tunajua Jeshi la Polisi lina Kitengo cha Kiintelijensia. Kitengo hiki kimekuwa maarufu sana katika kunasa taarifa za vyama vya siasa vya upinzani na wanaharakati, siku zote wakuu wake wamekuwa wakijitokeza kuwazuia wanapotaka kupinga jambo serikalini kwa maelezo kwamba taarifa za kiintelijensia zinaashiria kuvunjika kwa amani.

Tungependa kuamini kwa dhati Rais Kikwete ana dhamira ya kweli ya kupambana na wauaji wa albino, lakini vilevile tunaamini vita hii hawezi kushinda pekee yake bila ushirikiano kutoka kwa vyombo vya dola na wananchi.

Ni ukweli usiopingika kwamba ile nia ya dhati ya DCI mstaafu Mngulu ya kutoa hadharani namba za simu za Makao Makuu ya Polisi na zawadi iliyotangazwa na Mwema, zililenga kutaka ushirikiano wananchi.

Tunatoa rai kwamba azma ya Rais Kikwete inafaa kuungwa mkono kwa vitendo, vyombo vya dola kwa kutumia idara zao nyeti wafanye kazi kwa kujituma kuwabaini wote wenye nia ya kuwatendea maovu albino, pia wananchi wawe wa kwanza kuwa walinzi wa ndugu zetu albino. Kwa kufanya hivyo vita dhidi ya wauaji wa albino inawezekana.


Chanzo: MAONI: Tumsaidie Rais kudhibiti na kukomesha mauaji ya albino - Swahilihub - mwananchi.co.tz
 
Sidhani kama tatizo la albino ni kukosa mahali pa kuishi. Tatizo lao ni usalama. Sasa kama Waziri akichukua watoto wote, kila afisa wa jeshi la polisi na wale wenye ulinzi wakifanya linaweza kuwa suluhisho. Kuna maalbino karibu laki moja na hamsini elfu hivi.

Je hii takwimu ni mwaka gani? Na mgawanyiko wake upo vipi? (watu wazima na watoto) geographical location yao pia ni vipi (kwa kila mkoa kama sio wilaya na kijiji).
 
Mwanakijiji.......mchango murua kabisa mkuu..........lakini.....hivi unafikiri hivi vyombo vyetu vimeshindwa kabisa kupata suluhisho la matatizo ya albino...........no......i personnaly don't believe that......kutakuwa na upuuzi mwingi tu unaendleea ndani ya vyombo vyetu vya usalama..........

.......tena kwa taarifa yako umewapa wazo la ulaji........weee subiri utaona.........

.......uankumbuka kile kilio cha jamaa wa PCCB kupunguziwa bajeti ya allowances za operations huko mikoani...........now we are paying.......
 
....electronic chip zenye GPS zinaweza kuwasaidia usalama hawa ndugu zetu,zinawekwa under the skin,very small like grain of rice,akipata shida tuu anabonyeza then usalama watajua yuko wapi,its money lakini inasaidia,vile vile community wanazokaa najua kuna mgambo/raia wema na police kila kona kwa hiyo kunaweza kuwa na some arrangement za kuwapatia security hawa ndugu zetu....education against this barbaric nayo itasaidia sana,na incentive za pesa nyingi za kuwataja wanaohusika zinaweza kusaidia pia.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

TUNAWEZA kukaa chini na kukubali mapendekezo ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, juu ya vita dhidi ya mauaji ya maalbino au kuyakataa; tunaweza kukubali kuwa waganga wote wa kienyeji wafutiwe leseni zao kwa kudhaniwa kuhusika na uhalifu au kukataa; tunaweza tukakubali waziri mkuu aseme maneno ya kichochezi na yenye kuhatarisha amani nchini au kumpinga. Yote yamo ndani ya uamuzi wetu na ndani ya uwezo wetu.

.

Mawazo Mazuri,
Je watakusikiliza?ulishawahi kutoa Pendekezo kama hili MWanzoni kabla mauaji hayajapamba moto na ukawa umeandaa mchango wako wa laki tano.Hivi walikutafuta?

Mie hapo ndipo huwa nashindwa kuelewa,kwanini serikali yetu haitaki kukubali mazuri wanayoambiwa
 
Mkuu Mwanakijiji, nimesoma kwa makini sana post yako hapo juu, ambayo inaelezea tatizo la kuuawa Albino na solution unayoona inaweza kusaidia kukomesha tatizo lenyewe.

Mkuu naomba uniruhusu kusema yafuatayo;

Kwa maoni yangu, pesa haziwezi kusaidia sana kutatua tatizo lililopo. Nasema hivyo kwasababu, kwa kutumia pesa, watu wengi sana wanaweza kusingiziwa kujihusisha na kutafuta viuongo vya ndugu zetu hawa, na hivyo kusababisha matatizo makubwa zaidi. Ni kweli kuwa pesa zinaweza kufanya watu kuchukua hatua za ajabu. Ni uwezo huo huo wa pesa unaoweza kusababisha watu kuhukumiwa kwa hisia tu, ama kwa kuwa mshitaki ameishiwa pesa na ni lazima azipate kutoka katika mfuko uliopo. Mkuu, tumeona pia jinsi gani serikali inavyopata tabu na watumishi wenye uchu mkubwa wa pesa. Pesa kama hizo pia zinaweza kuishia kwa kiasi kikubwa mikononi mwa watu waliopewa dhamana ya kuzisimamia, kwa kuwa hata usimamizi wake itabidi utungiwe sheria na Bunge. Hili suala haliwezi kusubiri muda wote huo. Sheria zipo, na zinatumika. Zitumike pia kuwalinda Albino kama zinavyotumika kwa watu wengine wote.

Mkuu, Mimi sioni umuhimu wa wapiga Ramli. waganga wa tiba za asili nadhani ni muhimu kuchujwa na kupewa leseni mpya mapema iwezekanavyo. Nadhani hatua hiyo ya kufuta leseni zote, ni sahihi mpaka hapo serikali itakaporidhika kuwa waganga hao kweli wanastahili kuendelea na shughuli zao. Inabidi pia kuwa na regulation ya kisheria ya waganga wa namna hiyo. Maana walikuwa wana-operate kiholela mno.
 
Na viongozi WOTE ambao katika jimbo eneo lao anauawa albino wawajibike. Watoe maelezo ya kina ya kwa nini aliuawa na wakionekana hawakuchukua hatua dhabiti kuzuia mauaji hayo, waadhibiwe.
 
mapendekezo kama haya yana maana watu wafanye kazi kweli kwa kufuata sheria.. sasa kufuata sheriia ni vigumu sana kama huna viongozi wanaopenda utawala wa sheria.
 
Na viongozi WOTE ambao katika jimbo eneo lao anauawa albino wawajibike. Watoe maelezo ya kina ya kwa nini aliuawa na wakionekana hawakuchukua hatua dhabiti kuzuia mauaji hayo, waadhibiwe.

Mimi niko interested zaidi na kuwa severely punish the perpetrators. Kwenye mambo kama haya, kwa maoni yangu, tunahitaji jitu au mijitu kadhaa yenye hulka ya udikteta kukomesha mauaji kama hayo. Jitu ambalo litafuata sheria to the letter na ambalo halitakuwa na huruma wala suluhu yoyote ile kwa wauaji hao.
 
mapendekezo kama haya yana maana watu wafanye kazi kweli kwa kufuata sheria.. sasa kufuata sheriia ni vigumu sana kama huna viongozi wanaopenda utawala wa sheria.

Ni binadamu wachache wanaopenda kufuata sheria. Kinachotuzia wengi wetu ni uhakika kuwa tutakamatwa na tutaadhibiwa. Vile vile kiongozi bila kumhakikishia kuwa atakuwa answerable kwa pungufu lolote anakuwa mzembe. Ndiyo maana naamini kuwa wakibanwa na kuonyeshwa kuwa uongozi si free ride ndipo tutaanza kupata matokeo. Kwa wenzetu jambo kama hili likitokea basi wale walio kwenye mamlaka ni wakwanza kubanwa. Ndiyo uwajibikaji. Naamini kama viongozi kuanzia wale wa tarafa na mapolisi wakiwajibishwa kila pakitokea mauaji au ukatwaji wa viungo basi vitendo hivi vitapungua!
 
Mwanakijiji umekuja na wazo zuri sana, tena sana ambalo nafikiri viongozi wetu wangekuwa hata na utashi wa kuchukua mazuri toka kwa wengine walio nje yao basi leo tungekuwa mbali sana.

Tatizo langu kubwa ni credibility ya vyombo vyetu vya usalama hasa watendaji ambao nao huwa wanasaliti wananchi kwa ajili ya "PESA", Nina uhakika kabisa vyombo vyetu vinawajua wanaohimiza mambo haya, mbona wamekuwa ni wepesi sana kufichua mbinu yoyote inayofanywa kuihujumu serikali?

Baadhi ya wanausalama wetu wapo kwenye payroll ya majambazi/wahalifu na pia nina imani hata hawa wauaji wa albino pia wamewatia mfukoni wana usalama wetu hasa POLISI. Suala la Taarifa lisihusishe POLISI nashauri JWTZ tena Rank ya Kina Mwamunyange ndiyo wapewe jukumu hili la kuprocess simu za siri, yaani kila kwenye albino kuwe kuna mlinzi wa siri anayelipwa vizuri Toka JWTZ ambaye hata wanafamilia wa Albino hawamjui. Hawa jukumu lao liwe ni kupokea Taarifa Toka Central Command kwa kina Mwamunyange type na kufuatilia issue yoyote ile on the ground.

Na hawa makomandoo walipwe vizuri hasa. Hii program iwe ya miaka mitatu tu. Baada ya hapo warudishiwe polisi, Nakuhakikishia hapo watakamatwa wote na kama si kukamatwa basi kama kuna dawa za kuchanganya na viungo vya albino zitakuwa outdated, kwani watafanya research ya kutumia vitu vingine.
 
Kwanza viongozi(wanasiasa) waache imani za kishirikina...mengine baadae
 
Kwanza viongozi(wanasiasa) waache imani za kishirikina...mengine baadae

Viongozi wataachaje imani hizo kama wao ni reflection yetu sisi wenyewe wananchi....?

You know, people can say what they want about Mzee Es, but he nailed when he said that.....
 
Viongozi wataachaje imani hizo kama wao ni reflection yetu sisi wenyewe wananchi....?

You know, people can say what they want about Mzee Es, but he nailed when he said that.....
Unasemaje juu ya hoja za mchambuzi huyu
Njia pekee ya kuwanasa hawa ni kuhakikisha kuna dau kubwa zaidi pembeni.

Maana yake nini? Maana yake ni kwamba ukiweka fedha kwenye mapambano haya unalazimisha mtu kupima kipi bora.

Je, aende kuua mtu kwa sh milioni 10 wakati endapo akienda kuwatonya polisi na vyombo vya sheria na akaweza kumnatisha huyo mfanyabiashara na mtego ukapangwa na huyo mtu akatiwa mbaroni yeye ananyanyuka na sh milioni 15 ya halali, lipi alichague? Sasa hivi tunawataka watu hawa wasalitiane kwa sababu ya ‘uzalendo’ tu.

Hilo halitoshi, kama kweli tunataka kukomesha mauaji haya hatuna budi kuweka fedha pia kwenye mapambano haya. Maneno ya vitisho hayatoshi na kelele za majukwaani hazitoshi. Kutoa matamko ya kulaani hakutoshi.
 
Ndiyo maana naogopa kwenda kugombea ubunge wa Njombe vijijini 2010.. kwa sababu ya ushirikina wa viongozi wengine ambao wanakesha kwa waganga wa jadi kupiga tunguli...hebu anngalia walivyo mkolimba my sista Amina Chifupa...tatizo Amina alikuwa anatoa kitu na box wakaona mmh ngoja tumfundishe adabu wakampa kichaa...mtu gani anaumwa ghafla bin vuu?..wee ngoja baba yake Amina kasem aanawasomea al-badili.
 
Back
Top Bottom